Dkt. Hastings Kamuzu Banda: Haya ni kweli kumhusu?

Ninachojua kuhasi ni kutoa ile korodanu ya uzazi ili kusiwe na kuzaliana lakini tendo la kujaamiiana hubaki palepale, sasa kama walimuhasi, hawakuwa makini pengine jamaa alijilia. Kwa mantiki hii, hii I stori tu.
 
mkuu usiseme za uongo, mimi nilizisikia kutoka kwa mwalimu wangu tena anaheshimika.

Ulizisikia kutoka kwa Mwalimu wako tena anaheshimika.Duuuu huyom mwalimu wako anaheshimika kwa uwongo na muongo mkubwa sana.Naninafikii kuwa hata wewe na muongo sana kwani unaendeleza uongo wa mwalimu wako.
 
Wadau kama mnavyojua leo ndio maadhimsho ya miaka 60 tangu Elizabeth II atawazwe kua malkia wa Uingereza.

Sasa kuna kitu kimoja nimekikumbuka leo na naomba kwa mwenye kumbukumbu atujuze.

Nilipokua mdogo nilikua nasikia eti yule Ex Rais wa malawi hayati Hasting Kamuzu Banda alikua ni daktari binafsi wa Malkia. Na kazi yake kubwa ilikua ni kutibu sehemu ya uzazi (nyeti) ya huyo Queen.

Sasa Waingereza kwa kuhofia Dk Banda asije kula tunda, ikabidi wampe sharti la kuhasiwa. Na yeye akatoa sharti kwamba sawa ila apewe Urais wa Malawi. Wakakubaliana and the rest is history.

Jee wenzangu habari hii ni ya kweli?

Hebu ipitie historia yake hapa (Hastings Banda - Wikipedia, the free encyclopedia) halafu tuendelee na mjadala.
 
Ulizisikia kutoka kwa Mwalimu wako tena anaheshimika.Duuuu huyom mwalimu wako anaheshimika kwa uwongo na muongo mkubwa sana.Naninafikii kuwa hata wewe na muongo sana kwani unaendeleza uongo wa mwalimu wako.

What you know about my teacher? You know nothing about him. So please do not impugne his honour.
 
Habari hizi zinaweza kuwa ni za kutungwa ili zilikuwepo. Watungaji sio sisi.

Nilichosikia mimi ni hivyo hivyo kuwa Hastings alikuwa the best gyno na ndie alikuwa gyno wa qeen.

Kabla haja muatend alikuwa akipigwa nusu kaputi ili kutunza usalama wa malkia. Sasa kuna siku kiwango kilizidi hivyo kumfanya jamaa akawa importent.

Ili kumpooza ndipo Malkia akampa zawadi koloni lake la malawi. Ndipo akatafuta jina la Kiafrika la Kamuzu Banda! na kujiita rais wa maisha.

Hakuzaliwa Malawi, hakuwa Mmalawi, hakuzungumza lugha yoyote ya kiasili ya Malawi zaidi ya Kiingereza, alikuwa na mke zuga ila hakuwa na mtoto. Hakuna kumbukumbu zozote za kihistoria kuonyesha Hasting alizaliwa wapi na asili yake ni wapi bali alikuwa mtoto wa familia ya waliokuwa watumwa huru.

Mimi niliwahi kutembelea kaburi lake liko nje kidogo ya jiji la Lilongwe!.

Ukiondoa Jo Burg na Cape Town, Lilongwe ndio mji uliojengeka kwa modern planning kuliko mji mwingine wiwote barani Africa South of Equator,
ooh boooy....ningeshangaa story yote hiyo iishe bila....
 
Mkuu hamna lolote hayo ni mazungumzo baada ya habari, tulisikia mengi sana kama Nduli, Kaburu na yeye kuwa punga hii ni kutikana na kutokuelewana kiitikadi na Saint Nyerere
Haiyumkiniki kwa Malkia kutibiwa na dokta mmoja hata huyo raisi wetu wa bongo hatibiwi na dokta mmoja

Ulikuwa ni uwongo mkubwa sana. Ni stori za kwenye bao na kahawa
 
si kweli. Msomeni Kanyama Chiume ameelezea sana siasa za ukombozi wa Malawi. Hakuna kitu kama hiyo.
 
ukiacha story hiyo pia kulikuwa na stori kwamba banda alifanyiwa opereshen ya kubadilishwa ubongo. kwamba ubongo wake ulishakufa akawekewa ubongo wa mtoto aili asizeeke. ushushi tuu.
 
Jamani hizi ni propaganda za nchi yetu zidi ya yule Dikteta! Kwani hamjui Banda alikuwa haelewani na nchi yetu
 
Dr Hastings Kamuzu Banda raisi wa kwanza wa Malawi alizaliwa kati ya March-April 1898 na alifariki 25/11/1997 akiwa na umri wa miaka 99. Alitawala Malawi kutoka 1961 mapaka 1994, kabla ya hapo Malawi ilikuwa chini ya uangalizi wa Mwingereza ikijulikana kama British Nyasaland.

Banda alizaliwa karibu na Kasungu Malawi wakati huo ikijulikana kama British Central Africa. Wazazi wake ni Mhonongo Banda na Akupingamnyama Phiri. Hakuna anaejua tarehe sahihi ya kuzaliwa kwakua hakukua na desturi ya kuweka kumbukumbu ya vizazi na vifo miaka hiyo.

Jina la Kamuzu maana yake ni mzizi mdogo kwakua mama yake Banda alipata ujauzito baada ya kutumia mzizi mdogo aliopewa na mganga baada ya kuwa na matatizo ya uzazi kwa muda mrefu. Jina la Banda maana yake ni ki nyumba kidogo. Hastings ni jina alilopewa baada ya ubatizo lilitoka kwa mmisionary wa kanisa la Scotland karibu na kijiji chao.

Kati ya mwaka 1915-16 Banda aliondoka kijijini kwao kwa miguu akiwa na mjomba wake Hanock Msokera Phiri ambae alikuwa mwalimu katika shule ya mission iliyoitwa Livingsotne Wakieleke Hartley ambayo sasa hivi inaitwa Chegutu Zimbambwe. Mwaka 1917 alitembea kwa miguu tena kuelekea Johannesurg Afrika ya Kusini. Alifanya kazi Wituatersrand Deep Mine katika Transvaal Reef kwa miaka mingi kabla ya kukutana na Askofu W.T. Vernon wa kanisa la Methodist alieshangazwa na uwezo wa akili aliokuwa nao. Aliamua kumlipia ada ya masomo yake nchini Marekani ikiwa Banda atajigharamia usafiri wa kufika huko.
220px-Dr_HK_Banda%2C_first_president_of_Malawi.jpg


Kyalow

Banda alikwenda New York kuchukua masomo ya juu katika chuo cha watu wenye asili ya Afrika (African American) kiitwacho Wiberforce College ambacho sasa hivi kinajulikana kama Central State University Ohio. Alimaliza mwaka 1928 na msaada wa pesa kutoka kwa Askofu ulikomea hapo. Banda alianza kuishi kwa kutoa mada kwa muongozo wa mwanataaluma kutoka Ghana alieitwa Kweyir Aggrey ambae walikutana South Afrika.

Siku moja wakati anatoa mada katika club ya Kwanis Banda alikutana na Dr Herald ambae alimsaidia katika kujiunga na chuo cha udaktari Indiana University akiwa pale aliishi kwa Mrs Culmer kama mpangaji. Akiwa Bloominton aliandika insha kuhusu kijiji chake cha Chewa. Insha hii ilimvutia sana mwanataaluma wa lugha Mark Hanna watkin na ilipelekea Banda kufahamishwa kwa Edward Sapir mtaalamu wa masomo ya ubinadamu
(anthropologist) katika chuo kikuu cha Chicago ambako alihamia baadae.

maxresdefault.jpg


Katika kipindi chote hiki alishirikiana na Mark Watkin katika habari za Chewa na aliishi na Mmarekani mweusi Corina Saunders kama mpangaji mwenzake. Alipata shahada ya historia mwaka 1931. Wakati wote huu msaada wa pesa aliupokea kutoka kwa Mrs Smith ambae mume wake Douglas Smith alipata utajiri kwa kutengeneza dawa ya meno aina ya Pepsodent pia alikuwa na hisa katika kampuni ya kodak. Wengine waliomsaidia kwa pesa alikuwa Bwana B. Stephonson wa Delta Electronic Company na misaada hii ilimuezesha kusomea udaktari Meharry Medical College Tennessee na kuhitimu mwaka 1937.

Maisha ya Banda nchini Uingereza.
Ili kufanya kazi kama daktari nchini Uingereza ilibidi Banda kupata shahada ya pili ya udaktari, alijiunga na University of Edinburgh na aliweza kupata shahada tatu kwa wakati mmojoa. LRCP(Edin), LRCS(Edin), LRFPS(Glas) Scottish Triple Conjoint, awarded since 1886,[1] (Licence of the Royal College of Physicians of Edinburgh, Licence of the Royal College of Surgeons of Edinburgh, Licence of the Royal College of Physicians and Surgeons of Glasgow).
Masomo haya yalidhaminiwa kwa £300 kwa mwaka kutoka serikali ya Nyasaland kwa makubaliano atarejea nyumbani kama daktari baada ya kumaliza masomo, pia kulikua na Mscotish aitwae Kirk alimpa ufadhili na inasemekana ufadhili wa Mrs Smith bado uliendele na wadhamini wote watatu hawakujuana.

Alipojiunga na chuo cha magonjwa ya kitropik kilichoko mjini Liverpool serikali ya Nyasaland ilisitisha udhamini. Hiki kilikuwa kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia na kwa mujibu wa sheria madaktari wote waliandikishwa kuwa madaktari wa jeshi, Dr Banda alikataa hili na ililazimika kuacha masomo hapa. Alikua pia ni mzee wa kanisa la Church of Scotland.

Mwaka 1941 mpaka 1945 Dr Banda alifanya kazi kama daktari katika mji wa North Shields karibu na Newcastle upo Tyene. Alikuwa mpangaji wa Mrs Amy Walton sehemu iitwayo Alam Place. Dr aliendelea kumpelekea Mrs Walton Christmas card mpaka mauti yalipomkuta mwaka 1960. Mwaka 1944 alikutana na Merene French ambae alikua mka mwana wa mmoja wa wagonjwa wake, wawili hawa walianza mahusiano.

images


Mnamo mwaka 1946 kwa maombi ya Chifu Mwase Kasungu, ambae walikutana Uingereza mwaka 1939 na wanasiasa weingine ambao walishaanzisha vuguvugu la kisiasa nchini Malawi Dr Banda alihudhuria Nyasaland African Congress ambayo ilifanyika Manchester, huu ulikua mkutano wa tano wa Pan African Congress. Kutokea hapo alianza kuwa na ari na moyo wa kupigania nchi aliyozaliwa. Aliisaidia Congress kwa mawazo na pesa pia alifanya lobbing akisaidiwa na Waingereza kama mwakilishi wa Congress.

Banda alipinga sana juhudi za Bwana Roy Welensky, aliyekuwa mwanasiasa wa Rhodesia ya Kaskazini, kuunda umoja wa Rhodesia ya kusini na kaskazini pamoja na Nyasaland, jambo hili Dr. Banda aliona litazidi kumkandamiza haki za watu weusi wa sehemu hizi na wazi kabisa aliliita wazo hili kuwa ni la kijinga hata hivyo umoja huo uliundwa mwaka 1953.
Kulikuwa na fununu na shauku kuwa anarudi Nyasaland mwaka 1951, lakini alikwenda Ghana badala yake. Alikwenda kule baada ya kashfa iliyomhusu mhudumu wa mapokezi katika ofisi yake ya London Herlesden, Merene French kulikuwa na fununu kuwa alikua na ujauzito wa Dr. Banda, hakuna aliiwahi kuthibitisha hili. Banda aliandikwa kama sababu ya ndoa ya Bwana na Bibi French kuvunjika kwenye makaratasi ya talaka Bwana French aliandika anamwacha mke wake kwa kukosa uaminifu kwenye ndoa. Baada ya talaka Bibi French aliandamana na Dr Banda mpaka Ghana. Kufika Ghana Dr. alimueleza Bibi French kuwa hakutaka kingine tena zaidi kati yao, mapenzi yalikwisha. Bibi French alirudi London na mauti yalimkuta mwaka 1976.
banda-hastings-kamuzu-ap--258x258.jpg

.
Viongozi wa juu wa Congress akiwemo Henry Chipembere, Kanyama Chiume, Dunduzu Chisiza na T.D.T Banda (hawakua na undugu na Dr.) walimuomba arudi Nyasaland kuchukua uongozi wa chama. Banda akiwa Bandari ya Liverpool ambako alikua anajiandaa kurudi Ghana. Alikubali kurudi aliomba muda kidogo ili kupanga mambo yake binafsi, inawezekana kusafisha jina lake baada ya kashfa ya Bibi French. Viongozi wale wa chama walirudi bila Dr. Banda lakin walijua atakuja hivi karibuni. Kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya polisi na Waafrika, kuna ndege ilitaka kutunguliwa ikidhaniwa ndiyo ilimbeba Dr Banda Chileka Airport. Hatimae Banda liingia Malawi July 6, 1958 baada ya kuwa nje ya nchi kwa miaka karibu 42. Mwezi August mwaka huo huko Ntaka Bay, alitangazwa kuwa kiongozi wa Congress Party.

76399-004-54009FAA.jpg





Alianza kuzunguka kupinga Central African Federation ambayo pili ilijulikana kana Federation of Rhodesia and Nyasaland, aliomba watu wawe wanachama wa chama chake. Kipindi hiki lugha ya Chichewa ilimpiga chini, ilibidi atafutiwe mkalimani. Kazi ya mkalimani ilifanywa na John Msonthi na baadae John Tembo, ambae alibaki kuwa mtu wa karibu na Dr Banda kwa miaka mingi ya utawala wake. Alipokelewa kwa shangwe kila alipokwenda kuongea na kutokana na mada zake, Wamalawi wengi walielewa madhara ya ukoloni na hawakuupenda

Mnamo February 1959, hali ilikua mbaya sana kiasi kwamba majeshi ya Rhodesia yalianza kuletwa kutuliza ghasia na nchi iliwekwa kwenye tahadhari. Tarehe 3 March Dr. Banda pamoja na mamia Waafrika wengine waliwekwa ndani kwa kile kilichoitwa Operation Sunrise. Alifungwa jela ya Gwelo ambayo sasa hivi inajulikana kama Gweru Rhodesia ya Kusini. Uongozi wa Malawi Congress Party uliendelea chini ya Orton Chirwa ambae ndiye kwana alitoka jela.

Uingereza pia ilishachoshwa na harakati za makoloni kudai uhuru. Banda alitoka kifungoni mwaka 1960 na mara tu baada ya hapo alialikwa London kwenda kuongelea mazungumzo ya uhuru. Uchaguzi ulifanyika August 1961, Dr. Banda alichaguliwa kama waziri wa ardhi, madini na serikali za mitaa. Alianza kufanya kazi za waziri mkuu wa Nyasaland tarehe 1 February 1963. Dr Banda na viongozi wa juu wa MCP waliunda baraza la mawaziri na mapema baada ya hapo kupanua elimu ya secondari, kusitisha mikataba ya kilimo ya wakoloni pia mahakama za jadi zilipewa nguvu kutatua matatizo ya ardhi, walifanya mabadiliko mengi ambayo yalipelekea waziri wa Afrika wa serikali ya Uingereza R. A. Butler kukubaliana na maongezi ya kumaliza Federation.

Ni Banda ndiye alitoa jina la Malawi kutoka Nyasaland, jina hilo aliliona kwenye ramani wa Wafaransa "Lake Maravi" katika ardhi ya Bororos, alivutiwa na matamshi Malawi zaidi. Miaka sita kamili baada ya Dr Banda kurudi nchini kwake Nyasaland ilipata uhuru na kuwa moja ya nchi za jumuia ya madola Malawi. Hii ilikuwa 06 July, 1964.

1964 Mgongano wa baraza la mawaziri.

Kabla hata ya mwezi mmoja baada ya uhuru, Malawi ilipata pigo la mgongano wa mawaziri, lawama zilimuendea Banda alilaumiwa kwa kutoa maamuzi kuhusu kila kitu na kuwa wengine nafasi ndogo yakutoa hoja zao. Mawaziri waliwakilisha hoja ya kudhibiti nguvu za rais. Banda alipogundua hili alifukuza mawaziri wanne, mawaziri wengine walijiuzuru wenyewe na kuondoka nchini.

Banda alichaguliwa kama raisi wa kwanza wa kidemokrasia nchini Malawa, na serikali iliunda mfumo wa kupiga kura huru kila baada ya miaka mitano. Dr Banda alikua mgombea pekee wa nafasi ya uraisi. Serikali mpya ilimpa Banda nguvu nyingi kisheria na chama cha MCP kiliidhinishwa kuwa chama pekee cha siasa nchini Malawi. Chama Cha Congress kilitoa tamko kuwa Dr Banda ndiye raisi wa Maisha nchini humo. 1971 Bunge liliidhinisha Banda kuwa raisi wa Maisha na jina lake rasmi kuwa His Excellency the Life President of the Republic of Malawi, Ngwazi Dr. Hastings Kamuzu Banda. Jina la Ngwazi maana yake simba mkubwa au chifu wa machifu wengine watasema mshindi.

Kwa wengi Dr. Banda hakuwa na tabia za Ki-Malawi, kuanzia mavazi yake ya suti ya vipande vitatu inayo match na handkerchief, alitembea na fimbo yenye manyoya kwa kufukuzia inzi. Hakuzungumza Chichewa kabisa, alihitaji mkalimani na John Msonthi alifanya shughuli hiyo. June 1966 University ya Massachusetts ilimtunukia heshima ya doctorate iliyoambatana na theencomium pediatrician kwa kuongoza taifa lake changa.

Banda_and_Youens_in_1964.jpg


Ndani ya Malawi, watu walibadili mwonekano wa mapenzi kwa rais wao kuwa uoga. Alijijengea picha ya upendo kwa watu wake kama vile mwalimu mkuu na wanafunzi wake, lakini ukweli wenyewe ilikuwa ni serikali yenye amri hata kwa ile heshika ya Kiafrika kuwa mkubwa aheshimiwe lakini hii ilizidi. Dr. Banda alianzisha uongozi wake mwenyewe na alisema wazi "Kila kinachotoka mdomoni mwangu ni sheria na ifuatwe".

Ingawaje katiba ya nchi ilionyesha utawala wa sheria, uhuru wa kuongea lakini hivi vitu vyote havi katika maisha ya kila siku ya Malawi havikuwepo. Malawi ilikua nchi ya kipolisis. Barua zilifunguliwa, simu zilisikilizwa hii ilifahamika baada ya watu kugundua ukiongea neno lolote kuhusu rais simu inakatika. Vyama vya upinzani havikuruhusiwa na Dr. Banda alihimiza kabisa wamueleze watu ambao hawakubaliani nae, watu hao walikamatwa kama Kanyama Chiume au waliuwawa kama Dick Matenje au Dr. Attati Mpakati.

Ajali nne za Mwanza.
Katika mwaka 1983, mawaziri watatu Dick Matenje, Twaibu Sangala, Aaron Gadama na Mbunge David Chiwanga walikufa kwa kile kilichobandikwa jina "ajali ya barabarani". Dr Banda aliitisha "mkutano wa ndani katika kujadili vyama vingi" ndani ya Malawi. Wakati wa kikao cha mawaziri, mawaziri watatu walisema wazi wanataka vyama vingi na hii Banda aliona ni tishio kwa raisi wa maisha.

Kwa hasira na kufunga kikao kwa kusema bunge litakutana tena. Mwisho wa mkutano ule kila mtu aliekuwa alivuliwa rasmi madaraka yake ya kisiasa. Wanaume wale watatu walizungushwa katika jengo la Bunge la Zomba kwa maswali zaidi. Chiwanga inasemekana waliteswa kwenye chuma cha nyuma na iliamriwa wanyamazishwe. Wanne waliingia kwenye Peugeot 604 ya Matenje na kuendeshwa mpaka Thambani wilaya ya Mwanza magharibi kwa Blantyre, huko ajali ilitokea, chanzo cha kuaminika kinasema ajali ilitokea baada ya gari yao kurudishwa wakati wanakimbilia Mozambique. Baadae iligundulika waliuwawa kwa kugongewa misumari ya hema na nyungo kichwani. Banda aliamrisha mazishi yao yafanyike usiku na masanduku yasifunguliwe.

Maisha ndani ya Malawi ya Banda.

Watu wote walitakiwa wawe wanachama wa MCP. Kadi ya chama lazima utembee nayo kila unapokwenda na uwe tayari kuitoa kila inapohitajika. Kadi ziliuzwa mara nyingi na Umoja wa Vijana wa Malawi. Vijana hawa waliuza kadi hata kwa watoto ambao hawajazaliwa.

Umoja wa vijana wa Malawi lilikua ni kundi la hatari sana kwa kifupi lilikuwa jeshi la chama. Lilitumika kutisha na kunyanyasa wananchi hadharani. Vijana hawa walibeba silaha, walipeleleza na kuchunguza kila kinachoendelea katika nchi na ndio walioaminiwa kumlinda rais. Hawa walisaidia sana kukuza imani ya uwoga kipindi chote cha utawala wa Dr. Banda.

Banda alipenda sana kuonekana mtu wa muhimu na kuheshimiwa (cult of personality). Kila jengo la biashara lilihitaji kuwa na picha ya rais ukutani wala sio bango la biashara au saa ya ukutani la picha ya rais tu. Kabla sinema au video yeyote haijaonyeshwa lazima kuwe na clip ya rais Banda anapungia wananchi na mwimbo wa taifa unapigwa. Kila rais Banda alipotembelea lazima kikundi cha wanawake wacheze ngoma wakiwa wamevaa vitenge vyenye picha ya rais. Vikundi hivi vya wanawake vilitakiwa kuwa uwanja wa ndege wakimsubiri. Makanisa yote lazima yapate kibali cha rais kabla ya kuanza shughuli na makanisa ya Jehovah's Witnessess hayakuruhusiwa kabisa Malawi.

Banda alivyochukia Ujamaa.
Wakati wa utawala wa Dr. Banda, Malawi ilikataa kabisa kuhihusisha na serikali zote zilizokua na mfumo wa ujamaa ingawa baadae aliruhusu Romania na Albania kufungua ofisi za ubalozi mwaka 1985. Banda alikuwa mmoja wa maraisi wachache waliounga mkongo Marekani kuishambulia Vietnam, na hii ilichochewa na chuki yake dhidi ya siasa za ujamaa.

Uhusiano na nchi nyingine za Afrika.
Wakati nchi nyingi za Kusini mwa Afrika ziliacha ushirikiano wa kibiashara na Afrika Kusini kwasababu ya siasa za ubaguzi wa rangi, Malawi ilikua nchi pekee iliendeleza ushirikiano na Afrika Kusini na hata kuwa na ofisi ya kibalozi na biashara, jambo hili liliwachukiza sana viongozi wengine wa Afrika. Banda alisema katika hotuba yake moja Bungeni " Hakuna ugaidi linalowatisha, kuliko kujitenga na Afrika ya Kusini, washawishini waelewe siasa za ubaguzi wa rangi hazina faida. Aliendelea zaidi Viongozi wa Afrika ni wanafiki wameshikilia kupigania umoja wa Afrika, uhuru wa Afrika wakati huo wakiimba mwimbo wa Pan Africanism nchi zao zinaungua.
The_National_Archives_UK_-_CO_1069-165-9.jpg
 
Back
Top Bottom