Dr. Hussein Mwinyi Must Resign/get fired for Gongo la Mboto armory Inferno

And the boss is smilling....as always...what if this was little Riz1...would he smile?

Tanzanian-president-Jakaya-Kikwete-visits.jpg
 
Ujue Kauli yake ile ya Mbagala inamfunga,, sasa tunachotaka sisi ni kuachia ngazi tu mtu gani hayuko makini na kile anacho kiongoza? watu wangapi mpaka sasa wamekufa kwasababu ya Uzembe?
 
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Husein Mwinyi, amesema endapo itabainika kuwa milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mbagala Kizuiani, jijini Dar es Salaam ilitokea kwa uzembe, atajiuzulu.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam, na wanasiasa kumtaka ajiuzulu kutokana na uzembe uliosababisha milipuko hiyo kutokea na kupoteza maisha ya wananchi zaidi ya 27 na zaidi ya 300 kujeruhiwa na wengine kadhaa kukosa makazi baada ya nyumba zaidi ya 700, kuharibika.

Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1, Waziri Mwinyi alisema, analazimika kuweka mambo wazi kuwa wizara yake inafanya uchunguzi wa kina na kutoa ushirikiano kwa kamati maalum iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete na baada ya kumaliza kazi yake, ikibainika kuwa ilitokana na uzembe ama wa yeye au wasaidizi wake, atajiuzulu.

'‘Watu wengi ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam wamekuwa wakinitaka nijiuzulu, lakini kuna uchunguzi unaendelea, ikibainika kama kweli kuna uzembe, nipo tayari kuachia ngazi," alisema Dk. Mwinyi.

Aliongeza kuwa, suala la kuwajibika halina mjadala kama kuna sababu za msingi na inaonyesha kuwa kuna uzembe, ila si kujiuzulu tu kwa sababu watu wamesema.

Mwinyi ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, ametoa masimamo huo ikiwa ni siku chache zimepita tangu Chama cha NCCR-Mageuzi kumtaka kujiuzulu kutokana na kile kilichodaiwa kuwa, ilitokana na uzembe wa ukaguzi wa silaha katika ghala hilo na kusababisha maafa hayo.

Sababu nyingine iliyotolewa na chama hicho cha upinzani ni kuwa, serikali ilikaa kimya kuona wakazi wa Mbagala wakijenga na kukaribia eneo hilo la jeshi, jambo lililomsukuma Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Sam Ruhuza kumtaka kiongozi huyo na wasaidizi wake kuchukua hatua ya kujiuzulu.

Endapo waziri huyo atajiuzulu, atakuwa amefuata nyayo za baba yake, Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alijiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani kutokana na vifo vya mahabusu vilivyotokea katika gereza moja mkoani Shinyanga.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wiliam Lukuvi, jana alisema serikali imepeleka jopo la madakatari kutoka hospitali zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hospitali maalumu ya kuchunguza viungo (CBRT), ili kuwafanyia uchunguzi wa viungo wanafunzi wa shule za msingi za Mbagala ambao wanadaiwa kuathirika na milipuko hiyo.

Zoezi la kupima wanafuzni hao lilianzia katika shule za Mbagala Kuu, na Maendeleo na sasa linaendelea katika shule nyingine za msingi kwa wanafunzi na walimu kupimwa afya zao.

"Kuanzia kesho (leo), madaktari wa macho, masikio na viungo kutoka hospitali zote za Dar es Salaam, watakwenda katika eneo hilo kuangalia afya za wanafunzi wa shule zote, waliopoteza viungo watapatiwa vingine, miwani itatolewa bure na watakaopelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi watafanyiwa bure," alisema Lukuvi.

Aliongeza kuwa, jana serikali ilipeleka wataalamu wa saikolojia ambao walitambua kuwa watoto wengi wameathirika kisaikolojia, ndiyo maana wanashindwa kutulia na kukaa madarasani kwani wanahofu ya kujirudia kwa milipuko hiyo.

Alisema, Shirika la kuhudumia watoto la Save the Children, nalo limetoa msaada mkubwa kwa watoto wadogo kutokana na kuwapatia vifaa vya michezo na wanasesere ambavyo vinawasaidia kuchezea na kusahau milipuko hiyo.

Akizungumzia suala la tathimini na kufidia waathirika hao linaloendelea hivi sasa, alisema hofu kubwa ya wananchi wa Mbagala ni kuhusu jinsi watakavyofidiwa.

Lukuvi ambaye alisisitiza kuwa zoezi la utathimini linaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya haki, alisema linatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu na kwamba idadi ya nyumba zilizotarajiwa kufanyiwa tathimini imeongezeka kutoka 7,878 na kufikia 8,306.
"Ninaamini kuwa zoezi hilo litamalizika ndani ya muda tulioupanga. Kwa sasa nyumba 7,832 zimekwishapitiwa na tathimini hii inaendeshwa kwa haki, hivyo hata wapangaji wasiwe na wasiwasi," alisisitiza Lukuvi.

Aliongeza kuwa, idadi ya kaya zinazopatiwa msaada hadi sasa imeongezeka kutoka 3,750 lakini kutokana na kufuatilia hali ya waathirika hao na matatizo yao, walibaini kuwa idadi sahihi inayotakiwa kusaidiwa ni 4,873.

Alipoulizwa gharama ambazo serikali itatumia kuwalipa fidia wakazi hao, alisema mara baada ya zoezi hilo kukamilika, wataweza kulizungumzia hilo na iwapo watajengewa nyumba au kupewa fedha taslimu na kuhamishwa katika eneo hilo.

"Hayo tumeiachia task force (kikosi kazi), mara wakimaliza kuendesha zoezi hilo mwezi huu, nitawaiteni nyote na kuwaambia maamuzi yaliyochukuliwa, kwa sasa siwezi kulizungumzia hilo," alisema Lukuvi.

Katika hatua nyingine, Lukuvi amewataka wananchi kutokubali kutumika kisiasa, hasa katika matatizo hayo ya mlipuko wa mabomu.

Lukuvi ambaye jana alitembelea Manispaa ya Temeke kwa ajili ya kujitambulisha rasmi, alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja imepita tangu baadhi ya kikundi cha watu kutaka kuandamana wakimtaka kiongozi huyo kujiuzulu baada ya moja ya gazeti la kila siku kuandika kuwa aliwataka wakazi hao wazoee hali kama wenzao wa Kipawa.

Lukuvi akiwa ofisini kwake jana, alikanusha taarifa hiyo kwa kusema kuwa alichokisema ni kuwa, hajui siku gani zoezi la kuliweka salama eneo hilo litakamilika, hivyo wananchi wa Mbagala kwa kipindi hiki cha utafutaji wa mabomu yaliyotawanyika mara baada ya mlipuko huo, wakati tathimini ikiendelea, wanapaswa kuwa wavumilivu.

Hata hivyo, alisema maandamano yanayodaiwa kufanywa yanatokana na zoezi hilo kuingiliwa na suala zima la siasa, hivyo aliwataka watu kutokubali kuliingiza kisiasa.

"Watu wasiliingize suala hilo na siasa, yote yanayotokea sasa yanatokana na zoezi hili kuingiliwa na siasa," alisema Lukuvi. Lukuvi alikiri kuwa eneo la Temeke lina ushindani mkubwa wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kile cha Wananchi (CUF) kwani kati ya viti tisa vya uenyekiti wa serikali za mitaa, saba vinashikiliwa na CUF, huku viwili vikishikiliwa na CCM na kuongeza kuwa isiwe kigezo cha kuingizwa katika utaratibu huo.



Source Tanzania Daima.
 
WANANCHI HATUKO SALAMA TENA NA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA
KUONGEZEKA HIVYO SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake.

Jukumu la msingi halijazingatiwa; wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

Hatutaki tena tume kwa hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????
 
Kitendo cha watanzania kukaa kimya huku hawa viongozi wazembe wanao iaribu nchi kwa kuacha Vifo mbalimbali kutokea kiholeaholela si cha kiuungwana, hii inaonesha kuwa Watanzania pia wanakisuport kitedo hiki kwanini tusiandamani ili hawa watu waresign bwana
 
Hawawezi kujiuzulu hawa kwa sababu zifuatazo. 1.Uongozi kwa Tanzania(CCM) ni ajira, na si utumishi kwa wananchi. 2. Wameingia madarakani kwa kuteuliwa kwa upendeleo na kujuana. 3. Mkuu wao aliyewateua alipewa ushindi na Tume ya uchaguzi kwa hiyo ni rais wa tume. 4.Wanatumia nguvu za giza na kafara kupata uongozi. Watanzania tutarajie mengi kutoka serikali hii ya kidhalimu. Ila YANA MWISHO.
 
sio nyie wa gongo la mboto ni nchi nzima mkuu!

Husein Mwinyi kama hutaki kuresign kwa Amani tutakufanyia alichofanyiwa Raisi wa Misri, sasa ili usipate aibu hiyo we jiuzuru maapeemaaaaa, habari za nguvu za giza hapa hakuna nafasi tena, maana mumezoea nyinyi wa CCM:mullet::spider:
 
Husein Mwinyi kama hutaki kuresign kwa Amani tutakufanyia alichofanyiwa Raisi wa Misri, sasa ili usipate aibu hiyo we jiuzuru maapeemaaaaa, habari za nguvu za giza hapa hakuna nafasi tena, maana mumezoea nyinyi wa CCM:mullet::spider:

Hawawezi kujiuzulu hawa kwa sababu zifuatazo. 1.Uongozi kwa Tanzania(CCM) ni ajira, na si utumishi kwa wananchi. 2. Wameingia madarakani kwa kuteuliwa kwa upendeleo na kujuana. 3. Mkuu wao aliyewateua alipewa ushindi na Tume ya uchaguzi kwa hiyo ni rais wa tume. 4.Wanatumia nguvu za giza na kafara kupata uongozi. Watanzania tutarajie mengi kutoka serikali hii ya kidhalimu. Ila YANA MWISHO.
 
Back
Top Bottom