Dr. Kafumu: Tuliahidi kumpa Dangote ardhi, gesi, makaa ya mawe, limestone kwa bei nafuu

Hizi habari za kufungwa kwa kiwanda cha Dangote eti, sababu ya kushindwa kukiendesha kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa sio za kweli hata kidogo. Taarifa sahihi na zenye ukweli ni kwamba, kiwanda cha Dangote kipo kwenye matengenezo makubwa ya mitambo yake baada ya kutokea hitilafu za kiufundi. Acheni upotoshaji usiokuwa na tija!
Mkuu tulitegemea usitoe sababu za juu juu.
Hicho kiwanda kitakuwa kwenye matengenezo kwa muda gani, miezi sita au?
In the meantime as per ITV bei ya saruji Mtwara inagonga 15,000/~ .
Tupate majibu.
 
Huyu anasumbuliwa na hasira za kunyimwa kazi ya Waziri wa Nishati na madini.

Mbaya zaidi anasema maneno kama vile hakuna viwanda vingine vya saruji.

Sasa ukimpa Dangote hiyo misamaha yote, hivyo viwanda vingine vya saruji nchini vitapambana naye vipi katika soko?

Kwa maana nyingine, Mtalaam wetu alitoa misamaha ili viwanda vingine vya saruji vishindwe kupambana kwenye soko na hatimaye vifungwe.

Hizi ndizo akili zinazofanana na wale wataalam wetu walikuwa wanatoa misamaha ya kodi kwa sukari wakati kuna viwanda vingine vya sukari nchini.
 
Resolute wamelipa kodi kiasi gani kwa miaka yote waliokuwepo hapa kwetu? Nenda Nzega ukaone wameacha nini, na wananchi wamefaidika vipi na dhahabu yao iliyochukuliwa yote, au Barrick aka Acasia wamelipa nini? Tanzanite yetu Tanzaniteone wamelipa nini kwa wananchi wetu nenda Mererani ukawaulize Wananchi wamepata nini miaka yote ya kuwepo kwa Tanzanite?

Mkuu Barbarosa;
Nakubali kuwa wewe ni mzalendo halisi na mwenye uchungu na Tz yako lakini kwa mtindo huu tunaokwenda, sioni nuru mbele. Nachelea kusema.

Naomba tujikite zaidi kwenye hili la Dangote. Dalili tumesha ziona tiyari. Bei ya sementi ishapanda hiyo. Hakuna namna ya kuipunguza tena.

Kweli, wapiga dili walipiga. Ila unafuu ukawa kwa mlaji. Sasa mmeamua kuziba mianya, but at who's cost?? Mlaji aliye masikini. Tunaenda wapi??

Mimi mlaji nimekukosea nini hata uniadhibu wakati hao wapiga dili are countable?? Si wanajulikana yakhee? Mbona mnawaogopa kihivyo?

Mmebaki kutamka tu kiujumla, sijui viongozi flani flani. Hawana majina??

Tiba hii ni kali sana ila haiponyi kidonda bali yaongeza maumivu tu.

Mmefungia mikopo benki, mmefungia mikopo ya kusomesha, mmefungia sasa hata simiti, haya Barbarosa, acheni tuishi ka mijishetwani tu kwenye tembe zetu. Kweli haya sasa ni maisha bora.

Mnazuia mkaa, bei ya umeme juu, gesi ya Mtwara haijafika Kinyeresi pamoja na vifaru kuranda mitaani. Haya mkuu. Tuone kodi yako ikihesabiwa iwekwe basi wazi.

Tumezoea kuona zikikusanyiwa chungu kikubwa na kupakuliwa kiulainiiii bila kukimbizana kwa mifuko ya sandalusi. Isije kuwa yale yale. Nawaza tuu
 
Hizi habari za kufungwa kwa kiwanda cha Dangote eti, sababu ya kushindwa kukiendesha kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa sio za kweli hata kidogo. Taarifa sahihi na zenye ukweli ni kwamba, kiwanda cha Dangote kipo kwenye matengenezo makubwa ya mitambo yake baada ya kutokea hitilafu za kiufundi. Acheni upotoshaji usiokuwa na tija!
Jifurahishe, ni haki yako.
 
DK. KAFUMU on DANGOTE (A must read).

"Hii ni shida yetu watanzania wote, wataalamu, viongozi wa serikali na pia wanasiasa. Kwanza tuko SLOW, sijui tunaogopa kutoa maamuzi? Sijui ni taaluma duni? Sijui ni nini? Mwekezaji DANGOTE, tuliahidi kumpa malighafi ya LIMESTONE kwa ajili ya kuzalisha SARUJI kwa unafuu mkubwa; tuliahidi kumpa ardhi kwa bei nafuu au bure; tuliahidi kumpa gesi nyingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa makaa ya mawe kwa wingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa nafuu ya kodi na mengine mengi; mazingira yaliwavutia (Dangote na wenzake) sana. Dangote wakavutika wakaja. Mimi (Dk. Kafumu) nikiwa Kamishna wa Madini wakati huo nilitimiza wajibu wangu wa kuwapa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa LIMESTONE kadri ilivyohitajika. Nawashukuru sana STAMICO walinisikiliza na kiwanda kijajengwa. Awamu ya tano (ya JPM) imekuja na mambo mapya, ahadi zingine (kwa wawekezaji) zinasuasua, sijui ni nini! Prof Mjebda (anamtaja Prof. mwingine kwenye Whatsup Group) anaweza kutuelimisha hapa. Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa ikiwa ni pamoja na nchi kupata kodi za kutosha; ajira zitapatikana; sekta ya majenzi (ujenzi) itaimarika; uchumi utaimarika. Ni muhimu tuwahamasishe (wawekezaji) tuangalie matokeo ya muda mrefu na siyo haya ya haraka. Kiwanda kikifungwa shida ni yetu, hebu tuwe na mioyo ya kibiashara siyo siasa za uzalendo uchwara. Samahani sana "

Dkt. Dalali Kafumu,
Kamishna Mstaafu wa Madini (Tanzania),
Mbunge wa Igunga (wa sasa),
Kada wa CCM.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Nimehariri lugha kwenye maoni hayo ya kitaalamu ya Dk. Kafumu. Tujadili seriously.
JSM.

We Dr Kafumu, mlipoingia mkataba mbona hamkutuambia haya note, kwa nini mliweka siri? We huo uzalendo umeutoa wapi? Kwa nini mliweka siri? Kwa nini mumpendelee Dangote? Kulikoni?? Toga, Kifaru etc? Hapa lazima maslahi yenu binafsi yameguswa ndio maana umejitokeza. Ni kwa nini viongozi wetu hamna uzalendo jamani??
 
Mkuu Barbarosa;
Nakubali kuwa wewe ni mzalendo halisi na mwenye uchungu na Tz yako lakini kwa mtindo huu tunaokwenda, sioni nuru mbele. Nachelea kusema.
Naomba tujikite zaidi kwenye hili la Dangote. Dalili tumesha ziona tiyari. Bei ya sementi ishapanda hiyo. Hakuna namna ya kuipunguza tena.
Kweli, wapiga dili walipiga. Ila unafuu ukawa kwa mlaji. Sasa mmeamua kuziba mianya, but at who's cost?? Mlaji aliye masikini. Tunaenda wapi?? Mimi mlaji nimekukosea nini hata uniadhibu wakati hao wapiga dili are countable?? Si wanajulikana yakhee? Mbona mnawaogopa kihivyo?? Mmebaki kutamka tu kiujumla, sijui viongozi flani flani. Hawana majina??
Tiba hii ni kali sana ila haiponyi kidonda bali yaongeza maumivu tu. Mmefungia mikopo benki, mmefungia mikopo ya kusomesha, mmefungia sasa hata simiti, haya Barbarosa, acheni tuishi ka mijishetwani tu kwenye tembe zetu. Kweli haya sasa ni maisha bora.
Mnazuia mkaa, bei ya umeme juu, gesi ya Mtwara haijafika Kinyeresi pamoja na vifaru kuranda mitaani. Haya mkuu. Tuone kodi yako ikihesabiwa iwekwe basi wazi. Tumezoea kuona zikikusanyiwa chungu kikubwa na kupakuliwa kiulainiiii bila kukimbizana kwa mifuko ya sandalusi. Isije kuwa yale yale. Nawaza tuu

Chagua Wachaga chadema 2020 kama hauridhiki, wakuibie mpaka Shamba lako la urithi ndo akili itakujia!
 
Mpiga dili huyo akafie mbele, sisi tunataka Kodi zetu kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu!

Dangote alikuwa halipi kodi?

Kutoza kodi kubwa ili viwanda vife ndo faida eee

Unajua kwa nini viwanda vilikufa?

acha kuimba nyimbo za kisiasa wewe, ongea kichumi na sio kisiasa wewe

unafuata mkumbo tu....tumia lugha yako...sio kufuata lugha za uchwara uchwara tu
 
Kodi kwanza, hata kama kiwanda kikifungwa, wacha kifungwe.

Hata tukibakiwa na viwanda 10 vinavyolipa kodi ni sawa.

Ajira za watanzania zitapotea ngapi?

Dangote alikuwa halipi kodi?

Angalia faida za muda mrefu wewe////

Ethiopia Dangote ana kiwanda na umeme anapata wa bei nafuu
 
We Dr Kafumu, mlipoingia mkataba mbona hamkutuambia haya note, kwa nini mliweka siri? We huo uzalendo umeutoa wapi? Kwa nini mliweka siri? Kwa nini mumpendelee Dangote? Kulikoni?? Toga, Kifaru etc? Hapa lazima maslahi yenu binafsi yameguswa ndio maana umejitokeza. Ni kwa nini viongozi wetu hamna uzalendo jamani??

acha kucomment hewa hewa tu.

Ethiopia wanampa Dangote umeme bei rahisi na kodi analipa....Ethiopia wanauza cementi Kenya na Ajira zimeongezeka
 
Haya mambo yanachanganya sana,Mkuu JPM hebu sikiliza ushauri wa wataalamu tofauti,ni kweli unataka "kutunyoosha" na ni kweli umeikita nchi ikiwa ni ya wapiga deal wa kufa mtu,lkn twenda taratibu baba,baba punguza mwendo baba....Weka mguu wa kati kuonana na breki baba.Wasikilize wataalamu baba,Wanasema "A Jack of All Trade is a Master of None".Kuwa Rais haimaniishi unaelewa kila kitu,tafuta watu wako waaminifu watakaokushauri bila woga na kukuingiza chaka.

Nimesoma maelezo ya Mkurugenzi wa Dangote,yeye anasema waliahidiwa gas,na wakahaidiwa punguzo la kodi,lkn mpaka sasa gas hawajapata na hakuna dalili,matokeo yake wanazalisha kwa ghalama kubwa kwa kutumia diesel,kodi imepanda,malighafi ipo juu,hivyo wameamua kusitisha ili kuona wanajioangaje.Na baada ya kusema tu wanafunga,Mpaka sasa Cement imepanda kwa shilingi 400 toka bei ya zamani.

Anakuja Mwijage sijui Kaijage Waziri wa Viwanda,anasema huyo mkurugenzi wa Dangote kwanza sio msemaji wa Dangote,na wala hajui mambo ya ndani ya Dangote,tena huyo ni mgeni.Yeye waziri kafanya kazi TPDC na anajua kuwa Dangote wamefunga sbb mitambo ni mibovu na si ghalama za uzalishaji.Sasa unajiuliza,hivi Waziri na Boss wa kiwanda cha Dangote nani mkweli??

Mambo haya ya ajabu sana.Nimemsikiliza na Msajili wa Hazina bwana Mafulu,nimegundua wataalamu wa Serikali wanafiki na waoga sana,hata suala la fixed Account aliyethubutu ni Gavana wa BOT tu,hata huyu Mafulu alikaa kimya
Naunga mkono hoja yako kwa maelezo haya.
Nimesoma maelezo ya Mkurugenzi wa Dangote,yeye anasema waliahidiwa gas,na wakahaidiwa punguzo la kodi,lkn mpaka sasa gas hawajapata na hakuna dalili,matokeo yake wanazalisha kwa ghalama kubwa kwa kutumia diesel,kodi imepanda,malighafi ipo juu,hivyo wameamua kusitisha ili kuona wanajioangaje.Na baada ya kusema tu wanafunga,Mpaka sasa Cement imepanda kwa shilingi 400 toka bei ya zamani.
 
Kwa ufupi wawekezaji wa aina hii ni wazembe. Naamini angekuwa anawekeza ktk nchi serious, hata kama angeahidiwa hayo yote lazima angekataa. Huwezi kufanya investment ya mabilioni ya pesa halafu ukapewa ahadi nje ya written law, nawe ukakubali. Huyo investor ana mwanasheria au anapwaga tu kwa ahadi na kushikana mikono na kila rais aliyeko madarakani? Nahisi inachangiwa na asili ya utajili wao.

Watu hawa wamepata mitaji yao kwa 'upigaji dili'. Wanaamini dili zitaendelea tu indefinitely. Sheria gani inayomlinda ktk hizo ahadi? Kafumu na wenzake walitegemea nini kwa serikali zijazo na hasa kwa kuelewa kwamba tuna viwanda vingine kwa bidhaa kama hiyo? Yaani kilio cha Kafumu ni kuheshimu ahadi! Ahadi zilizo nje ya sheria za nchi? NO thanks!
pumba
 
Kodi kwanza, hata kama kiwanda kikifungwa, wacha kifungwe.

Hata tukibakiwa na viwanda 10 vinavyolipa kodi ni sawa.
Watanzania zaidi 1000 watakosa ajira raisi amejenga viwanda vingapi mpaka raisi hao watu waende kufanya kazi huko?
 
Ajira za watanzania zitapotea ngapi?

Dangote alikuwa halipi kodi?

Angalia faida za muda mrefu wewe////

Ethiopia Dangote ana kiwanda na umeme anapata wa bei nafuu
Ndio aende huko huko Ethiopia. Sasa hapa hatutaki watu wasiolipa kodi.
 
Resolute wamelipa kodi kiasi gani kwa miaka yote waliokuwepo hapa kwetu? Nenda Nzega ukaone wameacha nini, na wananchi wamefaidika vipi na dhahabu yao iliyochukuliwa yote, au Barrick aka Acasia wamelipa nini? Tanzanite yetu Tanzaniteone wamelipa nini kwa wananchi wetu nenda Mererani ukawaulize Wananchi wamepata nini miaka yote ya kuwepo kwa Tanzanite?

Serikali ya CCM iliingia mikataba feki, Viongozi wakalamba 10% wakasepa....Now we pay pains

Kiwanda ni tofauti na Mgodi

Mgodi ni rasilimali
 
DK. KAFUMU on DANGOTE (A must read).

"Hii ni shida yetu watanzania wote, wataalamu, viongozi wa serikali na pia wanasiasa. Kwanza tuko SLOW, sijui tunaogopa kutoa maamuzi? Sijui ni taaluma duni? Sijui ni nini? Mwekezaji DANGOTE, tuliahidi kumpa malighafi ya LIMESTONE kwa ajili ya kuzalisha SARUJI kwa unafuu mkubwa; tuliahidi kumpa ardhi kwa bei nafuu au bure; tuliahidi kumpa gesi nyingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa makaa ya mawe kwa wingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa nafuu ya kodi na mengine mengi; mazingira yaliwavutia (Dangote na wenzake) sana.

Dangote wakavutika wakaja. Mimi (Dk. Kafumu) nikiwa Kamishna wa Madini wakati huo nilitimiza wajibu wangu wa kuwapa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa LIMESTONE kadri ilivyohitajika. Nawashukuru sana STAMICO walinisikiliza na kiwanda kijajengwa. Awamu ya tano (ya JPM) imekuja na mambo mapya, ahadi zingine (kwa wawekezaji) zinasuasua, sijui ni nini!

Prof Mjebda (anamtaja Prof. mwingine kwenye Whatsup Group) anaweza kutuelimisha hapa. Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa ikiwa ni pamoja na nchi kupata kodi za kutosha; ajira zitapatikana; sekta ya majenzi (ujenzi) itaimarika; uchumi utaimarika.

Ni muhimu tuwahamasishe (wawekezaji) tuangalie matokeo ya muda mrefu na siyo haya ya haraka. Kiwanda kikifungwa shida ni yetu, hebu tuwe na mioyo ya kibiashara siyo siasa za uzalendo uchwara. Samahani sana "

Dkt. Dalali Kafumu,
Kamishna Mstaafu wa Madini (Tanzania),
Mbunge wa Igunga (wa sasa),
Kada wa CCM.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Nimehariri lugha kwenye maoni hayo ya kitaalamu ya Dk. Kafumu. Tujadili seriously.
JSM.
Wakudadavuwa atasema Kafumu kafumuliwa na kutumwa na Mengi ili amuharibie Muhongo. Na hamtamuona hapa hapa huyu Wakudadavuwa pamoja timu yake.
 
Huyu anasumbuliwa na hasira za kunyimwa kazi ya Waziri wa Nishati na madini.

Mbaya zaidi anasema maneno kama vile hakuna viwanda vingine vya saruji.

Sasa ukimpa Dangote hiyo misamaha yote, hivyo viwanda vingine vya saruji nchini vitapambana naye vipi katika soko?

Kwa maana nyingine, Mtalaam wetu alitoa misamaha ili viwanda vingine vya saruji vishindwe kupambana kwenye soko na hatimaye vifungwe.

Hizi ndizo akili zinazofanana na wale wataalam wetu walikuwa wanatoa misamaha ya kodi kwa sukari wakati kuna viwanda vingine vya sukari nchini.
Hivi wakati Dangote hajajenga hicho kiwanda walio mlamba miguu na kumwomba aje awekeze hapa Tanzania ni serikali ya Hashim Rungwe na sio ccm ? Kaja kawekeza kama alivyohaidiwa sasa hivi mnamletea zengwe ..wakati ule mna mlamba miguu hamkujua kwa upuuzi huo kuwa kuna viwanda vingine vya cement ?
Halafu hapa unataka kutuaminisha jamaa kaongea haya kisa kanyimwa uwaziri

Muda mwingine muwe mnawaza kabla ya kuandika upuuzi
 
Wengine tuko serious ktk kujadili, lakini Kafumu mwenyewe tunaomba awe mtaalamu. Lugha za kisiasa ni mbaya na hatutaki.

Huwezi nishawishi kwa kutumia lugha kama hiyo; Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa. Makubwa maana yake ni nini? Toa figures. Hiki siyo kiwanda cha kwanza kuzalisha cement hapa TZ. Unaporuhusu unafuu wa aina hiyo je, umeangalia matatizo yatakayojitokeza kwa viwanda vingine ambavyo hujavipa unafuu huo? Halafu kamishna wa zamani, mwenye Ph.D anasema nchi itapata kodi za kutosha, kodi gani hizo wakati mulitoa ahadi lukuki. Tunaomba ataje ni kodi gani na kwa makadirio zitakuwa bilioni ngapi. Halafu eti sekta ya ujenzi itaimarika na uchumi utaimarika. This is no useful!

Je, misamaha hiyo iko connected na tatizo la hao makamishna na wanasiasa kuwa na hisa ktk kiwanda hicho? Je, nini hatma ya viwanda vya Twiga, Tanga cement, nk. ktk soko la ushindani?

Kafumu acheni bhla-bhla! Kama msomi tumia figures badala ya maeneo ya bungeni: Nyingi, ya kutosha, kwa wingi, inatia moyo, ya kutosha, nk. ambayo ni maneno useless!
Huyo dakitari amejikamua mafuta sasa ni muda wa kijikaanga hadharani siasa na masilahi binafsi kwenye manufaa ya nchi ndo mwisho.aibu gani hiyo hawa watu chini ya awamu ya nne walikuwa wanaigeuza Tz kuwa nigeria
 
Ndio aende huko huko Ethiopia. Sasa hapa hatutaki watu wasiolipa kodi.

Dangote alikuwa halipi Kodi? kwa hiyo anadaiwa ngapi?

Hujui mada ni nini? Umepotea na unaongea siasa na sio uchumi..

Dangote anaongelea gesi na umeme ghali na ndio sababu viwanda vingi vilikufa Tanzania

Unajua kwa nini viwanda Tanzania vilikufa? taja sababu zote...moja wapo ikiwa ufisadi wa baba zenu Fisiemu
 
Back
Top Bottom