Dr Kigwangalla aruhusiwa kutoka hospitalini baada ya afya yake kutengamaa!

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Leo Septemba 11, 2018. Jopo la Madaktari Bingwa wa MOI linalomhudumia Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamisi Kigwangalla, limemruhusu kutoka wodini baada kujiridhisha kwamba afya yake imetengamaa na anaweza kurudi nyumbani ili kuja hospitali kama mgonjwa wa nje.

Jopo hilo la madaktari bingwa 5 wa kada za Mifupa, Usingizi na Magonjwa ya Ndani, limefikia uamuzi huo baada ya baada ya kumhudumia Dr Kigwangalla toka Agosti 12, 2018 alipohamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI kwa ajili ya matibabu ya kibingwa ya mkono wake wa kushoto baada ya kupata matibabu mengine katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amemtakia kila la heri Dr Kigwangalla katika kutekeleza majukumu yake ya Kitaifa kwani ni muda muafaka wa kwenda kuwatumikia wananchi.

"Kwa niaba ya Taasisi ya Mifupa MOI tunakutakia kila la heri katika kutekeza majukumu yako ya ujenzi wa Taifa, ilikuwa heshima kubwa kuwa nawe hapa kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja, tunaamini umeridhishwa na huduma zetu na kama kuna mahali umeona mapungufu ni vema ukatujulisha ili turekebishe", alisema Dkt. Boniface

Kwa upande wake Dr Kigwangalla ameushukuru uongozi wa Taasisi ya MOI, madaktari na wauguzi ambao wamekuwa wakimhudumia kwa kipindi chote alipokuwa wodini.
IMG_20180911_183250_105.jpg
IMG_20180911_183434_212.jpg
IMG_20180911_183234_803.jpg
 
Hivi hii nayo ni habari ya kuita waandishi wa wahabari?? si atoke kimya kimya akamsgukuru Mungu wake aonae sirini, sifa za kijinga tu
 
Hivi hii nayo ni habari ya kuita waandishi wa wahabari?? si atoke kimya kimya akamsgukuru Mungu wake aonae sirini, sifa za kijinga tu
Mkuu lazima ujue huyo ni public figure
Ndio maana kuna nyuzi humu za hilo tukio la ajali yake kibao
Hivyo jamii ilipaswa kutaarifiwa kuwa ametoka. Au ulitaka atoke kimya afu mje muulize tena humu yuko wapi
 
Back
Top Bottom