Dr. Kigwangalla: Ufafanuzi wa kauli yangu ya "Kutoka Nje ya Box"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg

AJIRA KWA VIJANA: MAELEZO YA MTAZAMO WA DKT. KIGWANGALLA.
___________________________________________________________
Nimeanzisha utaratibu wa kuandika jumbe zenye kuhamasisha mabadiliko ya kifikra kwa vijana wa nchi yetu. Sababu ikiwa ni imani yangu kubwa kwamba hizi ni zama zetu kuchukua majukumu ya kuongoza mageuzi kwenye kila eneo la maisha ya jamii yetu. Kwenye siasa. Kwenye sanaa. Kwenye biashara. Kwenye kilimo. Kwenye tafiti. kila kona.

Katika moja ya maandiko yangu kwenye ukurasa wangu wa Twitter (HKigwangalla ) niliandika ujumbe wenye lengo la kuwaamsha vijana wahitimu wa vyuo kufungua bongo zao na kutoka nje ya box ili wazitambue fursa na watumie vipaji vyao kubadili hali zao na za Taifa kwa ujumla. Ujumbe huu haukueleweka.

Jambo moja zuri na la uhakika ni kwamba ujumbe ule umefikisha lengo kwa wahusika. Umezua mjadala. Naamini hii ni hatua muhimu sana kwenye mawasiliano. Suala la ajira ni lazima tulijadili. Maana halikwepeki. Ajira ni maisha yetu.

Bahati mbaya sana ni kwamba tukisema 'ajira', kila mtu haraka haraka anawaza ajira ya benki, serikalini, kiwandani nk. Tulipofikia hizi hazitoshi, na tunakoelekea kutakuwa na janga la kitaifa la watu kukosa mahala pa kujishikiza ili kupata kipato chao cha kujikimu. Ni lazima tuwe wabunifu, kama nchi, tujiandae.

Utafiti wa NBS wa mwaka 2014 unaonesha ni watu 2,141,351 tu (takriban 4.3%) wa Tanzania bara walioajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi. Na ongezeko la ajira rasmi kutoka mwaka 2013 mpaka 2014 lilikuwa ajira 282,382 tu. Na kwamba sekta isiyo rasmi inaajiri watu wengi zaidi kuliko sekta ya umma. Pia, 61.1% ya vijana walio kwenye umri wa kati ya miaka 15 - 24 wameajiriwa kwenye sekta binafsi. Lazima tujiulize kwa mwaka tunazalisha wahitimu wangapi kwenye fani zote, na viwango vyote vya elimu, kuanzia Cheti mpaka Shahada? Pia tuna fungu kiasi gani la mishahara kiasi cha kutoa ajira kwa wote wanaohitimu? Muajiri mkubwa ni sekta binafsi, ambaye ameajiri 67% ya wote wenye ajira nchini.

Mfano rahisi kwangu ni mfano wa wahitimu wa taaluma ya udaktari. Kwa mwaka wanahitimu takriban madaktari 1300, uwezo wa kuajiri ni madaktari kati ya 300 - 500 (kwa sekta zote za umma, hiari na binafsi). Hawa wengine wanaenda wapi? Nini kifanyike? Majibu yake yapo kwenye 'kujiajiri' na kuzalisha fursa mpya za ajira.

Sekta ya umma hufika mahali ikakoma kuajiri kwa kipindi fulani, sababu haitanuki. Inabidi kukuza ajira kwenye sekta binafsi. Ni lazima tuongeze uzalishaji. Ni lazima tufanye kazi ili tuzalishe ajira. Ndiyo maana Serikali ya CCM ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli inahamasisha ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Kuna watu wanadhani serikali itajenga viwanda ili wao wakapate ajira. Kuna wengine wanadhani suluhu ya kujenga uchumi wa viwanda basi ni kuwapa mitaji wasomi waliohitimu vyuo vikuu. La sivyo hawawezi kujiajiri. Kuna watu wanaamini kuwa ili wajikomboe kimaisha ni lazima serikali iwabebe, iwaajiri ama iwape mitaji. Mimi nadhani hizi ni fikra potofu miongoni mwa vijana wetu. Ndiyo maana nimeanza kuwahamasisha wafikirie 'nje ya box'. Wafikirie kubuni miradi itakayotatua changamoto mbalimbali kwenye jamii, na kwa kufanya hivyo watakuwa wamejiajiri na wataajiri wengine.

Kuna mambo mengi sana kwenye kufikia kuwa na kizazi cha watu wabunifu wenye uwezo wa kujiajiri na kuajiri wengine, kubwa ni kuwa na msingi kwenye mfumo wetu wa elimu, kwamba uwaandae vijana kufikiri kibunifu zaidi na kijasiriamali kuliko kufikiri kwa 'soma kwa bidii shuleni, faulu, pata digrii, nenda kapate ajira nzuri'. Na pia kuwa na mifumo inayowezesha na kurahisisha vijana wetu wabunifu na wajasiriamali kutambuliwa, kuendelezwa, na kuungwa mkono kwenye kazi zao za kibunifu, ikiwemo kuwezeshwa.

Kwa hali ilivyo sasa, naamini tunahitaji kuwa na vijana wajasiri, wabunifu na wenye kuchukua hatua za kubeba 'risk' za kila aina kuanzisha shughuli mbalimbali za kimageuzi kwenye biashara, kilimo, sanaa, jamii nk. Ni lazima vijana wetu waote 'ndoto' kubwa za mafanikio, watamani mambo makubwa, watamani mafanikio, wavutiwe na mafanikio ya wenzao; wajitoe kufanyia kazi mawazo yao, wabadilishe hali zao - watoke kwenye kundi la kulalamika na kulaumu, waingie kwenye kundi la wenye kuchukua hatua za kuishi ndoto zao. Kundi la ambao wataendelea kulaumu, kulalamika na kumtafuta mchawi wa maisha yao litabaki na watu wengi kwa hakika - na hawa wataajiriwa na kundi (dogo) la wale watakaohamasika kuota vitu vikubwa na kuziishi ndoto zao.

Mimi niliishi ndoto yangu - kuja kuwa Daktari. Mbunge. Mjasiriamali. Na leo nimepewa heshima ya kuwa Naibu Waziri kwenye Serikali. Njia yangu haikuwa rahisi. Nilizaliwa Hospitali ya Maweni Kigoma, Baba yangu akiwa mtu msomi akifanya kazi benki ya NBC pale Kigoma, na mama yangu akiwa Mwalimu wa shule ya msingi. Ingetarajiwa niwe na maisha mazuri utotoni na hata ukubwani.
Sababu ningeandaliwa kila kitu na wazazi. Haikuwa hivyo. Baba na mama waliachana (sababu hazinihusu) nikiwa na miaka kati ya minne na mitano, niliishia kurudishwa kijijini kwao baba (Goweko, Tabora) nikiwa na miaka minne/mitano hivi. Nikachunga sana ndama na mbuzi, nikaugua Surua nk. Mdogo wangu alifariki kwa ugonjwa na kupungukiwa damu. Nikabaki peke yangu. Nilienda shule bila viatu, kwa kushona viraka. nk.

Maisha yangu yote ya utoto yalikuwa ya kuhangaika chini ya ulezi wa bibi, babu, na mama yangu. Niliishi utoto wangu kwa kula mlo mmoja (wakati mwingine uji tu) , tena wa chumvi. Fagio la chuma lilipitia ajira ya mama yangu, na alilazimika kufanya biashara ya mama ntilie ili kutupatia mahitaji yetu muhimu. Niliuza jerebi, samaki, vitumbua na mihogo na karanga mitaa ya Nzega. Vijana niliokua nao wapo na ni mashahidi wa hili. Nilipona kifo kwa njaa ya mwanzo wa miaka ya 80.
High school, nilisoma ShyBush, ambapo kulikuwa hakuna walimu wa kutosha. Niliporudi likizo, nililazimika kuazima notisi za rafiki zangu akina Joseph Pius Mwami (leo hii Mhandisi) na nilizinukuu usiku kucha bila kufumba macho, chumbani kwangu ambapo kulikuwa hakuna umeme, nilisoma kwa kibatari. nk.

Nimepata Digrii ya Udaktari. Ubingwa wa Afya ya Jamii, Uongozi na Usimamizi wa Biashara nk. Nimeanzisha kampuni, zikakua mpaka kufikia kuzungusha zaidi ya bilioni 7 kwa mwaka. Nimekuwa Mbunge nk. Yote haya si katika mafanikio makubwa ninayoweza kusema najivunia. The biggest success ever in my life has been to achieve 'self-recognition' (kujitambua!). Kujua nguvu na uwezo wangu, kujua nina kusudi gani maishani na kutenda yanayopaswa kutendwa.
Ukijitambua utafika mbali. Ukikuta milango imefungwa utapita hata dirishani. Ukijitambua hushindwi kitu. Kujitambua kwangu kumenifanya nione kila kitu kinawezekana, maana kama mimi na historia yangu, leo hii nimeweza kuwa Daktari, nk, nini sasa kitanishinda?

Mimi baada ya kuhitimu masomo yangu ya digrii ya kwanza ya udaktari, nilianza internship, wiki 3 kabla ya kumaliza nilisimamishwa kazi sababu ya mgomo wa madaktari wa mwaka 2005. Kila tulipoenda tulikuwa hatuajiriki! Niliamua kuanzisha kampuni (pamoja na rafiki zangu wawili - wote graduates.) Niliachana kabisa na habari za kusaka ajira, nikaamua kuwa mjasiriamali, mtafiti na consultant wa kujitegemea (ndiyo nikapata mkataba wa kuwashauri WAMA kama mtaalamu wa mikakati, siyo kama muajiriwa).

Kabla ya hapo nilikuwa naendesha biashara ya taxi (nilianza na moja na zilifika 4 - kila moja ikiniletea wikiendi sh 60,000), salon ya kike moja pale chuoni Muhimbili (ikileta sh 200,000 kila wikiendi), na nne ndogo ndogo za kiume kule mitaani (kila moja ikiniletea wikiendi sh 20,000). Niliuza biashara zote hizi na kuunganisha nguvu na mtaji wa kuanzisha biashara ya IT na ya pamba (kama wakala). Mwaka wa pili tulikopa benki ya CRDB na kununua kiwanda chetu wenyewe. Leo hii tuna viwanda viwili (cha kuchambua Pamba - ginnery, na cha kukamua mafuta (ya pamba na alizeti), tuna matrekta (saba) na malori (zaidi ya 30).

Biashara ya taxi niliianzisha kutokana na pesa zangu nilizoweka akiba kutokana na kazi za kibarua nilizokuwa nafanya baada ya kumaliza high school - nilikuwa nafundisha tuition, shule moja ya sekondari ya Badri iliyopo Nzega mjini, na kibarua mgodini. Aliyeniuzia gari nilimpa pesa nusu akanipa gari nikafanya kazi ya taxi huku nikimlipa kidogo kidogo mpaka deni likaisha. Nakumbuka Wakili Alex Mgongolwa ndiye alisaini mkataba huu wa mauziano.

Kueleza kwa ufupi hivi ni rahisi. Ndani yake kuna details kama za kukosa hela ya pango. Kama ya kwenda kusoma nje ya nchi na kusambaza magazeti kwenye baridi ya asubuhi. Kama kukosa hela ya mafuta ya gari na kutembea kwa mguu kutoka msasani (nilipokuwa naishi) kwenda mjini (upanga) kwenye ofisi yetu. Kama kutapeliwa. Kuzunguka benki zaidi ya 10 kutafuta mkopo na kunyimwa. Kuna mengi.

Wengine watasema hata Ubunge 2010 nilibebwa, sawa tu. Lakini sisi wakimbu huwa tuna msemo wetu mmoja, kwamba 'lift humkuta mtu aliye njiani'.

Imeandikwa na Dkt. Kigwangalla, Mbunge, Nzega Vijijini.
[HASHTAG]#NjeYaBox[/HASHTAG] [HASHTAG]#TeamBelieve[/HASHTAG] [HASHTAG]#BePositive[/HASHTAG] [HASHTAG]#FikiriTofauti[/HASHTAG] [HASHTAG]#SiasaNiVitendo[/HASHTAG] [HASHTAG]#HapaKaziTu[/HASHTAG] [HASHTAG]#SasaKaziTu[/HASHTAG] [HASHTAG]#HamisiKigwangalla[/HASHTAG] [HASHTAG]#TeamHK[/HASHTAG]
 
Ahache siasa mwambie yeye ni dactari......

Tena waziri wa wizara nyeti ya magonjwa ya binadamu..........

Anashindwa kujua kuwa yeye elimu aliyonayo alitakiwa kuwa nani Sasa na yeye ni nani?...........

Anaujua mfumo wa Tanzania wa elimu jinsi ulivyo ?......

Anayetakiwa kuandika haya ya kuamasisha sio waziri mbunge au Lectures wa udsm......

Ni Mtu kama Backhresa,Mo,Mengi,Wakina Kusaga ambao sijui record yao ya kuajiriwa ilikuwa lini na wapi..........

Mwambie ahache porojo kujiajiri sio kazi rahisi kwa mifumo mibovu iliyopo Tanzania............
 
View attachment 465945

Nadharia nzuri. Ukichukua mazingira yako kuwa mazingira waliyomo vijana wote hapo ndipo linakuja tatizo la kuwaita wale, ambao bado wanahangaika na hawajaweza kufaulu kuondokana na umaskini walio nao, "wavivu/hawataki kufanya kazi". Lakini kuna maxim moja naiheshimu sana. Inasema: "If the theory does not fit the practice ignore the theory".
 
Long story, Dr hongera KWA mchanganuo. Ajira KWA ujumla ni tatizo karibu nchi zote duniani hasa bars LA Africa. Pia kuna makundi tofauti ya vijana, graduate na waso graduate, ni kazima kuwa na mkakati KAZI ndani ya makundi haya, nini mtazamo wako ukichukulia ni Kundi kubwa ambalo sector moja haiwezi mudu. [HASHTAG]#drkigwangala[/HASHTAG]
 
Mngekuwa mnataka vijana wajiajiri si mngeanza kugawa milioni 50 kwa kila kijiji ila badala yake serikali hii unayoitumikia imeelekeza mabilioni kwenye miradi ya huko Chato na kununua mandege mengi kwa mpigo utazani serikali haina majikumu mengine.

Kingine kinachokera ni hii serikali kushindwa kupeleka ada vyuoni matokeo yake graduates wa mwaka jana baadhi yao vyeti vyao vimezuiwa na vyuo mpaka pale Bodi itakapopekeka hela.

Lipeni ada na si kununua mandege na kuelekeza hela huko Chato vijana wakajitafutie ajira hata private na kuachana na hii serikali iliyoshindwa kuajiri hata walimu na madaktari wanaohitajika sana kwa kisingizio cha aibu kabisa cha kuhakiki watumishi laki tano kwa miezi 8!

Pathetic!
 
Mngekuwa mnataka vijana wajiajiri si mngeanza kugawa milioni 50 kwa kila kijiji ila badala yake serikali hii unayoitumikia imeelekeza mabilioni kwenye miradi ya huko Chato na kununua mandege mengi kwa mpigo utazani serikali haina majikumu mengine
Enheeee na wangeanza kufundisha masomo ya ujasiriamali mashuleni na vyuoni
 
Kipindi nimemaliza chuo nilikaa almost miaka miwili bila ajira, nakumbuka nilikuwa na bro wangu mmoja akisoma uturuki alikuwa akinipigia simu na kunisema mimi ni mzembe nashindwa kutafuta na kutumia FURSA kibao zilizojaa hapa Tanzania kisha anafuatisha na lecture ya lisaa zima kuhusu kujitambua na kujiajiri...Baadaye nikabahatika kupata kiajira ambacho ninacho mpaka leo...Yeye baada ya kumaliza kutokana na sababu flani za msingi hakuja na pesa ya maana...Naye ana mwaka sasa yupo mtaani....huwa ananipigia simu kunilalamikia maisha magumu...nami namwambia WEWE KIJANA UNASHINDWA VIPI KUTUMIA FURSA...SIO LAZIMA UAJIRIWE, TAFUTA FURSA, ZIPO NYINGI TU....

My take

Huu ni kama mchezo tu, aliyeshiba siku zote hamjui mwenye njaa...Maisha hayana formula....Wengi wanaopiga kelele za kutumia fursa either wameajiriwa au walibahatika kutoka katika familia tofauti na zetu ambazo bumu lote unasomesha wadogo zako na kulisha wazazi wako....
 
Back
Top Bottom