Dr. Ferdinand Masau: Daktari mzalendo anayejuta kuwa mtanzania

Status
Not open for further replies.
1. Huwezi kuwa mzalendo halafu ukajuta kuwa Mtanzania. Sentensi hizo zinakinzana.

2. Kwenye mgogoro wa THI na NSSF, Dr. Masau ndio mwenye makosa. Pesa alizokuwa analipia pango zilikuwa zinatoka kwa wafadhili Ujerumani. Wafadhili hao walikataa kuendelea kutoa pesa baada ya Dr. Masau kutokutekeleza wajibu wake wa kupanga kwenye jengo linalokidhi viwango walivyokubaliana. Matokeo yake akakosa pesa zza kulipa pango. Ukishidhwa kulipa pango unatolewa kwenye jengo, its that simple.

3. NSSF siyo charity organisation. Wanahitaji lile jengo kwa ajili ya uwekezaji.

4. Dr. Masau asitafute wa kumlaumu kwa sababu tatizo kubwa ni kwamba alikuwa NAIVE na akawa anatuymia theory kuliko uhalisia. Sasa uhalisia anaujua, so atafute tena definition ya uwezo wake.

5. Kulikuwa na mkataba kuwa serikali imshaidie kuendesha hiyo hospitali tangu kipindi cha Anna Abdallah kama waziri wa afya, lakini Masau alikataa vipengele vinavyompunguzia nguvu za maamuzi. Sasa ana nguvu zote za kuamua anachotaka, asimlaumu mtu kwa sababu kwake yeye nguvu za maamuzi zilikuwa muhimu kuliko huduma kwa wagonjwa.
 
Serkali ya Tz full kuchnganyikiwa walimsupport babu wa Loliondo leo wanashindwa kumsupport Dr Masau!
Alafu ili suala wabunge wetu hawalioni?Bse sio kila mtu anaweza kwenda India acheni kuwanyenyekea hawa maponjoli wana kwao hao!
 
Habari ya THI inasikitisha lakini watanzani lazima wakati mwingine mkubali kuupokea ukweli. Wadau wengi mmelalamika kuhusu hatua za nssf bila kupata taarifa za mgogoro wenyewe. Napenda kwanza kudeclare kuwa mmoja wa mwanafamilia yangu amekuwa akifadika na matitabu ya THI lakini haina maana mtazamo wangu juu ya mgogoro huu utabadilishwa na manufaa hayo. Dr huyu amekaa muda mrefu sana bila kulipa chochote pale, deni limelimbikizwa na kuwa kubwa sana, inasemekana anadaiwa 6 bilion(sijapata evidence lakini ndo figure inayotajwa). Nssf walifungua kesi na cha kushangaza THI walikuwa wahaendi mahakamani, na ikafika kipindi mahakama ikatoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja (hapa wanasheria wanajua). Mbali ya hapo muda pia ukaendelea bila wao kuchukua hatua yoyote, nssf wakaenda tena mahamani kuomba kuenforce ile judgement na ndo hapo court broker akaenda kufunga milango na vyote vilivyomo ndani.
Sasa hoja zangu!
Je Dr. Masao alikuwa na haki ya kufanya biashara bure? Alikuwa anacharge fedha na alikuwa anatibu magonjwa yote tofauti na wengi wanavyodhani kuwa ni moyo tu. Kwanini hakuwa anaenda mahakani kujitetea japo kuomba unafuu? Mpaka court order inatoka alikuwa hajui chochote hadi wafanyakazi wanakuja asubuhi wanawakuta mabaunsa langoni, kwanini alijiweka mbali hivyo na uendeshaji wa mgogoro huu?

If it is true then he doesn't deserve any mercy
 
Wakuu naomba kutofautiana (bila dhihaka wala matusi) na wengi wenu mnaofikiria kuwa ameonea,siijui kwa undani hii ishu ila nina maswali machache ninayojiuliza
1. Mapato aliyokuwa anapata Dr Masau yalikuwa hayakidhi/hayatoshi gharama za uendeshaji ikiwemo Pango
2. Kama zilikuwa hazitoshi alishawahi kuomba msaada serikalini kupunguziwa/kuondolewa kodi ya Pango?
3. Kama zilikuwa hazitoshi alishawahi kuomba ufadhili wowote nje ya nchi wa kulipia pango? Kuendesha hiyo hospitali?
3. Kama zilikuwa hazitoshi kwanini hakuongeza gharama za kutibu ili hospitali ijiendeshe kwasababu kuendelea kutoza
gharama ndogo mwisho wake ni kushindwa kujiendesha na kufunga/kufungiwa hiyo hospitali na hivyo kushindwa kutoa
msaada aliokusudia kwa WaTZ?
4. Kwanini hakutafuta jengo lenye pango nafuu hata kama lipo mabwe Pande wagonjwa wangeenda tu cause obvious
bado ni karibu ukilinganisha na India
Kwa Mtazamo wangu Dr Masau pengine alikuwa na lengo zuri la kutusaidia Watanganyika lakini hakuwa na mpango mzuri au alichukulia poa kwa vile tu anatoa huduma nzuri akasahau hii ni nchi inayoendeshwa na Manyang'au
 
nilipokua form five na ile kombi yetu ya PCB,tulienda pale kupata motivation kidogo.....dah..jamaa alilalamika sana,yaan alikua akielezea challenge ambazo kiukweli zinauma....pole sana Dr.,ondoka bwana utaishia kuwa kama Ulimboka..
 
tusimamie ukweli! watanzania tumefika hapa tulipo kwa kupenda zaidi vya bure, kusaidiwa na huruma ya watu na wafadhili mbalimbali badala ya kutafuta kujitegemea . Hapa sidhani ni busara hata kidogo kuilaumu NSSF/serikali katika jambo hili, assume kama vituo vyote vya binafsi vinavyotoa huduma za afya kwa wananchi wamiliki wake wangeitaka serikali isaidie gharama zake za uendeshaji tena bila mkataba maalumu, kusingekuwa na haja ya serikali kuruhusu private sector. Namshauri Dr. Massau atafute jinsi ya kusimama mwenyewe kama kweli ana nia ya kutoa huduma ya afya, badala ya hii ya kufanya shughuli zake binafsi akitegemea huruma ya serikali tena bila mkataba wowote kwa kisingizio kuwa huduma yake ni muhimu sana hivyo ni lazima asaidiwe na serikali. Hata Babu wa Loliondo alianza mwenyewe kwanza na baadae serikali ikajitoa kumsaidia baada ya kuona jinsi alivyokuwa anakusanya watu. Na yy akusanye watu kwa huduma yake nzuri ataweza kujiendesha tu.
 
vipanga siku zote wanamapungufu yao na falsafa zao (huwa wako kwenye ulimwengu wao , ukimwambia habari ya mahakama hakuelewi kwani sometime wanasahau hata msosi), hivyo iliitajika wanasaikolojia wengine kutathimini huduma yake na kutoa majibu. ni mabilioni mangapi yanaliwa adharani na hakuna anayefikishwa hata police post.
 
moyo(1).jpg

RIP DR Masau
 
1. Huwezi kuwa mzalendo halafu ukajuta kuwa Mtanzania. Sentensi hizo zinakinzana.

2. Kwenye mgogoro wa THI na NSSF, Dr. Masau ndio mwenye makosa. Pesa alizokuwa analipia pango zilikuwa zinatoka kwa wafadhili Ujerumani. Wafadhili hao walikataa kuendelea kutoa pesa baada ya Dr. Masau kutokutekeleza wajibu wake wa kupanga kwenye jengo linalokidhi viwango walivyokubaliana. Matokeo yake akakosa pesa zza kulipa pango. Ukishidhwa kulipa pango unatolewa kwenye jengo, its that simple.

3. NSSF siyo charity organisation. Wanahitaji lile jengo kwa ajili ya uwekezaji.

4. Dr. Masau asitafute wa kumlaumu kwa sababu tatizo kubwa ni kwamba alikuwa NAIVE na akawa anatuymia theory kuliko uhalisia. Sasa uhalisia anaujua, so atafute tena definition ya uwezo wake.

5. Kulikuwa na mkataba kuwa serikali imshaidie kuendesha hiyo hospitali tangu kipindi cha Anna Abdallah kama waziri wa afya, lakini Masau alikataa vipengele vinavyompunguzia nguvu za maamuzi. Sasa ana nguvu zote za kuamua anachotaka, asimlaumu mtu kwa sababu kwake yeye nguvu za maamuzi zilikuwa muhimu kuliko huduma kwa wagonjwa.

ze marcopolo,
Unaipenda sn tanzania lakini sio mzalendo ni kwa luwa tu unafaidika na resources zilizopo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom