Dr. Joyce Ndelichako (NECTA) alichemka kwa kitendo cha Kumshambulia kijana Julius | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Joyce Ndelichako (NECTA) alichemka kwa kitendo cha Kumshambulia kijana Julius

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwakalinga Y. R, Jul 12, 2012.

 1. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Leo asubuhi nimefanikiwa kusikiliza Interview ya kijana Julius aliyeandika Verses/Rhymes ama mistari ya hip hop -bongofleva kwenye karatasi ya majibu mtihani wa Form 4- NECTA uliofanywa 2011.Kitendo cha Joyce Ndelichako (PhD) kwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kusoma kilichoandikwa,kwa maoni yangu nathubutu kuandika kuwa alikurupuka,haiingii akilini mwanafunzi kuandika mambo yale kwenye karatasi ya majibu halafu mtu mwenye taaluma ya juu (PhD) kama mama Joyce kushindwa kutafuta sababu za mwanafunzi yule kwa nini aliandika mambo yale tena kwa ujasiri wa kiwango kile.

  Kijana Julius asubuhi ya leo katika kwenye kipindi cha Power Breakfast-Clouds fm, kwa kinywa chake mwenyewe amesema alifanya vile kama kufikisha ujumbe kwa Watanzania kuwa mfumo wa elimu haulengi kuwaelekeza vijana /watoto kwenye mambo wanayoyajua kwa ufasaa.Unapomwelekeza mtoto/mwanafunzi kwenye mambo anayoyapenda na kuyaamini kuwa yatamsaidia yeye kuweza kujiingiza katika shughuli halali za uzalishaji inasaidia kutumia rasilimali chache kumfikisha huyo mwanafunzi/mtoto mahala pazuri kwa manufaa yake na taifa kwa ujumla.Pia ameelezea kuwa yeye aligundua kuwa ana kipaji cha music ila hakupewa fursa hiyo kutokana na mfumo wa elimu uliopo,ujumbe aliotaka kufikisha kwa jamii ,ni kiasa jamii ithamini taaluma na fani mbalimbali kwa mrengo wa kuwakomboa wananchi/vijana wasio na ajira.

  Julius ametoa mifano hata hawa kina Diamond tunaowaona leo ,wazizi wao walikuwa wanakimbizana nao wakiwalazimisha kwenda shule pasipo kutambua vipaji vyao.Hata wazazi/walezi wa baadhi ya wasanii hawa mara kwa mara wammekuwa wakihojiwa na kukiri kuwa vijana wao walikuwa hawapendi shule ila leo wanajivunia mafanikio yao.Kwenda shule ni jambo jema ila mfumo uendane na mahitaji/mazingira ya jamii husika.


  My take;
  Inashangaza sana kuwa Tanzania kuwa watu wana taaluma na wanaitwa Maprofesa,madaktari wa falsafa wameshindwa kuona matatizo ya ufumo wa elimu yetu katika kuwasaidia vijana/watoto na taifa kwa ujumla.Nimesikiliza pia single mpya ya Kijana Julius ameonyesha uwezo wa juu sana kama msanii chipukizi.Julius aliwasilisha kilio cha wengi kwa njia ile-hivyo naye ni Mwanaharakati, naamini itakuwa fundisho na somo kwa baraza la mitihani.
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Takataka (uchafu) ni kitu chochote kilichopo eneo lisiloruhusiwa/ husika....Swali lilimtaka aandike mashairi ya music?? Kwanini alipoteza mda na pesa za wazazi si angejiondoa mapema ili ayakarabati mashairi yake vizuri na sasa angekuwa na albam nzima!! Pili kuna somo la Music...na linatahiniwa na NECTA ...na ni kozi ambayo angeweza ku-opt.....ili aendeleze kipaji chake kitaalamu zaidi..

  Siungi mkono hoja!
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hapa naona kama unamwonea Dr Ndalichako. Wao (NECTA), pamoja mambo mengine kazi yao kubwa ni kutunga na kusahihisha mitihani kwa mujibu syllabus ambayo imeandaliwa kwa kuzingatia sera, sheria na taratibu zilizopo kwa wakati huo (ambazo Dr Ndalichako sio muhusika wa uandaaji wake). Labda kama hoja yako ni mitihani inayotungwa kutoendana na syllabus iliyopo.
   
 4. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kila jambo lina wakati wake, angependa mziki angeenda bagamoyo chuo cha sanaa, maana kule NECTA si sehemu yake...
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Siungi mkono hoja kwa 100%. Kwenye mitihani, ambapo msahihishaji wa swali ni mtu mmoja tukiongezea na mkaguzi pengine wanaweza kufika 10 as maximum people to read that article. Sasa huyu Julius anasema alikusudia kufikisha ujumbe kwa watanzania kihivyo kweli? No way, hakuwa serious na alichokuwa anakifanya.
   
 6. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Upumbavu kabisa na wote siyo huyo kijana hata Clouds wenyewe.Muziki gani pasipo na shule ya maana au ni producer gani anaingia studio bila kuwa na elimu bora kama sound engineering,electrical etc.Pia kumbukeni kuwa muziki ni taaluma inasomewa darasani kama ilvyoprofessional zingine.Na nzuri zaidi kama hajui na wote nyie ni kwamba shule nzuri zina option ya kuendelea na masomo ya kawaida na muziki ikiwa kama somo la ziada na unakuta shuleni wanafunzi wanaofanya option ya muziki wanatoa burudani kama kawaida utafikiri kuna mabingwa kama Michael Jackson vile.Muhimu ni kwamba shule zetu za serikali ziajiri walimu wa muziki na masomo mengine ya michezo ili kuwapa skills na kuendeleza viapaji vyao wanao taka, otherwise ni ujinga kutetea mawazo ya huyo mwanafunzi aliyeshindwa kujibu mitihani na kuibukia kwenye upumbavu wake wa kuandika mashairi.
   
 7. s

  sawabho JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hii tabia ya kuendekeza Uanaharakati kila sehemu italimaliza taifa !!! Yaani mtu atahiniwe somo lingine, atoe majibu ya somo lingine, halafu tuseme ana kipaji, kipaji gani hicho kisichojali muda na mahali ? Kila kitu kina utaratibu wake. Kama alikuwa na kipaji cha muziki alitakiwa kumweleza mzazi wake mapema kuwa anahitaji shule ya muziki, apelekwe Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Hata hivyo, kuna umuhimu wa kumaliza elimu ya Msingi na Upili ili kumjengea mtoto Uelewa wa Taifa lake kuhusiana na mataifa mengine kabla ya kuanza kutafuta elimu ya fani kama vile kwenda VETA au Vyuo vya Sanaa. Hao wanaokimbilia muziki wakiwa kidato cha kwanza ndio hao tunaowaona wakifanya fujo mitaani na kuwa limbukeni, baada ya muda anaigizwa na "Original Comedy" aikiwa "aliyefulia" !!! maana hawana elimu ya maisha akipapata millioni 5 anaona kapata pesa !!!!
   
 8. k

  kiwososa JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,083
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Aliyemdanganya huyo dogo akienda shule hataimba ni nani? elimu ya form four level ni basic sana kwa maisha ya sasa mahali popote na katika fani yeyote
  Huyo dogo ni kilaza tu ndo maana hata kwenye huo muziki anaodai anauweza ni kazi bure kama ameshindwa hata kusoma na kujibu mtihani wa form 4
  SIUNGI MKONO HOJA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Huyo dogo ni mpumbavu,angekua mjinga angegundua makosa yake kitambo!
   
 10. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 734
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Na wewe ni jamii ya julius, we ulitaka dr. hafurai, alikosa njia ya kufikisha ujumbe? ni kilaza tu huyo, maswali yalimuona. Mwanzisha thread na julius wote ni VILAZA.
  CPA(T)
   
 11. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  We uunge mkono hoja usiunge poa tu! cha msingi msg sent! we unadhani huu mfumo wa elimu uliopo unamuandaa mtoto kujipanga kimaisha!? hakuna kitu zaidi ni mambo ya kimawazo zaidi kuliko vitendo,yeye amepeleka ujumbe hata kama haukutakiwa kuwa pale wakati ule bali umefika.
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hakuna ujumbe wowote uliofika hapo sana kapoteza muda wake na pesa ya mzazi/mlezi wake! Ajiandae kuwa kibaka ama kutumikishwa na vidume mjini!
   
 13. s

  sawabho JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kwa nini asimalize kidato cha nne, sita au Chuo Kikuu ili kupata elimu ya jumla halafu akaenda VETA au Chuo cha Sanaa kupata elimu ya fani ?. Mfumo gani huo unataka umwandae mtu kimaisha kabla hajafahamu kusoma na kuandika au kujieleza kwa ufasaha, huyo ataishia kuimba nyimbo na kudhulumiwa na wale wenye maduka pale Kariakoo kwa sababu ataingia mikataba asiyofahamu maana yake.
   
 14. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,267
  Trophy Points: 280
  Kwa wadau wa fani Kama sisi, dogo alifikisha ujumbe.

  Hata mimi nimemsikia asubuhi, kafunguka vizuri tu, Na kasema watu wasimuone Kama yeye ni jeuri.

  Kasema kua watu wanatahiniwa kwa vitu ambavyo havitakuja kuwasaidia maishani.

  Historia yake inaonyesha kua elimu haikua Bahati yake, kwani kamaliza form4 akiwa Na miaka 22 baada ya kurudia rudia na kuhama hama sana. Kusoma yenyewe kasoma kwa tabu sana.

  Hao kina Diamond ukifuatisha utakuta form4 kamaliza kwa mbinde, labda hata "kazungusha", lakini leo anatembelea VX ambayo wengine Na MBA zao hawana.

  Dogo yuko juu, Ndalichako alikosea.
   
 15. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nini una shindwa kufikiri?
  Kwa hiyo unaona hapo palikuwa ni sehemu sahihi pa yeye kuandika huo ujumbe?
  Angalia usije ukawa una tetea vitu visivyo na msingi kabisa na tumaini wewe ni mtu mzima!

  Je kwenye huo mtihani kulikuwa na swali linalo huyu kutoa maoni kama hayo?

  Jaribu kufikiri kwa kina kabla ya kupost.
   
 16. okaoni

  okaoni JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 1,197
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  pale ambapo mtu anajibu kitu tofauti kabisa na alichoulizwa yawezekana akawa eitha ni philosopher au anaakili nyingi zaidi ya kawaida au kuna tatizo la ubongo ikiwa na ugonjwa au matumizi ya madawa ya kulevya.kwa maelezo yake amerudia mtihani ya form two mara nyingi hivyo kwenye akili nyingi hayupo.nadhani ni madawa ya kulevya yanamtuma kufanya vituko
   
 17. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kweli kwa nilivyomsikiliza dogo ana upeo wa kufikiri tofauti na jinsi watu walivyomchukulia
   
 18. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nitaongeza uwezo wangu wa kufikiri ,ila ujumbe amefikisha nampongeza
   
 19. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kumbe unauelewa kuwa alikuwa anapoteza fedha za wazazi wake kwa mfumo mbovu wa elimu.Soma haya maelezo

  Unapomwelekeza mtoto/mwanafunzi kwenye mambo anayoyapenda na kuyaamini kuwa yatamsaidia yeye kuweza kujiingiza katika shughuli halali za uzalishaji inasaidia kutumia rasilimali chache kumfikisha huyo mwanafunzi/mtoto mahala pazuri kwa manufaa yake na taifa kwa ujumla.Pia ameelezea kuwa yeye aligundua kuwa ana kipaji cha music ila hakupewa fursa hiyo kutokana na mfumo wa elimu uliopo,ujumbe aliotaka kufikisha kwa jamii ,ni kiasa jamii ithamini taaluma na fani mbalimbali kwa mrengo wa kuwakomboa wananchi/vijana wasio na ajira
   
 20. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nimepoteza muda wangu kuisoma hii thread.
   
Loading...