Dr. Kafumu: Tuliahidi kumpa Dangote ardhi, gesi, makaa ya mawe, limestone kwa bei nafuu

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
DK. KAFUMU on DANGOTE (A must read).

"Hii ni shida yetu watanzania wote, wataalamu, viongozi wa serikali na pia wanasiasa. Kwanza tuko SLOW, sijui tunaogopa kutoa maamuzi? Sijui ni taaluma duni? Sijui ni nini? Mwekezaji DANGOTE, tuliahidi kumpa malighafi ya LIMESTONE kwa ajili ya kuzalisha SARUJI kwa unafuu mkubwa; tuliahidi kumpa ardhi kwa bei nafuu au bure; tuliahidi kumpa gesi nyingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa makaa ya mawe kwa wingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa nafuu ya kodi na mengine mengi; mazingira yaliwavutia (Dangote na wenzake) sana.

Dangote wakavutika wakaja. Mimi (Dk. Kafumu) nikiwa Kamishna wa Madini wakati huo nilitimiza wajibu wangu wa kuwapa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa LIMESTONE kadri ilivyohitajika. Nawashukuru sana STAMICO walinisikiliza na kiwanda kijajengwa. Awamu ya tano (ya JPM) imekuja na mambo mapya, ahadi zingine (kwa wawekezaji) zinasuasua, sijui ni nini!

Prof Mjebda (anamtaja Prof. mwingine kwenye Whatsup Group) anaweza kutuelimisha hapa. Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa ikiwa ni pamoja na nchi kupata kodi za kutosha; ajira zitapatikana; sekta ya majenzi (ujenzi) itaimarika; uchumi utaimarika.

Ni muhimu tuwahamasishe (wawekezaji) tuangalie matokeo ya muda mrefu na siyo haya ya haraka. Kiwanda kikifungwa shida ni yetu, hebu tuwe na mioyo ya kibiashara siyo siasa za uzalendo uchwara. Samahani sana "

Dkt. Dalali Kafumu,
Kamishna Mstaafu wa Madini (Tanzania),
Mbunge wa Igunga (wa sasa),
Kada wa CCM.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Nimehariri lugha kwenye maoni hayo ya kitaalamu ya Dk. Kafumu. Tujadili seriously.
JSM.
================
 
DK. KAFUMU on DANGOTE (A must read).

"Hii ni shida yetu watanzania wote, wataalamu, viongozi wa serikali na pia wanasiasa. Kwanza tuko SLOW, sijui tunaogopa kutoa maamuzi? Sijui ni taaluma duni? Sijui ni nini? Mwekezaji DANGOTE, tuliahidi kumpa malighafi ya LIMESTONE kwa ajili ya kuzalisha SARUJI kwa unafuu mkubwa; tuliahidi kumpa ardhi kwa bei nafuu au bure; tuliahidi kumpa gesi nyingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa makaa ya mawe kwa wingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa nafuu ya kodi na mengine mengi; mazingira yaliwavutia (Dangote na wenzake) sana. Dangote wakavutika wakaja. Mimi (Dk. Kafumu) nikiwa Kamishna wa Madini wakati huo nilitimiza wajibu wangu wa kuwapa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa LIMESTONE kadri ilivyohitajika. Nawashukuru sana STAMICO walinisikiliza na kiwanda kijajengwa. Awamu ya tano (ya JPM) imekuja na mambo mapya, ahadi zingine (kwa wawekezaji) zinasuasua, sijui ni nini! Prof Mjebda (anamtaja Prof. mwingine kwenye Whatsup Group) anaweza kutuelimisha hapa. Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa ikiwa ni pamoja na nchi kupata kodi za kutosha; ajira zitapatikana; sekta ya majenzi (ujenzi) itaimarika; uchumi utaimarika. Ni muhimu tuwahamasishe (wawekezaji) tuangalie matokeo ya muda mrefu na siyo haya ya haraka. Kiwanda kikifungwa shida ni yetu, hebu tuwe na mioyo ya kibiashara siyo siasa za uzalendo uchwara. Samahani sana "

Wengine tuko serious ktk kujadili, lakini Kafumu mwenyewe tunaomba awe mtaalamu. Lugha za kisiasa ni mbaya na hatutaki.

Huwezi nishawishi kwa kutumia lugha kama hiyo; Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa. Makubwa maana yake ni nini? Toa figures. Hiki siyo kiwanda cha kwanza kuzalisha cement hapa TZ. Unaporuhusu unafuu wa aina hiyo je, umeangalia matatizo yatakayojitokeza kwa viwanda vingine ambavyo hujavipa unafuu huo? Halafu kamishna wa zamani, mwenye Ph.D anasema nchi itapata kodi za kutosha, kodi gani hizo wakati mulitoa ahadi lukuki. Tunaomba ataje ni kodi gani na kwa makadirio zitakuwa bilioni ngapi. Halafu eti sekta ya ujenzi itaimarika na uchumi utaimarika. This is no useful!

Je, misamaha hiyo iko connected na tatizo la hao makamishna na wanasiasa kuwa na hisa ktk kiwanda hicho? Je, nini hatma ya viwanda vya Twiga, Tanga cement, nk. ktk soko la ushindani?

Kafumu acheni bhla-bhla! Kama msomi tumia figures badala ya maeneo ya bungeni: Nyingi, ya kutosha, kwa wingi, inatia moyo, ya kutosha, nk. ambayo ni maneno useless!
 
Dalali Kafumu ww na chama chako mnatuchanganya. Mbona kuna taarifa imetolewa na gazeti la Mwananchi ikikanusha tishio la kiwanda hicho kufungwa? Gazeti hilo limemnukuu bosi fulani wa kiwanda hicho akisema kiwanda kiko kwenye matengenezo ya hitilafu ya kawaida iliyojitokeza.

CCM plz walk the talk.
 
Haya mambo yanachanganya sana,Mkuu JPM hebu sikiliza ushauri wa wataalamu tofauti,ni kweli unataka "kutunyoosha" na ni kweli umeikita nchi ikiwa ni ya wapiga deal wa kufa mtu,lkn twenda taratibu baba,baba punguza mwendo baba....Weka mguu wa kati kuonana na breki baba.Wasikilize wataalamu baba,Wanasema "A Jack of All Trade is a Master of None".Kuwa Rais haimaniishi unaelewa kila kitu,tafuta watu wako waaminifu watakaokushauri bila woga na kukuingiza chaka.

Nimesoma maelezo ya Mkurugenzi wa Dangote,yeye anasema waliahidiwa gas,na wakahaidiwa punguzo la kodi,lkn mpaka sasa gas hawajapata na hakuna dalili,matokeo yake wanazalisha kwa ghalama kubwa kwa kutumia diesel,kodi imepanda,malighafi ipo juu,hivyo wameamua kusitisha ili kuona wanajioangaje.Na baada ya kusema tu wanafunga,Mpaka sasa Cement imepanda kwa shilingi 400 toka bei ya zamani.

Anakuja Mwijage sijui Kaijage Waziri wa Viwanda,anasema huyo mkurugenzi wa Dangote kwanza sio msemaji wa Dangote,na wala hajui mambo ya ndani ya Dangote,tena huyo ni mgeni.Yeye waziri kafanya kazi TPDC na anajua kuwa Dangote wamefunga sbb mitambo ni mibovu na si ghalama za uzalishaji.Sasa unajiuliza,hivi Waziri na Boss wa kiwanda cha Dangote nani mkweli??

Mambo haya ya ajabu sana.Nimemsikiliza na Msajili wa Hazina bwana Mafulu,nimegundua wataalamu wa Serikali wanafiki na waoga sana,hata suala la fixed Account aliyethubutu ni Gavana wa BOT tu,hata huyu Mafulu alikaa kimya
 
Dalali Kafumu ww na chama chako mnatuchanganya. Mbona kuna taarifa imetolewa na gazeti la Mwananchi ikikanusha tishio la kiwanda hicho kufungwa? Gazeti hilo limemnukuu bosi fulani wa kiwanda hicho akisema kiwanda kiko kwenye matengenezo ya hitilafu ya kawaida iliyojitokeza.

CCM plz walk the talk.

Hiyo ni kauli ya kuisitiri serikali. Leo asubui Waziri Mwijage aliojiwa na Clouds Fm akasema ametuma watu wakaongee ma wakurugenzi wa kiwanda cha Dangote. Wajue ni jinsi gani watamaliza matatizo yaliojitokeza.
Tatizo liko kwenye kodi,makaa ya mawe na limestone.
 
IMG-20161130-WA0054.jpg
Mpiga dili huyo akafie mbele, sisi tunataka Kodi zetu kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu!
Yaani vitu anavyofanya Raisi hairuhusiwi Kupinga au kukosoa?
 
Bora lipi? Kupata 50 kwa miaka mitano au kupata 200 kwa siku 4?

Resolute wamelipa kodi kiasi gani kwa miaka yote waliokuwepo hapa kwetu? Nenda Nzega ukaone wameacha nini, na wananchi wamefaidika vipi na dhahabu yao iliyochukuliwa yote, au Barrick aka Acasia wamelipa nini? Tanzanite yetu Tanzaniteone wamelipa nini kwa wananchi wetu nenda Mererani ukawaulize Wananchi wamepata nini miaka yote ya kuwepo kwa Tanzanite?
 
DK. KAFUMU on DANGOTE (A must read).

"Hii ni shida yetu watanzania wote, wataalamu, viongozi wa serikali na pia wanasiasa. Kwanza tuko SLOW, sijui tunaogopa kutoa maamuzi? Sijui ni taaluma duni? Sijui ni nini? Mwekezaji DANGOTE, tuliahidi kumpa malighafi ya LIMESTONE kwa ajili ya kuzalisha SARUJI kwa unafuu mkubwa; tuliahidi kumpa ardhi kwa bei nafuu au bure; tuliahidi kumpa gesi nyingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa makaa ya mawe kwa wingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa nafuu ya kodi na mengine mengi; mazingira yaliwavutia (Dangote na wenzake) sana. Dangote wakavutika wakaja. Mimi (Dk. Kafumu) nikiwa Kamishna wa Madini wakati huo nilitimiza wajibu wangu wa kuwapa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa LIMESTONE kadri ilivyohitajika. Nawashukuru sana STAMICO walinisikiliza na kiwanda kijajengwa. Awamu ya tano (ya JPM) imekuja na mambo mapya, ahadi zingine (kwa wawekezaji) zinasuasua, sijui ni nini! Prof Mjebda (anamtaja Prof. mwingine kwenye Whatsup Group) anaweza kutuelimisha hapa. Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa ikiwa ni pamoja na nchi kupata kodi za kutosha; ajira zitapatikana; sekta ya majenzi (ujenzi) itaimarika; uchumi utaimarika. Ni muhimu tuwahamasishe (wawekezaji) tuangalie matokeo ya muda mrefu na siyo haya ya haraka. Kiwanda kikifungwa shida ni yetu, hebu tuwe na mioyo ya kibiashara siyo siasa za uzalendo uchwara. Samahani sana "

Dkt. Dalali Kafumu,
Kamishna Mstaafu wa Madini (Tanzania),
Mbunge wa Igunga (wa sasa),
Kada wa CCM.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Nimehariri lugha kwenye maoni hayo ya kitaalamu ya Dk. Kafumu. Tujadili seriously.
JSM.
Kwakweli ni uzalendo uchwara ila poa tu wanasema Tanzania ya viwanda wakiwa ikulu has sijui viwanda vitajengwa ikulu
 
Bora ungenyamaza kimya kuliko kuandika pumba kama hizi uwe unajiongeza.

Dkt. Dalali Kafumu,
Kamishna Mstaafu wa Madini (Tanzania),
Mbunge wa Igunga (wa sasa),
Kada wa CCM.

Wazungurusha mikono na washika ukuta mmeona suala la Dangote ndiyo point yenu kisiasa kuikosoa serikali yetu pendwa, fukuzeni mafisadi mnaowalea kwanza.
 
Wengine tuko serious ktk kujadili, lakini Kafumu mwenyewe tunaomba awe mtaalamu. Lugha za kisiasa ni mbaya na hatutaki.

Huwezi nishawishi kwa kutumia lugha kama hiyo; Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa. Makubwa maana yake ni nini? Toa figures. Hiki siyo kiwanda cha kwanza kuzalisha cement hapa TZ. Unaporuhusu unafuu wa aina hiyo je, umeangalia matatizo yatakayojitokeza kwa viwanda vingine ambavyo hujavipa unafuu huo? Halafu kamishna wa zamani, mwenye Ph.D anasema nchi itapata kodi za kutosha, kodi gani hizo wakati mulitoa ahadi lukuki. Tunaomba ataje ni kodi gani na kwa makadirio zitakuwa bilioni ngapi. Halafu eti sekta ya ujenzi itaimarika na uchumi utaimarika. This is no useful!

Je, misamaha hiyo iko connected na tatizo la hao makamishna na wanasiasa kuwa na hisa ktk kiwanda hicho? Je, nini hatma ya viwanda vya Twiga, Tanga cement, nk. ktk soko la ushindani?

Kafumu acheni bhla-bhla! Kama msomi tumia figures badala ya maeneo ya bungeni: Nyingi, ya kutosha, kwa wingi, inatia moyo, ya kutosha, nk. ambayo ni maneno useless!
Unaweza kweli ukawa serious kujadili, lakini bahati mbaya kipande hiki cha observation ya Dk Kafumu (nilivyoelewa mimi) imechotwa kutoka kwenye mjadala kwenye group lake la whatsap, hivyo hakuna mtiririko wa yote aliyonena huko, lakini angalau kipande hiki kinajaribu kuonyesha kuna tatizo mahali fulani, na kwa uelewa wangu ninaona kama Dk Kafumu ana expose mgongano uliopo katika ku-treat investors. Kipande cha andishi la Dk Kafumu linatoa angalizo kwamba sisi ni double standard kwa wawekezaji!
 
Back
Top Bottom