Dr. Kapiteni wa TMJ Hospital ni hatari kwa wagonjwa wa kike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Kapiteni wa TMJ Hospital ni hatari kwa wagonjwa wa kike

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by vita, May 6, 2011.

 1. v

  vita Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Wanajamii inabidi mumfahamu daktari wa TMJ Hospital kwa jina la Kapiteni. Huyu ni mkongomani asiye na adabu hata kidogo.

  Kila msichana na mwanamke anaeingia katika chumba chake cha udaktari lazima amtongoze kisha anampeleka nyumbani kwake ambako si mbali na hospitali kufanya ngono.

  Anatumia advantage yake ya udaktari kuwadanganya kuwa atawasaidia matibabu na wasichana ambao wengine ni sawa na wajuu zake anawadanganya eti ata waoa!

  Huyu anatakiwa apewe funzo kwa sababu mchezo huo anaoufanya kulala ovyo wasichana, wachumba na wake za watu hawezi kuuacha.

  Hivi toeni mapendekezo daktari huyu tumfanye nini?
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Sioni uhusiano kati ya taaluma ya udaktari na technic ya mtu kutongoza...nadhani hao anaowatongoza ni watu wazima na wanaweza/wana haki ya kukubali au kukataa. Kujaribu kusema hawawezi kukataa kwa sababu tu ni daktari si sahihi. Kam mtu ana nia ya kukataa mbona kuna hospitali nyingi tu ambazo anaweza kwenda si lazima TMJ, na pia kuna madkatari weengi tu sio lazima Kapiteni.

  Mlaumu Kapiteni kama Kapiteni kwa tabia yake, na si taaluma yake...tena unapost JF Doctor habari za udaku ukijaribu kuipa image ya kitaaluma.
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Dah nampata huyo dr. anapenda sana hako kamchezo
   
 4. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  simlaumu sana maana hao anaowadanganya wanapenda wenyewe kudanganyika! na wako wanaume wengi tu wa hivyo na wanawake tunatakiwa kuwa makini na kutumia akili zetu!
   
 5. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Ingekua watoto wadogo ningeshauri...
   
 6. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wamependa wenyewe kaka. Kwani anawabaka au wanavua chu..i wenyewe
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Riwa, nakubaliana na wewe juu ya authenticity ya hii habari (imekaa kidaku!).

  Lakini kama unajaribu kuashiria kuwa daktari hana priviledged position juu ya mgonjwa-mtongozwaji hapo natofautiana na wewe. Kumtongoza mtu kwa kawaida unahitaji kujua baadhi ya information zake (jina, anaishi wapi, contacts etc) na pia kupata opportunity ya kuwa mahali penye privacy na unayekusudia kumtongoza...vyote hivi kwa maoni yangu daktari anaweza kuvipata kutokana na taaluma/position yake. Daktari pia kwa taaluma yake anaweza kuwa na access na tupu za mgonjwa (kwa baadhi ya mogonjwa anaweza kumwambia mgonjwa wake avue nguo kwa mfano!). So kama tunalinganisha daktari na mtongozaji mwingine asiye daktari wa mgonjwa, ni wazi kuwa daktari ana kitu cha ziada katika hiyo process ya kutongoza na yatokanayo.

  Kwa kweli mimi binafsi naona ni unethical kwa daktari kumtongoza mgonjwa. pamoja na kwamba ni kweli pia sio lazima mwanamke akitongozwa akubali...anao uhuru wa kukataa! Ndio sa zingine tunasikiwa daktari kabaka mgonjwa wake!
   
 8. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  SMU nikuthibitishie tu kuwa ni 'unethical' kwa daktari kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mgonjwa wake, na mbaya zaidi...kutumia taaluma au 'authority' (sijui kama ni neno sahihi) uliyonayo kum'exploit' mgonjwa sexually. Hiyo ni offense ambayo ukitiwa hatiani unafutiwa usajili na kuhukumiwa kwa jinai kufungwa jela. Kwa hiyo kama mtu hashitaki ina maana ameridhia...na pale unaporidhia hiy inamtoa muhusika kama daktari bali yanakuwa maridhiano ya kawaida kati ya marafiki wawili.

  Hivi unadhani hakuna madaktari wanaotongoza wanawake wakapigwa vibuti? Wapo weeengi sana, sasa hii advantage ya taaluma yao inatokea wapi?! Huwezi check record za mgonjwa ukachukua address au namba ya simu kisha kuzitumia binafsi kumtongoza...ukishtakiwa unafutwa kazi na hata kufutwa usajili kwa muda kwa kutmia vibaya taarifa za mgonjwa.

  Bado nadhani hii issue ni maridhiano ya watu wawili na wala haina uhusiano na taaluma.
   
 9. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Anawapelekaje kwake bila maridhiano
  ilivyosema RIWA ni sahihi kabisa
   
 10. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  kama wanakubali we kinachokuuma ni nini hasa.
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Riwa,
  Hukuwezi kuwapo kwa consent ya haki kama upande mmoja upo kwenye advantageous position dhidi ya mwingine. Kwa mujibu wa mleta habari tuhuma dhidi ya Kapiteni ni hizi hapa:

  Labda kwa ajili ya mjadala, lets assume ndio tuhuma rasmi zimepekwa bodi ya madaktari au chombo kingine cha kusimamia maadili ama cha sheria na zaidi lets also assume ni tuhuma zinazoweza kuthibitika. Je bado huoni uhusiano wa tuhuma hizo na taaluma ya Kapiteni? Ningeweza kuelewa kama tuhuma zingekuwa anawatongozea baa au sehemu nyingine kwa mfano bila hata wao kujua kuwa ni daktari wao.

  Mimi naona kitaaluma siyo sahihi kwa dk kumtongoza mtu aliyekuja kwake kwa ajili ya matibabu (kama kapiteni anvyotuhumiwa kufanya) hata kama mgomjwa ana uhuru wa kukataa. Wewe unaonaje?
   
 12. mkokoteni

  mkokoteni Member

  #12
  May 6, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Vita,
  Umetoa shutuma nzito lakini hukuweka wazi kama na wewe ni muathirika wa hizi move za doctor. au labda umepewa mandate na waathirika kuleta shutuma hizi. umesema wengine ni wake na wachumba lakini huja taja hata jina moja. swali je na wewe umezipata habari hizi ili nasi tujiridhishe tunajadili jambo lililopo, kinyume chake ni kutaka kumchufulia jina doctor huyu. hii sio sahihi hata kidogo. haya ni majungu.
   
 13. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Mwenye email ya TMJ management au Fax awafahamishe.......... hata kama ni makubaliano ya huyo dr. anayetumia nafasi yake kutongoza na hao wagonjwa, bado kitaaluma na uongozi wa hospitali inawavunjia Heshima big time.

  Hivyo nashauri mwenye mawasiliano na TMJ awape taarifa, afanyiwe uchunguzi na hatua zichukuliwe dhidi yake.
   
 14. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  umeshampatia publicity tayari huyo docta! wanawake wanaopenda majomboz wote watakuwa wanaenda kwake! gud work!
   
 15. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #15
  May 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mlifikiri atakutana nao porini au bar ambako labda kwake yeye hapati muda wa kwenda huko?!Mi nadhani ni wakati wa dada zetu,wake zetu wajifunze kukataa make sidhani kama atawalazimisha kufanya nao ngono kinguvu? Lakini kwa kuwa wanataka wao kwa kujirahisisha basi na jamaa anafanya kweli.
  ......tujiulize ni wangapi wamepata wachumba /wake kupitia huko ofisi wanakofanyia kazi?Kama jibu ni,wapo wengi..... basi mwacheni doctor labda atafuta wa kumweka ndani.
   
 16. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe unayetetea kwamba maadam mwanamke amekubali mwenyewe tatitizo ni la mwanamke si kweli na inawezekana hamjaoa mkaona uchungu. Kumbuka most ya hawa wanawake hawakukutana baa na huyu dokta bali walikwenda kupata huduma akaanzisha upuuzi wake. Hivi mke wako akienda pale akatongozwa tu hata kama hakutoa halafu akafika home akakueleza utajisikiaje? nasema hivi kwa sababu hapa wengi wametoa majibu very simple bila kujua katika ndoa mtu ile kumtongoza tu mke wako na akaja kukuambia unaweza mmaliza. Mimi nashauri huyu dokta awekewe mtego akamatwe achukuliwe hatua kwani very unethical kama alivyosema Riwa. Mbaya zaidi anatumia ofisi ya hospitali kama mtego wa kuwanasa wanawake na mbaya zaidi wagonjwa. Angekuwa anawatongoza anapokutana nao baa ni kitu kingine lakini siyo ofisini kwake.
   
 17. H

  Haika JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  To be fair, Ni mategemeo yangu, kuwa mwanaume anatakiwa apate msichana ambaye anaweza kumtongoza, ndio amtongoze. Kama ni kazini au la. Lazima awe kwenye position ya advantage.
  Swala la kuwepo au kutokuwepo kwa ethics katika matendo yake nadhani liingizwe pale kunapokuwa na kulazimisha, kudanganya etc.
  Lakini kama ni hiari, nadhani tuwaachie wenyewe.
  Labda walalamike hao wanawake.
  Ni wanawake wachache ambao watafikia umri wa uzee bila kukutana na madaktari kadhaa ambao wataintorduce topic ya mapenzi au sex wakati wa matibabu.
  Kuna baadhi ya wanawake ambao kimuonekano tu ni vigumu mwanaume kukaa nae faragha bila kutamani au kupata wazo la kuomba huduma hio pia.
  Ni kweli huyu kaka anapenda hako kamchezo, lakini huwa anafanya na wenzake wenye kukapenda, samahani kama mkeo ni mmojawapo.
  Generaly japo ni mkorofi, wanasema ni daktari mzuri. Akiondoka TMJ haitakuwa kama ilivyo sasa.
   
 18. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2011
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kha! mtu kama babu yako anakudanganya atakuoa?! nawe unadanganyika?! hiyo akili au matope. watakuwa wanatiwa kwa kukubali bana acheni hizo.
   
 19. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Ukiona katiwa si mgonjwa huyo
   
 20. Amina Thomas

  Amina Thomas JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2011
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 272
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi namfahamu huyu jamaa kwa miaka mingi sana. Ni doc mzuri sana ila hako ka tatizo anako sana tu. Lakini kwani lazima ukubali? Wanaume wengi wanaangaliaga mazingira kama unatongozeka au la! Kama mwanamke unaajiheshimu na una mumeo au mchumba kwa nini ukubali kudanganywa?
   
Loading...