Dr.Hastings Kamuzu Banda: Haya ni kweli kumhusu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.Hastings Kamuzu Banda: Haya ni kweli kumhusu?

Discussion in 'International Forum' started by trachomatis, Nov 9, 2011.

 1. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Kwamba alikuwa daktari wa binadamu,na pili alipata kumtibia Malkia Elizabeth kwa kigezo kuwa ndiye Daktari mwenye kiwango cha juu kwa kipindi hicho,na kuongezea hapo kwa sharti kwamba ahasiwe?
   
 2. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Zaidi ya hapo ni kuwa aliahidiwa kulindwa siku zote za utawala wake. Ndiyo akajihesabia yeye ni Rais wa maisha.
   
 3. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni kweli kabisa alikuwa dakatari bingwa!
  Ila wasiwasi nilionao ni kama alikuwa hajiusishi na kukameruni masaburini ili kujiliwaza na upweke:photo:
   
 4. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hata mimi niliwahi kusikia hivyo.Kwahiyo kipindi hicho waingereza/wazungu hawakuwa na daktari mzuri kumzidi Kamuzu Banda,mpaka wakakubali malkia atibiwe na mtu mweusi?
   
 5. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Habari ni hii,

  Kwanza, hakuwahi kuwa daktari wa Malkia wa Uingereza japo alikuwa daktari mzuri sana huko Uningereza. Pili, uraisi wa maisha alipewa na waMalawi wenyewe mwaka 1970. Tatu, jamaa kumbe hakua hasi (dunye) hata kidogo, alikuwa anakula kisirisiri na hata kuzaa watoto...

  Mnamo mwaka 1951, wakati Hastings an-practice udaktari huko Uingereza alizaa na receptionist wake ambaye pia alikuwa ni mke wa rafiki yake (inaonekana alisababisha mpaka waka-divorce), huyo mama alikuwa anaitwa Mrs. Marene French, Kamuzu alikataa katakata mtoto na mama!

  Na hivi juzi juzi tena ameibuka jamaa anayedai kuwa ni mtoto wake, huyu jamaa alifanya DNA testing na ikaonekana kuwa ni kweli Hastings Kamuzu Banda ni mzazi wake lakini ndugu za banda ambao ndio wanamiliki utajiri aliouacha wamegoma kukubali...

  Huyu jamaa (mtoto wake) jina lake ni Jumani Johansson au Jim Jumani Immanuel Masauko Kamuzu Banda ana uraia wa Sweden anakoishi na baba wa kufikia lakini pia ana passport ya Malawi....
   
 6. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Asante sana. Ina maana Dr. Banda alisoma udaktari wa binadamu Uingereza,na ingawa kwa miaka hiyo alikuwa bora Afrika,hakuwahi kumtibu Malkia wala mafua,ama ushauri achilia mbali kumpa Panadol si ndiyo?
   
 7. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Nielimisheni pia kuhusu sababu ya hii notion kuenea kwamba alihasiwa.Ilikuwa ni kumtafutia umaarufu,au kuondoa mashaka kwa wanaomzunguka kutokana na masuala fulani ya kibinafsi?
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Great! ................sichesee JF; JF ni chiboko!
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Ni uvumi ulioenea sana hapa Tanzania..............niliwahi kumwuliza mmalawi mmoja akanicheka sana! Alikanusha vikali na kwa kuwa tulikuwa mimi na yeye tu sikujua kama anamtetea kwa maana ya uzawa ama ni ukweli !
   
 10. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kuna taarifa vilevile kuwa Kamuzu Banda aliyetoka Malawi miaka ile ya awali siye yule aliyerudi kuja kutawala Malawi wakati wa uhuru. Inaonekana waingereza walibwatapeli wa Malawi. Ushahidi wa hilo unatokana na kwamba Kamuzu hana ndugu wa kikweli
   
 11. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kumbuka kuwa Kamuzu alikaa nje ya Nyasaland kwa miaka arobaini na nane (48), alianza South Africa, then akaenda USA, then akaenda Uingereza, then akaenda Ghana, halafu akarudi Uingereza tena ndipo akarudi Nyasaland...


  Yeye binafsi hakua na nia ya kurudi Nyasaland lakini akina Chiume, Tembo na wengine ndio waliomshawishi arudi, tabu nyingine ni kuwa kipindi alipokubali kurudi wakoloni (waingereza) walikuwa wanamzuia asifanye hivyo kwa kuhofia kuwa ataenda chukua nchi...


  Na mwisho kitu kilichowafanya waNyasa wafikirie kuwa Kamuzi huyu si yule wamjuaye ni kuwa jamaa alikuwa ameshasahau lugha ya kwao (Kichewa) so kila alipokuwa anahutubia mikutano ilibidi atumie mkalimani, hali hiyo iliendelea mpaka umauti ulimpomfika...


  Wakati alipokuwa USA alitengeneza ada ya shule kwenye mashindano ya kuongea, kuwa guest speaker na pia kuaandika makala kwenye newsletters. Elimu yake ya kusomea darasani ilikuwa digrii moja ya filosofia na digrii nne (4) za udakatari wa binadamu pia alikuwa na digrii ya heshima ya udaktari wa filosofia (PhD.)

  Hebu msikie makali yake kidogo hapa chini:


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Nimeelimika vya kutosha. Habari ya kuhasiwa nadhani ni ya kutungwa hapa TZ
   
 13. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Nimeelimika vya kutosha. Habari ya kuhasiwa nadhani ni ya kutungwa hapa TZ
   
 14. s

  silent lion JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 537
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Wadau kama mnavyojua leo ndio maadhimsho ya miaka 60 tangu Elizabeth II atawazwe kua malkia wa Uingereza.

  Sasa kuna kitu kimoja nimekikumbuka leo na naomba kwa mwenye kumbukumbu atujuze.

  Nilipokua mdogo nilikua nasikia eti yule Ex Rais wa malawi hayati Hasting Kamuzu Banda alikua ni daktari binafsi wa Malkia. Na kazi yake kubwa ilikua ni kutibu sehemu ya uzazi (nyeti) ya huyo Queen.

  Sasa Waingereza kwa kuhofia Dk Banda asije kula tunda, ikabidi wampe sharti la kuhasiwa. Na yeye akatoa sharti kwamba sawa ila apewe Urais wa Malawi. Wakakubaliana and the rest is history.

  Jee wenzangu habari hii ni ya kweli?
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hii story nilishaisikia lakini ilikuwa tofauti kidogo.
  Inasemekana kuwa Malkia alikuwa ni mgonjwa na daktari pekee wa kumtibia alikuwa ni Banda.
  Ugonjwa ulikuwa sehemu 'mbaya' ndipo kwa kutomwamini daktari huyo mweusi wakapeana masharti ya kumwasi.
  Naona si kweli kwa sababu zingeweza kutumika njia nyingine za kumwepusha Banda kula tunda.
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  sijui nani huwa anazitunga.....
   
 17. ALF

  ALF Senior Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  je hayo mambo yalifanyika lini? Sababu banda ana mtoto nafikiri anaishi Afrika Kusini. Au alihasiwa baada ya kuwa na mtoto?.
   
 18. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  That is a MYTH
   
 19. s

  silent lion JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 537
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mkuu kumbuka Banda alizaliwa 1898 na elizabeth alitawazwa kua Malkia mwaka 1952 yaani Banda akiwa na miaka 54. So inawezekana ikawa kweli.
   
 20. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wangekuwa walimkorokochoa miaka hii, mbegu zingewekwa kwenye friji. Wait a minute, walimkorokochoa ili iweje, maana kuna mambo mawili hapa; mbegu na kisafirisha mbegu. Walilenga nini zaidi?:behindsofa:
   
Loading...