Dr Hosea aliwezaje kuwafunga Mramba na Yona?!!

Nimetafakari sana jambo hili baada ya kupitia taarifa za yule mkurya wa Musoma aliyefisadi mradi wa maji Bunda pamoja na Musoma hotel. Nikasikia kuwa eti huyio fisadi ni mfadhili wa CCM huko " kijijini" Musoma ndio maana anaogopwa hata na vyombo muhimu. Najiuliza ilikuwaje mkurugenzi wa zamani wa Takukuru alisimamia kesi ya Mramba na Yona kwa ufanisi tena bila woga hadi jamaa wakatupwa gerezani?.....Haiwezekani kukopa mikakati na ujasiri wake hata kama alikuwa na mapungufu mengine? Naomba niishie hapo!
Kwa taarifa yako mahuza ni moto wa kuotea mbali
Hata hiyo iliyofanyika ni geresha tu kumnyang'anya hiyo musoma hotel
Mahuza ndie aliemchomoa bwana slow slow kwenye ukuu wa wilaya,,,kisa ni mgodi wa CATA MINE kule kiabakari

Weka mbali na watoto
 
Upunguani ndo huu sasa, kosa la kuchukua hela za umma pamoja na kifungo unatakiwa ukitoka ulipe, ila kutumia madaraka kwa kutoa msamaha kinyume na sheria means ulikosea kutoa msamaha ila hukula hiyo pesa,rudi skuli
Mkulu mi' nimekuelewa vzr zaidi na usipende kila mtu akuelewe maana kuna watu huku dah....!! Sijui ndo ujuaji au..?
 
Waswahili husema mambo usiojua ni kama usiku wa Giza.Jiulize jamaa wakati wa Zabuni ya kununua Hotel kitu gani kiliipelekea serikali kuuza Hotel?kwa kifupi ukiwa na fedha usipende kununua Mali za serikali,Nunua au Jenga chako.Miradi wa Maji nao Jiulize kwa nini imekuwa hivyo cha Msingi inahitajika Repoti na Utetezi wake ili wanajf wafanye analysis
Ukiwa MKANDARASI, USILOGWE KUPEWA TENDA ZA MIRADI YA MAJI.
Miradi ya Maji ni kikaango cha Makandarasi na kitovu cha mafisadi wa Wizarani na Halmashauri.
Mzigo wote unatupwa kwa Mkandarasi.
 
Back
Top Bottom