Dr. Kigwangala ataja wanaume kuwa vinara wa michepuko

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252

Kigwangallah.jpg
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kusema kuwa wanaume wengi wamekuwa vinara wa michepuko jambo ambalo linapelekea kupata virus vya UKIMWI na kwenda kuwaambukiza wanawake.

Kigwangalla amesema hayo leo bungeni wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti maalum CHADEMA, Susan Lyimo ambaye alitaka kujua kwanini idadi kubwa ya wanawake ndiyo wamekuwa waathirika wa virus vya UKIMWI, akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya alikiri kuwa ni kweli kuna utofauti japo si mkubwa sana na kudai kuwa wanawake wengi wanapata maambukizi haya kutokana na utofauti wa kibaolojia wa maumbile lakini pia kutokana na mienendo ya wanawake na wanaume.
"Maambukizi kati ya wanawake na wanaume kuna uwiano, lakini hili la wanawake kuwa wengi kuonekana wanapata virus vya UKIMWI ni kutokana na utofauti ya kimaumbile ya kibaolojia kati ya wanawake na wanaume, tabia za wanaume na wanawake. Lakini wanaume wengi wamekuwa na tabia za kuchepuka sana hivyo wao wanaweza kuvitoa virus huko na kuleta kwa wamama nyumbani, maana wanaume ndiyo chanzo cha michepuko ukilinganisha na wanawake" alisema Kigwangalla
Mbali na hilo Kigwangalla aliwataka wanaume kuachana na tabia za michepuko, na kujiwekea utaratibu wa kupima afya zao na wenza wao ili wame na uhakika na afya zao na kutopeleka virus hivyo kwa wake zao majumbani kwao.
"Mimi nawashauri wanaume waepukane na michepuko watulie kwenye ndoa zao, tujiwekee utaratibu wa kupima hali zetu na wenza wetu, kwa wale ndugu zangu waislam tumepewa fursa ya kuoa hata wake nne, hivyo ni bora upime hali za wenza wako wote hao kisha uoe wote na kuepukana na michepuko tunayoiokota huko, ni bora upime ili uchukue mtu na kuweka ndani kabisa" alisisitiza KigangwallaKigangwalla

Chanzo: EATV
 
Angewajua hao anaowaamini, hata ukimwachia milioni bado anahadaika kwa fungu la nyanya gengeni. Jirani yangu alimfuma mkewe na muuza vyombo ambaye kwa maelezo
ya wanawake wenzie wanasema alivutiwa nae kwa jinsi anavyoweza kugonganisha vijiko
huku akiimba wakati wa kunadi biashara yake mtaani.
 
Inamaana mwanaume mmoja huwa anaambukiza mwanamke zaidi ya mmoja?

Kwa hiyo yeye DR.Kigwangala hajawahi kuchepuka katika ndoa yake ndio maana anatoa ushauri kwa wengine?
 
Akili za CCM bwana! Ikiwa mwanaume ndio anapata na kwenda kumuambukiza mwanamke, si ina maana kwamba na huyo mwanaume kishapata? Sasa hapo ndio kajibu nini?

Well then, huyo mwanaume anayechepuka na kupata ukimwi kisha anaenda kumuambukiza mkewe, anachepuka na nani kama sio mwanamke?
 
Anazingua,..akatafte kazi ya kufanya,..hayo sio maneno ya kuongea,ajui wanawake ndo vinala wakutunza HIV kutokana na maumbile,..kwa iyo tusichepuke,
 
Angewajua hao anaowaamini, hata ukimwachia milioni bado anahadaika kwa fungu la nyanya gengeni. Jirani yangu alimfuma mkewe na muuza vyombo ambaye kwa maelezo
ya wanawake wenzie wanasema alivutiwa nae kwa jinsi anavyoweza kugonganisha vijiko
huku akiimba wakati wa kunadi biashara yake mtaani.

Hahaaaa mkuu acha utani yani alifurahishwa na biti la vijiko tu??

Halaf mtu kama huyo utakuta anapewa kila kitu na mumewe ila matokeo ndo hayo.

"Hawa nduguze Hawa(Eva) ni wakuishi nao kwa akili na uvumilivu tu"
 
Michepuko sio dili, baki njia kuu

Hii slogan huwa siielewi nikiwa na sideChick hahaha
 
Angewajua hao anaowaamini, hata ukimwachia milioni bado anahadaika kwa fungu la nyanya gengeni. Jirani yangu alimfuma mkewe na muuza vyombo ambaye kwa maelezo
ya wanawake wenzie wanasema alivutiwa nae kwa jinsi anavyoweza kugonganisha vijiko
huku akiimba wakati wa kunadi biashara yake mtaani.
Jamaa yaani awa watu wanapenda sana slope yaani vitu vya bure we katibu tyu utakula mtaa mzima .. Boda anamsamee Mara 4au 5 nauli anamla pasipo kujua kuwa iyo ni sawa na buku 5
 
Angewajua hao anaowaamini, hata ukimwachia milioni bado anahadaika kwa fungu la nyanya gengeni. Jirani yangu alimfuma mkewe na muuza vyombo ambaye kwa maelezo
ya wanawake wenzie wanasema alivutiwa nae kwa jinsi anavyoweza kugonganisha vijiko
huku akiimba wakati wa kunadi biashara yake mtaani.
Kuna jamaa yangu alipata kusema "wanawake husimama kwa mguu mmoja, kuanguka kwao ni kugusa tu."
 
Huyo nae amekuaje sikihizi hata simuelewi

Je amepima wamaume wangapi idadi sawa na wanawake akalogindua hilo?
Hospitali hazina dawa hata mkiwa na bima unapewa panadol hawajibiki yeye yupo kimya

Mzee wa kutumbua rekebisha huyo
 
Back
Top Bottom