DR Jonas Tiboroha alitakiwa awe mwenyekiti wa Yanga

Bukali

JF-Expert Member
May 7, 2018
708
500
Dr Tiboroha, ndiye hasa alitakiwa awe mwenyekiti wa Yanga.

Kipindi akiwa katibu mkuu, aliifanya Yanga kuwa timu tishio sana Tanzania.

Angalia scout ya Wachezeji kama Ngoma, Kamsoko, Twite. Ni watu ambao walikuja Yanga wakiwa wanafahamu kazi yao ni kufanya nini.
Yanga ya Msola na Dj Mwakalebela, inapesa za GSM lakin wanaosajiliwa kwa kweli hata sijui wanakuja kufanya nini? Angalia usajili wa Sapong, Fiston, Yakuba. Ambao ni straika hakuna wanacho fanya, tuwape mda ndo umekuwa wimbo.

Fiston ni bora wangelivunja mkataba wa Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar ama kumlejesha Molinga. Sasa naona hata katikati wanakata viuno tu, Feitoto timu ikiwa imezidiwa hawezi kupushi. Naona pengo la Juma Abdul kupandisha mashambulizi.

Beki nayo imesahau kuweka marking ya ukabaji wanarundikana eneo moja yaani wanafuata mpira wote. Uongozi wa Yondani pengo lake limeonekana. Yanga tusitafute mchawi eti tunahujumiwa how?

Au marefa wanatuminya siyo kweli, maana tengeneza nafasi nyingi then funga ilikusudi maholi ya kataliwe tione. Scout ya Yanga haipo kabisa, viongozi hakuna wanachofanya wanawaza kula pesa ya GSM.

Usajili wa bado sana, sasa kuna hatari tena ya kutema timu karibu nusu. Kupisha usajili wa magumashi.
 
Anigrain

JF-Expert Member
Nov 15, 2020
281
500
Yanga bana, wakishinda sifa zote wanapewa kina GSM kupitia injiania hersi Kwa kuwaletea wachezaji na kuiweka team kwenye mazingira mazuri ya kambi na kutoa posho Ila wakitoa draw lawama zinaenda Kwa msola utazani yeye ndio alikuwa anaenda Airport kupokea wachezaji

Hakuna taasisi rahisi kuongoza kama yanga maana akili za wapenzi,mashabiki,wanachama zinafanana Sana, team ikipata matokeo mabaya uongozi unaita press wanataja watu wa kulaumiwa then mashabiki nao wanaunga Tela, Ila kiuhalisia yanga uwezo wake ni mdogo Sana wapo pale juu Kwa sababu ya historia Yao na nguvu ya mashabiki, azam wana kikosi kizuri kuliko yanga Ila wanakosa pressure ya mashabiki kutaka matokeo na kuhoji pindi wanapofanya vibaya, ni kama vile ligi kuu ya England maji yashajitenga na mafuta na VPL nayo ndio inaelekea huko

Ndugu zangu watani wekezeni kwenye kiwanja mtapata team nzuri Ila mkiendekeza hizo janja janja mtamaliza nafasi ya 2 ata miaka 8, ukweli usemwe Tu quality ya wachezaji wa Simba ni kubwa Sana basi Tu kwakuwa wanacheza na ihefu ligi moja tunachukulia kawaida, huwezi kuwa na forwardline ya sarpong,kisinda,nchimbi,waziri junior,fiston,faridi utegemee kupata ubingwa mbele ya team yenye bocco,kagere,mugalu,Luis,chama, Morrison, nunueni wachezaji wenye quality ndugu zangu muache kucheza Kwa kuhamasishwa na mcheze Kwa uwezo
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
29,425
2,000
Lijinga sana hili.
.
FB_IMG_1614921759508.jpg
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
8,436
2,000
Dr Tiboroha, ndiye hasa alitakiwa awe mwenyekiti wa Yanga.

Kipindi akiwa katibu mkuu, aliifanya Yanga kuwa timu tishio sana Tanzania.

Angalia scout ya Wachezeji kama Ngoma, Kamsoko, Twite. Ni watu ambao walikuja Yanga wakiwa wanafahamu kazi yao ni kufanya nini.
Yanga ya Msola na Dj Mwakalebela, inapesa za GSM lakin wanaosajiliwa kwa kweli hata sijui wanakuja kufanya nini? Angalia usajili wa Sapong, Fiston, Yakuba. Ambao ni straika hakuna wanacho fanya, tuwape mda ndo umekuwa wimbo.

Fiston ni bora wangelivunja mkataba wa Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar ama kumlejesha Molinga. Sasa naona hata katikati wanakata viuno tu, Feitoto timu ikiwa imezidiwa hawezi kupushi. Naona pengo la Juma Abdul kupandisha mashambulizi.

Beki nayo imesahau kuweka marking ya ukabaji wanarundikana eneo moja yaani wanafuata mpira wote. Uongozi wa Yondani pengo lake limeonekana. Yanga tusitafute mchawi eti tunahujumiwa how?

Au marefa wanatuminya siyo kweli, maana tengeneza nafasi nyingi then funga ilikusudi maholi ya kataliwe tione. Scout ya Yanga haipo kabisa, viongozi hakuna wanachofanya wanawaza kula pesa ya GSM.

Usajili wa bado sana, sasa kuna hatari tena ya kutema timu karibu nusu. Kupisha usajili wa magumashi.
Yanga inahujumiwa na Viongozi na Kocha! Usajili wa Fiston unatia aibu! Yule Saido Ntibazonkiza nae ni spana mkononi!! Mpaka leo tunawategemea Sarpong na Nchimbi watuokoe!

Timu haina kabisa morali!! Sijui kuna mgomo baridi unaendelea ndani kwa ndani!! Naona dalili za ubingwa zinaanza kuyeyuka baada ya sare mfululizo na kipigo kutoka kwa hawa vibonde Coastal Union a.k.a Simba B.
 
Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,459

Hamna mgomo timu yetu n mbovu tu lilikuwa n suala la muda tu timu yetu kufungwa angalia mechi ya kujipima na African sport timu ilivyocheza eti tukajipa matumain kuwa ile n mechi ya kujipima tu tukaenda mbeya angalia rythm ya timu ilionesha Kuna shida sehemu

Baadaye na kagera magoli ya hovyo beki mbovu hapo mashabiki walianza shtuka nakupiga kelele

Ushindi wa mbinde na mtibwa kengold nadhan king'ora kililia kule ugenini baada kupoteza Jana

Ukiangalia mlolongo huu utajua tu timu Haina ile consistency

Wachezaji wanasubir molari ya mashabiki na viongozi ili wacheze naiona sare na polisi

Timu ikirudi dsm kuna mawili kutokea kocha msaidiz kuondoshwa kuja mwambusi au kiongoz mkubwa kujiuzuru

Au hata kocha mkuu kutimuliwa

HAYA YOTE YATATEGEMEA MATOKEO YA JUMAPILI
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
29,425
2,000
Yanga inahujumiwa na Viongozi na Kocha! Usajili wa Fiston unatia aibu! Yule Saido Ntibazonkiza nae ni spana mkononi!! Mpaka leo tunawategemea Sarpong na Nchimbi watuokoe!

Timu haina kabisa morali!! Sijui kuna mgomo baridi unaendelea ndani kwa ndani!! Naona dalili za ubingwa zinaanza kuyeyuka baada ya sare mfululizo na kipigo kutoka kwa hawa vibonde Coastal Union a.k.a Simba B.
Suala la kuwa kuna kamgomo fulani siyo siri tena wachezaji wazawa hawana morali kabisaaaaa hebu ona huyo dogo anavyofanya masihara. Msola na Mwakalebela watawagharimu sana,wanamkatisha tamaa mwekezaji kwani hawana mchango wowote kwa Club zaidi ya kutoa matamko ya kuwachochea washabiki kuwa TFF, Simba na marefa wanaihujumu Yanga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom