Nyamtalakyono
JF-Expert Member
- Dec 17, 2015
- 795
- 479
Rais wangu John Pombe Magufuli Salaam, Napenda kusema kuwa katika maisha yangu sitaacha kukuamini maana ni kwa kipindi kirefu toka ukiwa waziri nimefuatilia kauli zako nautendaji wako wa Kazi na nimebaini wewe ni mtu mwema unayejali utu wa mtu na hasa wale wanyonge ambao wanakosa pa kusemea. Mh Rais wangu mpendwa, pamoja na watu wengi hasa wale wasioitakia mema nchi kusema mambo mengi na kukuita majina mengi yasiyofaa naomba usikate tamaa Bali chapa Kazi maana hata Yesu wapo waliomkataa lakini leo wanaomba arudi lakini kelele za mlango haziwezi kumzuia mwenye nyumba kupata usingizi. Naomba siku zote usiache kusema ukweli hata kama hauwafurahishi wengi. MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU. Tutazidi kukuombea.