Dr Festus Limbu (Magu MP)?

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Wakuu,

Ningependa kujua Dr Festus Limbu ameleta maendeleo gani pale Magu?au na yeye umefika muda kama Kimiti na Mzindakaya?
 
Duh huyu mkulu sijui alipotelea wapi?Mara ya mwisho kumsikia ni wakati akiwa naibu waziri wa Mkapa!!Hivi ana PhD ya nini vile?
 
Duh huyu mkulu sijui alipotelea wapi?Mara ya mwisho kumsikia ni wakati akiwa naibu waziri wa Mkapa!!Hivi ana PhD ya nini vile?

annamaria,

Unaonaje tukafanya mkakati wa kumtoa wapele tuweke "change we can believe in"
 
Sie wana Magu,tunasema inatosha mwaka huu asije tena,tumeshapata mbadala,kwaheri Festo Limbu.anzisha miradi hukohuko Dar.
 
Vijana nendeni Magu mkagombee Limbu keshachoka, Tangu enzi alivyokuwa NCCR-Mageuzi na baadae CCM keshachoka.Vijana jitoeni mhanga.
 
Wakuu,

Ningependa kujua Dr Festus Limbu ameleta maendeleo gani pale Magu?au na yeye umefika muda kama Kimiti na Mzindakaya?

Mkuu siamini kama unauliza swali hili JF. Sidhani kama kuna mbunge mwenye uwezo wa kuleta maendeleo kwenye jimbo lolote lile. Kwa kuwa wenye jukumu la kuleta maendeleo kwenye jimbo lolote ni wanajimbo wenyewe, sio mtu mmoja. Mchango wa mbunge ni kusaidiana na wanajimbo kupata channels za kujiendeleza.

Kama unaweza kusema ni mbunge gani ambaye ameleta maendeleo kwenye jimbo lake, mtaje, au kama unafahamu jimbo lolote ambalo limeendelea litaje.

Kama kuna jimbo lolote ambalo limepiga hatua kidogo kuliko mengine, ni kutokana na juhudi za wanajimbo (ikiwa ni pamojoa na mbunge kama ni mwanajimbo) na sio juhudi za mbunge pekee.

Pamoja na kuwa simfagilii Limbu (political mathematicians ambaye aliamua kuswitch vyama ili tu apate ubunge na uwaziri), lakini siwezi kuvutwa kwenye cheap politics za kumponda kwa kusema ameleta maendeleo gani, very possible alitoa mchango kwa taifa alippokuwa waziri kuliko kwa jimbo lake. Ingekuwa ni vizuri kama tungeanza kujiuliza wenyewe tumesaidia vipi majimbo yetu, kabla ya kuanza kuwanyooshea vidole wengine.
 
Kuna mbunge gani Tanzania aliyeleta maendeleo jimboni mwake?
Chief! naamini maendeleo hayaletwi na mbunge pekee bali wadau wote kwenye jimbo... kwa jinsi baadhi yetu tulivyo wavivu hata tungeimport wabunge bado tungechemsha...
 
Mkuu siamini kama unauliza swali hili JF. Sidhani kama kuna mbunge mwenye uwezo wa kuleta maendeleo kwenye jimbo lolote lile. Kwa kuwa wenye jukumu la kuleta maendeleo kwenye jimbo lolote ni wanajimbo wenyewe, sio mtu mmoja. Mchango wa mbunge ni kusaidiana na wanajimbo kupata channels za kujiendeleza.

Kwa maoni yangu hatutarajii Mbunge atoe fedha kutoka mfukoni kwake ili alete maendeleo kwenye jimbo. Wanajimbo wanahitaji mtu wa kuwahamasisha na kuwaonyesha njia ya maendeleo, kusimamia na kuratibu michango ya jamii, kuunganisha katika kutafuta misaada na kadhalika. Haya ni baadhi ya majukumu ya Mbunge.

Yeye kama Mbunge vile vile anao uwezo wa kujua fedha kiasi gani zimeletwa kwenye jimbo lake, na hivyo kuangalia jee ni kweli zimetumika kama zilivyopangwa au zimetumika kwa masafari ya Waheshimiwa Madiwani?

Kama hawezi kufanya hivyo haina faida kuwa na mbunge
 
Duh huyu mkulu sijui alipotelea wapi?Mara ya mwisho kumsikia ni wakati akiwa naibu waziri wa Mkapa!!Hivi ana PhD ya nini vile?

Limbu ana PhD ya mambo ya fedha (finance and financial management) na haina mawaa. Mkapa ktk teuzi zake alikuwa makini, na baraza lake la mawaziri halikuwa na PhD za ajabu ajabu
 
PH.D ya Festus Limbu ni ya uchumi tena ya uhakiki na wala sio ya kuchonga kama ya CHEGENI!!
 
Dr Limbu yupo amejitahid kwa kadiri ya uwezo wake kuweka mji wa magu kuwa na barabara zinazopitika kwa kipindi chote.bado wana Magu wanashida ya maji
 
Back
Top Bottom