johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,855
- 141,793
Dr Kigwangalla amesema kuwa ajali ya gari aliyopata ni jambo kubwa lakini wamejifunza mengi. Mosi amejifunza kuwa kifo kipo lakini kubwa zaidi ni uwepo wa Mungu wa mbinguni. Kigwa anasema alimuona dereva wake akimkwepa twiga na ghafla gari ikaanza kupaa kama ndege inatake off, ndipo alipomkumbuka Mungu na kuswali dua yake ya mwisho. Zaidi ya hapo hakumbuki kilichoendelea zaidi ya kujikuta yuko hospitali. Tukio lile lilimtisha kiasi cha kumfanya aanze kupanga urithi na jinsi ya kulipa madeni atakayoyaacha hapa duniani, amedisitiza Kigwangala. Amemalizia kwa kusema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri na baada ya mapumziko atarudi ofisini kukamilisha kazi aliyoiacha baada ya kuwa ziarani huko misituni kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu.......Get well soon Dr Kigwangalla!