Dr. Kafumu: Tuliahidi kumpa Dangote ardhi, gesi, makaa ya mawe, limestone kwa bei nafuu

Nina wasi wasi na udokta wake na alivyokuwa kamishna wa madini anajivunia nini na alileta impact gani
 
Resolute wamelipa kodi kiasi gani kwa miaka yote waliokuwepo hapa kwetu? Nenda Nzega ukaone wameacha nini, na wananchi wamefaidika vipi na dhahabu yao iliyochukuliwa yote, au Barrick aka Acasia wamelipa nini? Tanzanite yetu Tanzaniteone wamelipa nini kwa wananchi wetu nenda Mererani ukawaulize Wananchi wamepata nini miaka yote ya kuwepo kwa Tanzanite?
Huko Nzega hawa jamaa wa Resolute wameacha shimo la kina kirefu pamoja na uharibifu wa mazingira wa kutosha. Nina imani NEMC wanajua na wanafuatilia hambo hilo.
 
Resolute wamelipa kodi kiasi gani kwa miaka yote waliokuwepo hapa kwetu? Nenda Nzega ukaone wameacha nini, na wananchi wamefaidika vipi na dhahabu yao iliyochukuliwa yote, au Barrick aka Acasia wamelipa nini? Tanzanite yetu Tanzaniteone wamelipa nini kwa wananchi wetu nenda Mererani ukawaulize Wananchi wamepata nini miaka yote ya kuwepo kwa Tanzanite?
Hivi nani aliyeingia nao mkataba? Hao unaowatetea hawakujua hayo mambo? Nani asiyejua ulaji uliokuwa unapatikana ndani ya chama? Ccm wenyewe ndiyo wakwanza kuliga dili. Mda huu hatuongelei porojo. Jibu hoja za kafumu na dangote kinadharia na siyo kimaneno. Dangote hana miaka miwili kuanzia aanze uzalishaji, mkubwa wenu hakuwepo kwenye baraza la mawaziri? Kwa nini hakuliona hilo?
 
Ni wazi kuwa tuna viongozi ambao hawana uzalendo na taifa hili. Kama Kafumu anavyosema tuache uzalendo uchwara, tuangalie manufaa ya muda mrefu katika kila sekta
 
KADIRI SIKU ZINAVYOENDELEA NENO Uchwara linazidi kushika kasi.Ilianza dikteta uchwara,na sasa imeingia uzalendo uchwara. Ngoja tusubiri uchwara mwingine unakuja.........................
 
Wazungurusha mikono na washika ukuta mmeona suala la Dangote ndiyo point yenu kisiasa kuikosoa serikali yetu pendwa, fukuzeni mafisadi mnaowalea kwanza.
Na nyie wazungusha viuno mnaua viwanda huku mnaimba nchi ya viwanda labda nchi ya VITANDA siyo viwanda nnavyovijua mimi.
 
Hayo maarifa ya huyo jamaa ni kuuza nchi, haiwezekani watu wenye akili tmamu mumpe vitu hivyo vyote kwa unafuu huo, haiwezekani!!
Unajua kiwanda cha Dangote kimetoa ajira kwa watanzania wangapi? Uwe unajiongeza kabla ya kuandika pumba
 
DK. KAFUMU on DANGOTE (A must read).

"Hii ni shida yetu watanzania wote, wataalamu, viongozi wa serikali na pia wanasiasa. Kwanza tuko SLOW, sijui tunaogopa kutoa maamuzi? Sijui ni taaluma duni? Sijui ni nini? Mwekezaji DANGOTE, tuliahidi kumpa malighafi ya LIMESTONE kwa ajili ya kuzalisha SARUJI kwa unafuu mkubwa; tuliahidi kumpa ardhi kwa bei nafuu au bure; tuliahidi kumpa gesi nyingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa makaa ya mawe kwa wingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa nafuu ya kodi na mengine mengi; mazingira yaliwavutia (Dangote na wenzake) sana. Dangote wakavutika wakaja. Mimi (Dk. Kafumu) nikiwa Kamishna wa Madini wakati huo nilitimiza wajibu wangu wa kuwapa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa LIMESTONE kadri ilivyohitajika. Nawashukuru sana STAMICO walinisikiliza na kiwanda kijajengwa. Awamu ya tano (ya JPM) imekuja na mambo mapya, ahadi zingine (kwa wawekezaji) zinasuasua, sijui ni nini! Prof Mjebda (anamtaja Prof. mwingine kwenye Whatsup Group) anaweza kutuelimisha hapa. Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa ikiwa ni pamoja na nchi kupata kodi za kutosha; ajira zitapatikana; sekta ya majenzi (ujenzi) itaimarika; uchumi utaimarika. Ni muhimu tuwahamasishe (wawekezaji) tuangalie matokeo ya muda mrefu na siyo haya ya haraka. Kiwanda kikifungwa shida ni yetu, hebu tuwe na mioyo ya kibiashara siyo siasa za uzalendo uchwara. Samahani sana "

Dkt. Dalali Kafumu,
Kamishna Mstaafu wa Madini (Tanzania),
Mbunge wa Igunga (wa sasa),
Kada wa CCM.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Nimehariri lugha kwenye maoni hayo ya kitaalamu ya Dk. Kafumu. Tujadili seriously.
JSM.
Hizi habari za kufungwa kwa kiwanda cha Dangote eti, sababu ya kushindwa kukiendesha kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa sio za kweli hata kidogo. Taarifa sahihi na zenye ukweli ni kwamba, kiwanda cha Dangote kipo kwenye matengenezo makubwa ya mitambo yake baada ya kutokea hitilafu za kiufundi. Acheni upotoshaji usiokuwa na tija!
 
Mpiga dili huyo akafie mbele, sisi tunataka Kodi zetu kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu!
Ivi wewe na wenzako hii posho mnayopata(7000) inasababisha mnasaliti ndugu zenu wanaokufa njaa uko vijijini, kwa nini nyeupe msiseme ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi? Mmelishwa unga wa ndere? Ni nani atuletee unga wa rutuba tuiponye nchi hii dhidi ya vijana walolishwa unga wa ndere?
 
Unaweza kweli ukawa serious kujadili, lakini bahati mbaya kipande hiki cha observation ya Dk Kafumu (nilivyoelewa mimi) imechotwa kutoka kwenye mjadala kwenye group lake la whatsap, hivyo hakuna mtiririko wa yote aliyonena huko, lakini angalau kipande hiki kinajaribu kuonyesha kuna tatizo mahali fulani, na kwa uelewa wangu ninaona kama Dk Kafumu ana expose mgongano uliopo katika ku-treat investors. Kipande cha andishi la Dk Kafumu linatoa angalizo kwamba sisi ni double standard kwa wawekezaji!
Kwa ufupi wawekezaji wa aina hii ni wazembe. Naamini angekuwa anawekeza ktk nchi serious, hata kama angeahidiwa hayo yote lazima angekataa. Huwezi kufanya investment ya mabilioni ya pesa halafu ukapewa ahadi nje ya written law, nawe ukakubali. Huyo investor ana mwanasheria au anapwaga tu kwa ahadi na kushikana mikono na kila rais aliyeko madarakani? Nahisi inachangiwa na asili ya utajili wao.

Watu hawa wamepata mitaji yao kwa 'upigaji dili'. Wanaamini dili zitaendelea tu indefinitely. Sheria gani inayomlinda ktk hizo ahadi? Kafumu na wenzake walitegemea nini kwa serikali zijazo na hasa kwa kuelewa kwamba tuna viwanda vingine kwa bidhaa kama hiyo? Yaani kilio cha Kafumu ni kuheshimu ahadi! Ahadi zilizo nje ya sheria za nchi? NO thanks!
 
Back
Top Bottom