Dr.hamisi kigwangalla acha undumila kuwili,...!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.hamisi kigwangalla acha undumila kuwili,...!!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by THE DON KIBEDAI, Dec 15, 2011.

 1. T

  THE DON KIBEDAI Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  DR.HAMISI KIGWANGALLA ACHA KUCHEZA NA AKIRI ZETU WEWE,..HUU UNAOUFANYA NI UNDUMILA KUWILI NA UOGA WA KUOGOPA KUWAJIBIKA,....!!!! USIWE BENDERA FATA UPEPO,.. WEWE KAMA BADO WAHITAJI POSHO IONGEZEKE ENDELEA KUIDAI TUACHE TUNAOIPINGA,.....!!!!
  TOKA HUKO ULIKO UJE UTUAMBIE WEWE UMETUMIA VIKAO GANI KUTOA MISIMAMO TATA HII HAPA CHINI,...AMA HUKU MTANDAONI SI HADHARANI...??

  STATUS YA KIGWANGALLA HAPA FACEBOOK

  "Mhe. January Yusuph Makamba (MP, M-CC, MNEC) has the following platform ya kuongelea: Bunge, Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Sekretariet ya CCM, Kamati ya Uongozi ya Bunge...hivi ni haki na halali kwa yeye na nafasi yake kutoa kauli ya kupinga posho hadharani ilhali ana fursa zote hizi za kuzuia ama kurekebisha? Kama hazitaki hizo posho si angeweza tu kuacha kuzichukua, ama angeweza kushawishi chama na serikali kwamba hazifai na zitolewe ama zisiongezwe! Wenzangu mnaonaje hili! Hivi wana-CCM wenzangu tumerogwa ama?"

  MSIMAMO WAKE KATIKA BLOG YAKE,...www.kigwangalla's.blogspot.com

  Kufuatia kuwepo kwa mjadala mzito wa kitaifa kuhusu ongezeko la posho ya kikao (Sitting allowance) ya wabunge kama ilivyoongezwa siku za karibuni, ofisi ya Mbunge wa Nzega imelitafakari suala hili na kuona umuhimu wa kutoa taarifa kwa wananchi wa jimbo la Nzega na watanzania kwa ujumla kuhusiana na msimamo wa Mhe. Mbunge. Tamko hili linazingatia maswali mengi kutoka kwa wapiga kura wa jimbo la Nzega na baadhi ya watanzania waliotaka kujua nini msimamo wa Dr. Hamisi Kigwangalla, MB (Nzega, CCM) kuhusu posho, hususan ongezeko hili la kutoka 70,000 hadi 200,000.

  Mbunge wa Nzega ana msimamo ufuatao:

  Kwamba, posho ama ujira wa mwia, ni malipo halali ya kazi ya Mbunge na kwamba ongezeko lolote litakalofuata kanuni na taratibu za haki na usawa kwa watu wote litakuwa halali.

  Kwamba, Ongezeko hili kama lilivyotamkwa na Mhe. Spika Anna Makinda (MB), limekuja kutokana na ongezeko la ukali wa maisha katika mji wa Dodoma linaleta mashaka na utata mkubwa kuhusiana na uhalali wake, linaonesha usaliti wa wabunge kwa wananchi waliowachagua na linaiaibisha taasisi ya Bunge kama mtetezi wa wanyonge na mdhibiti na msimamizi mkuu wa serikali. Mbunge wa Nzega anaamini kwamba sababu hii inawakimbiza wabunge mbali zaidi na wananchi na kwamba ni kweli kuna mfumuko mkubwa wa bei lakini hauwagusi wabunge tu pekee yao, unamgusa kila mtanzania, na kama ofisi ya Rais inaona umuhimu wa kuboresha hali ya maisha ya wabunge, basi ingewapandishia mishahara yao, ingewaongezea mafuta ya gari kwa ajili ya kufanyia kazi zao, ingeboresha mfuko wa jimbo, ingeboresha ofisi zao n.k. Kwa hakika kabisa, kwa sababu zilizotolewa na Mhe. Spika, posho iliyopaswa kuongezwa siyo posho ya kikao bali ni posho ya kujikimu. Na hata kama Mhe. Spika alikuwa na nia ya kuongeza posho ya kikao, basi kwa vyovyote vile sababu isingekuwa hii ya ukali wa maisha mjini Dodoma, maana hauongezeki kwa wabunge peke yao tu!

  Kwamba, kwa kuwa sababu za kuongezwa kwa posho ya kikao haziendani na malengo ya uwepo wa posho hiyo, basi wabunge wote waungane mkono na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe, Mbunge wa Bumbuli Mhe. January Makamba na Mbunge wa Nzega Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Nzega) waikatae posho hii ili kuwatendea haki watanzania wanaohangaika kutafuta mkate wao wa kila siku. Kuna madaktari wanakesha usiku kucha na wanalipwa posho ya on call allowance ya TZS 10,000 tu, kumlipa Mbunge posho ya 200,000 haijengi mazingira ya usawa ya kuugawana umaskini wa nchi yetu.

  Kwamba, ili kupunguza visingizio vya wabunge kudai maslahi makubwa zaidi kwa kuwa wanaombwa sana amisaada na wapiga kura wao, ofisi ya Bunge ianzishe kitengo cha kutoa elimu kwa umma kuhusu kazi na majukumu ya Mbunge ili kuwaelimisha wananchi kwamba kusaidia matatizo binafsi siyo kazi yao na hivyo wasihukumiwe kwa kutokutoa misaada bali kwa kuisimamia serikali ipasavyo.

  Tamko hili limetolewa leo Tar 12/12/2011 na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB)

  :embarassed2:WABUNGE WA CCM WOTE NI MIZIGO KWA TAIFA,....... ..................................................TAFAKARI CHUKUA HATUA KALI:embarassed2:
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mi sielewi huyu Dr anataka nini haswaa !.
   
 3. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  nyinyi hamumujui Said Nassoro!!!(hamis andrea),hajapata kuwa kiongozi mzuri hata siku 1,kwanza kwa asili yeye ni mtu mnafiki!!!!!!
   
 4. Kinyengeli

  Kinyengeli JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ogopa sana mtu mnafiki kama Kigwangallah( Said Bagaile)
   
 5. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Nyabafu nimechoka kuwasiliza marofa hawa ngoja nimfuate Kibweka kama anajipya lolote sababu leo kapwaya sana kwenye lile jukwaa letu
   
 6. T

  THE DON KIBEDAI Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Dr. Kigwangala mweupe kichwani cjapata kuona,........
   
 7. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni Litakataka fulani.
   
 8. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hata mimi silewi.

  Lakini huwa sielewi na wewe huwa unataka nini haswa.
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Hii babari ipo humu tangu tarehe 08/ 12/ 2011.

  [​IMG] EMT

  8th December 2011 16:51
  #1 [​IMG]
  [​IMG] JF Senior Expert Member Array


  Join Date : 13th January 2010
  Posts : 3,832
  Rep Power : 32  [h=2][​IMG] Posho za wabunge: Kigwangala on January Makamba[/h] Hivi punde Mh. Hamis Kigwangala ameweka status yake Facebook juu ya Mh. January Makamba:

  "Mhe. January Yusuph Makamba (MP, M-CC, MNEC) has the following platform ya kuongelea: Bunge, Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Sekretariet ya CCM, Kamati ya Uongozi ya Bunge...hivi ni haki na halali kwa yeye na nafasi yake kutoa kauli ya kupinga posho hadharani ilhali ana fursa zote hizi za kuzuia ama kurekebisha? Kama hazitaki hizo posho si angeweza tu kuacha kuzichukua, ama angeweza kushawishi chama na serikali kwamba hazifai na zitolewe ama zisiongezwe! Wenzangu mnaonaje hili! Hivi wana-CCM wenzangu tumerogwa ama?"
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  niliwahi kusema kwamba jamaa ni malaya wa kisiasa
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Huyu ndiye yule wa Bashe...?? Halafu JK anajitayarisha kumchagua Waziri...anyway ngoja tuone
   
Loading...