Dr. Gharib Bado ni mwenyekiti wa baraza la chuo UDOM

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal bado anatambulika kama mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu cha dodoma (udom council chair). Licha ya Rais Kikwete kumteua Balozi Juma Mwapachu kuwa mwenyekiti mpaya wa baraza la chuo kikuu cha dodoma tangu tarehe 14 September 2011 na taarifa rasmi kutolewa na ofisi ya uhusiano ya chuo hicho kupitia tovuti ya chuo hicho tarehe 03/10/2011, Bado tovuti (website) ya chuo kikuu cha Dodoma inamtambua Dr. Bilal kama mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, ambapo kuna picha inayomtambulisha Dr. Bilal kama mwenyekiti wa baraza la chuo.

Najiuliza maswali kadhaa juu ya jambo hili,

1. Je chuo kikuu cha Dodoma hakina wataalamu wa IT (Information Technology) wanaoweza kufanyia marekebisho suala hilo kwenye tovuti ya chuo mpaka leo!!!!???? Au kama wapo hawajui majukumu yao?????

2. Je, inawezekana uteuzi huo wa Balozi Juma mwapachu hauanzi mara moja na hivyo kumlazimu kusubiri muda muafaka wa yeye kuanza majukumu yake pale Dr. Bilal atakapo maliza muda wake rasmi.

3. Je, ni kwamba uongozi wa chuo kikuu cha dodoma umesahau kwamba Rais Kikwete alishateua mtu mwingine kushikilia nafasi hiyo au hawana desturi ya kutembelea tovuti ya chuo chao????

Nawasilisha.
 
Kiongozi kwani ungeandika tu website haijabadilishwa kuna tatizo gani? Naona taarifa unazo na si za uongo lkn unashambulia website na wana ICT wa UDOM kwa kutaja jina la Makamu wa Rais ambaye ahusiki na mabadiliko hayo. Busara ni jambo jema sana katika maisha. Nawasilisha.
 
Kaka kama wewe ni msomaji mzuri wa magazeti hupaswi kuhoji juu ya hiyo heading niliyoandika. Jinsi inavyoonekana kwenye website ndivyo inavyoeleweka na watu wengi. Wewe utafahamu kwamba website haijabadilishwa lakini watu wengi wanaotembelea website ya UDOM wataelewa Dr. Bilal ndo mwenyekiti wa baraza la chuo, na ni kitu hicho ndocho nilichoeleza. Kumbuka website inatembelewa na watu wengi duniani kwa hiyo wanachokiona ndicho watakiamini. So kama wewe ni mmoja wa wana IT wa UDOM fanya hima kubadilisha picha hiyo na kuweka ya Juma mwapachu ili kuto wa mislead watu ambao hawana taarifa na uteuzi wa rais.

thanks.
 
Back
Top Bottom