Dr Kafumu: Kama uchaguzi utarudiwa sintoshiriki kama mgombea

Ptz

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
541
384
Dr Dalaly Peter Kafumu yuko anahojiwa Star tv sahizi katika kipindi cha "Medani za kisiasa" anasema hayuko tayari kugombea tena ubunge kama rufaa yake itashindwa na kuwa ataendelea kushiriki kuleta maendeleo ya Igunga nje na Ubunge
 
Dr Dalaly Peter Kafumu yuko anahojiwa Star tv sahizi katika kipindi cha "Medani za kisiasa" anasema hayuko tayari kugombea tena ubunge kama rufaa yake itashindwa na kuwa ataendelea kushiriki kuleta maendeleo ya Igunga nje na Ubunge

Hayuko kambi ya BABA EL so anajua hawezi kushinda tena hata siku moja .
 
Naona na mtoto wake Benedict Kafumu nae ameshachaguliwa mwakilishi wa wilaya wa CCM. Amakweli CCM ni BM-VW. Baba, mama, Vimada na watoto.
 
Mi huyu ndie kiongoz bora kwani amefanya maamuz sahii ili pia ameachia viongoz wa CCM wenye uwezo wagombee. Na tutambue kuwa co lazima uwe mbunge ndio ufanye shuguli za maendelee. Hongera Dr kafumu
 
Naona damu za watu walizomwaga na mwenzie Mwigulu Chemba zinamkosesha amani anajiuliza atawarudia vipi wana Igunga. Na saizi wananchi wameuza pamba na mvua zimeanza hawatadanganyika na chakula cha msaada. Heri abakie na aibu ya kujiangusha kuliko fedheha ya kushindwa ubunge
 
Anasema yeye si fisadi.anatakiwa kufunzwa maana ya ufisadi kwani nadhani uozo ulioko ktk sekta ya madini na yeye lazima alichangia kwa kutenda ama kwa kuachia wengine watende.anasema chadema wanakichonganisha na wananchi.hajui kuwa ni ccm ndiyo wanajichonganisha ccm na wananchi.chadema inachofanya ni kuwaweza wananchi kujua kuwa matatizo waliyonayo ni kwa sababu ya ufisadi wa ccm.
 
Ccm haiwezi shinda popote tanzania kihalali kwa sasa kwani mambo kwishaharibika
 
Katika hali ya sasa kugombea chochote kupitia CCM lazima uwe na mtandao wako pamoja na nguvu nyingi sana ya kifedha. Kugombea kupitia CCM kwa sasa ni ngumu sana. Utaongea sera gani watu wa kuelewa wakati kila kitu kipo kwenye nchi yetu kipo as if ni autopilot..watu wanajichukulia maamuzi yao wenyewe bila kukemewa..its hard.
 
polisi wanaua mwandishi mwangosi na picha zionaonyesha live tukio alafu tume inasema polisi hawausiki. hii ni moja ya v2 vitakavyoigarim ccm ktk chaguzi zake ukiachilia mbali matatizo ya kijamii kama elimu bora, afya bora, ajira n.k. wa2 wengi sana wameelimika japo sio sana lkn kwa elimu hiyohioyo ndogo ya kijamii ndio inayowanya wananchi kuchukua maamuzi ambayo kwao no sahihi. waliona kbs uchaguzi uliofanyika igunga ilivyogharimu maisha ya w2 na ubabe wa viongozi kubeba silaha m?ajukwaani sasa hawatakua tayari kutum?ika kama karai wakati wa ujenzi alafu ujenzi ukiisha karai halina tena thamani.
 
Ningekuwa Kafumu ningesema: Naachana na Siasa za makundi, na siasa uchwara. Napigania mgombea halali wa chama atakayepita bila ya rushwa au upendeleo wa aina yoyote. Napigania uchaguzi huru na wa haki usiokuwa na mizengwe yoyote!
Alamsiki!
 
Jamaa kwa nini asimwambie Nape kuwa amechoshwa na siasa uchwara?
 
Dr Dalaly Peter Kafumu yuko anahojiwa Star tv sahizi katika kipindi cha "Medani za kisiasa" anasema hayuko tayari kugombea tena ubunge kama rufaa yake itashindwa na kuwa ataendelea kushiriki kuleta maendeleo ya Igunga nje na Ubunge

Asiudanganye uma. Makosa yaliyosababisha avuliwe ubunge yanatokana na rushwa, hivyo sheria hazimruhusu kugombea ubunge au uongozi wowotewa uma kwa muda wa miaka kumi. Asijifanye hataki kugombea.
 
Back
Top Bottom