Dr Jakaya Kikwete afuata ushauri wa mwanahabari Masyaga Matinyi?

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,883
31,049
New Habari wahitilafiana uteuzi wa Zakia Meghji

Mwandishi Wetu
Novemba 24, 2010


KIWEWE cha uteuzi wa Baraza la Mawaziri kimesambaa kutoka miongoni mwa wateule watarajiwa hadi katika makundi mengine wakiwamo baadhi ya wanahabari na vyumba vya habari na kuibua mivutano saa zaidi ya 24 kabla ya Rais Jakaya Kikwete kufanya uteuzi, Raia Mwema imebaini.

Katika chumba cha habari cha New Habari Corp, mhariri wa habari wa gazeti la kila Jumapili ameingia matatani na mhariri mkuu baada ya kuandika makala kwenye gazeti hilo akitoa angalizo kwa Rais Kikwete kutomteua kuwa waziri mmoja wa vigogo kati ya watatu aliowateua kuwa wabunge.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais anapewa nafasi ya kuteua wabunge 10 na amekwishatumia nafasi hiyo kwa kuteua watatu wiki iliyopita.

Waliokwishakuteuliwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Maliasili na Utalii, Zakia Meghji na Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.

Baada ya uteuzi huo kufanyika, zilijengeka hisia kwamba kuna uwezakano mkubwa wa wateule hao kupata uteuzi mwingine na kuwamo kwenye Baraza la Mawaziri, ambalo katika hotuba yake ya kuzindua Bunge Alhamisi wiki iliyopita, Rais Kikwete alisema litakuwa la waadilifu na wachapakazi.

Hata hivyo, kabla ya uteuzi huo mhariri huyo wa habari wa gazeti la Mtanzania Jumapili, Masyaga Matinyi aliandika makala katika safu yake ya Tuzungumze Jumapili yenye kichwa cha habari “JK angalizo kuhusu Meghji”

Katika makala hayo, anatoa angalizo kuwa Meghji hastahili kuteuliwa kuwa waziri kwa sababu baadhi ya wizara alizopata kuziongoza zilidorora kiutendaji na hata kuwa na kashfa wakati wa uongozi wake, akitolea mfano Wizara ya Maliasili na Utalii, achilia mbali Wizara ya Fedha ambako Rais Kikwete hakumrejesha tena baada ya Serikali ya awali kuvunjwa.

Safu hiyo ambayo kwa kawaida ni maoni ya mtu binafsi na si msimamo wa gazeti au kampuni, Masyaga anaandika; “Nadhani kwa wale wafuatiliaji wa mambo mtakumbuka hali ilivyokuwa wizarani hapo (Maliasili na Utalii) wakati huo (Meghji akiwa Waziri), ambako Katibu Mkuu alikuwa Philemon Luhanjo, ambaye kwa sasa ndiye Katibu Mkuu Kiongozi anayejiandaa kung’atuka kisheria.”

“Labda tukumbushane machache, wakati wawili hao wakiongoza wizara hiyo, sekta ya uwindaji wa kitalii iligubikwa na matatizo mengi, ikiwamo rushwa, wizi wa maliasili zitokanazo na wanyama, upendeleo katika ugawaji wa vitalu…ambako inadaiwa hata mama Meghji naye ama anamiliki vitalu au familia yake imo kwenye biashara hiyo nono.

“…Kuna baadhi ya wamiliki wa vitalu wasio Watanzania waliweza kumiliki vitalu vitano au zaidi na kuhodhi kabisa biashara hiyo ambayo kimsingi inapaswa kuwanufaisha Watanzania kwanza.

“Hivyo uteuzi wa mama Meghji kuwa Mbunge bila shaka kwa njia moja ama nyingine unatokana na wajanja hao ambao sasa wanaona kuna kila dalili za kubanwa hasa na Ofisi ya Waziri Mkuu, na sasa wanapambana kumrejesha mtu wao ili waendelee kutafuna utajiri wetu.

Anaendelea kuandika; “Baadhi yetu juzi tulishangaa sana, siku ambapo Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiapishwa, tulimuona mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa wa uwindaji wa kitalii akiwa amekaa kwenye jukwaa kuu la viongozi. Sasa tukabaki tunajiuliza ana umuhimu gani hadi akae pale, sehemu ambayo hata mawaziri waliokuwa wakimaliza muda wao hawakuruhusiwa kukaa.”

Hata hivyo, baada ya kuandika makala hiyo, gazeti la siku iliyofuata la kampuni hiyo (Novemba 22, 2010), Mhariri aliandika taarifa ya kumuomba radhi Meghji; yenye kichwa cha habari: Kunradhi Meghji.
Katika taraifa hiyo iliyochapishwa ukurasa wa mbele, mhariri anaandika; “Katika toleo la jana, No 5301 la Novemba 21, 2010 katika ukurasa wa 8, mwandishi Masyaga Matinyi aliandika makala yenye kichwa cha habari kisemacho “JK angalizo kuhusu Meghji.”

Katika makala hiyo Matinyi alikuwa akimshauri Rais Jakaya Kikwete asimteue Zakia Meghji katika Baraza la Mawaziri lijalo kwa kutoa tuhuma nyingi dhidi ya Meghji.”

“…..makala aliyoandika Matinyi imevunja maadili ya uandishi wa habari na sera ya Gazeti la Mtanzania ya kutochafua wala kushambulia watu, kwa hiyo tunapenda kuchukua fursa hii kumuomba radhi Meghji..Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo na Rais Kikwete.

“Kwa upande wetu, Matinyi tunaahidi kumchukulia hatua za nidhamu kwa mujibu wa sheria za kazi na hasa kutokana na mwendelezo wake wa kuandika makala zenye mwelekeo wa kuchagua watu au taasisi, hata baada ya kuonywa asifanye hivyo, kana kwamba anao msukumo zaidi ya kuandika habari au makala za kawaida.

Kutokana na mvutano huo, Raia Mwema liliwatafuta wahusika hao, mhariri wa habari na mhariri wake mkuu ili kujua kilichojiri hasa kwa wadau hao wa tasnia ya habari inayopaswa kutumikia umma na si kuwaonea au kuwabeba watu au viongozi kwa maslahi binafsi.

Kwa upande wake, Matinyi Masyaga aliliambia Raia Mwema kuwa bado anasimamia kile alichokiandika kwa kuwa anavyo vielelezo vya kutosha na kwamba mara baada ya mhariri wake kuandika kunradhi, sehemu ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wameahidi kumwaga vielelzo zaidi kwa Matinyi vinavyothibitisha kile kinachotajwa uovu wa Meghji wizarani hapo.

Kwa mujibu wa Matinyi vielelezo hivyo vinahusu ugawaji na umiliki wa vitalu vya uwindaji na biashara ya nyara za serikali pamoja na baadhi ya kampuni za utalii, baadhi zikiwa na makao yake Arusha, kutolipa mapato kama inavyopaswa.

“Kiongozi wa namna hii kumrejeshea tena uwaziri nchi hii inakwenda wapi kamanda? Hivi hakuna Watanzania wengine wasio na madoa kiutendaji wakapewa kazi hiyo? Tunazo taarifa wanaonufaika na sekta ya uwindaji wa kitalii wanahaha kuhakikisha wizara yenye kushughulikia sekta hiyo anapewa mtu wao.

“Wawindaji hao kwa muda sasa wamekuwa wakifanya juhudi hizo na lengo mojawapo ni kuweka mtu wao na kisha kubadilisha regulations (kanuni) mpya za vitalu na uwindaji ambazo zimeandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu zikitaka mtu kutomiliki vitalu vya uwindaji zaidi ya viwili, kwa sasa mtu mmoja anamiliki vitalu zaidi ya hivyo hata 10.

“Jiulize hadi sasa kwa nini regulations hizo hazitangazwi rasmi licha ya kukamilika…kuna nini? Halafu nilichoandika kwenye gazeti ni maoni yangu, si msimamo wa gazeti. Kosa langu nini?

Hata hivyo, kwa kuzingatia kanuni za uendeshaji magazeti, mhariri ndiye anayepitisha au kukataa chochote kinachochapishwa gazetini. Gazeti hili lilimuuliza Matinyi kama kazi yake iliidhinishwa na mhariri na kama baada ya kuchapishwa kwa makala yake aliitwa na mhariri wake kutoa vielelezo kabla ya mhariri kuandika ‘kunradhi’ kwa Meghji.

Alijibu akisema taratibu zote zilifuatwa na kwamba alishangaa kuona siku iliyofuata ameandikwa kwenye gazeti akihukumiwa ametoa tuhuma za uongo bila kuulizwa na mhariri wake kama anavyo vielelezo au la.

“Hapa kinachofanyika ni unafiki tu, hakuna chochote chenye maslahi kwa nchi. Msimamo wangu ni ule ule, kwamba hata kama Rais Kikwete atamteua Meghji kuwa waziri siamini kama anastahili nafasi hiyo,” alisema.

Naye mhariri wa habari wa gazeti la kila siku la Mtanzania, Manyerere Jackton alitoa maoni yake bila ufafanuzi zaidi akisema; “Hatutakuwa huru mpaka siku moja tutakapoamua kuwa huru.”

Kwa upande wake, mhariri Deodatus Balile alisema hapakuwa na shinikizo lolote kutoka kwa yeyote katika kufikia uamuzi wa kuomba radhi kwa Meghji bali ni uzingatiaji wa uandishi wa habari na utekelezaji wa majukumu ya mhariri.

Source: Raiamwema.
 
Masyaga hama kambi, uliyoko haiendani na uadilifu unaouonyesha

hakuna kitu hapo, mtanzania ndilo gazeti linaloongoza nchini kwa kushambulia watu tena kwa kuwapakazia mambo ya uongo.

huyo masyaga matinyi hajaanza jana kuandika mambo ya personalities, kuna siku alimshambulia dr.shein na mhariri wake hakumuomba radhi dr.shei. Baada ya dr.shein kuteuliwa kugombea urais zanzibar, mimi binafsi niliwasiliana nae nikamuuliza kwamba baada ya tuhuma zake zote kwa dr.shein lakini bado kateuliwa kugombea urais zanzibar, sasa unasemaje? alinijibu kwa ufupi tu kwamba, tumuunge mkono dr.shein.

kama masyaga akitaka kuhama kambi, basi itakayomfaa ni quality media group tuliyosikia kwamba inakuja hivi karibuni.
 
nimempigia simu nikampongeza. hata kama ana kambi lakini kutuepusha na fisadi mehgi katusaidia. kumbukeni unafiki wa meghji alipokuwa akimjibu slaa bingeni kuhusu tuhuma za epa, na jinsi yeyey binafsi alivyoshiriki
 
Asante masyaga wewe ni mwanamume la sivyo utajiri wetu wote ungehamia kwa mama mkwe na wanaomzunguka
 
My take:

Kama bila ya huyu mhariri kutoa habari hii, inawezekana huyu mama angekuwemo kwenye baraza la mawaziri na haya madudu yangefanyika!! BRAVO MATINYI!!
 
Gazeti la Mtanzania kwa mara nyingine limejipambanua haliko kwa maslahi ya watanzania bali kikundi kidogo cha mafisadi.
 
Back
Top Bottom