Dr. Ferdinand Masau: Daktari mzalendo anayejuta kuwa mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Ferdinand Masau: Daktari mzalendo anayejuta kuwa mtanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sikiolakufa, Jul 6, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa mlio Dar es Salaam Hospitali pekee binafsi ya magonjwa ya moyo Tanzania Heart Institute mnaijua. Leo hii nimesikitishwa sana na hatua ya serikali kum frustrate Dr. masau kupitia shirika dhalimu la NSSF kuifunga hospitali hii na kupiga mnada vifaa vyote kisa mgogoro wa kodi... huyu bwana ana uwezo mkubwa na anatambulika dunia nzima kama ni one of the best heart surgions angekuwa na uwezo kuzamia huko ughaibuni kufanya shughuli zake. lakini kutokana na mapenzi na nchi yake aliamua kuanzisha taasisi ili kusaidia wagonjwa maskini ambao kwa namna yoyote ile hawawezi ku afford operation za moyo ambazo gharama zake huenda mpaka milioni kumi na zaidi... TANZANIA IS A TYPICAL DISFUNCTIONAL BANANA REPUBLIC...TUTAENDELEA KUWA MEDIOCRE TU
   
 2. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Kitu kinachogomba hapa ni ubinafsi..kwa ajili hakuna kiongozi maskini, basi wana uhakika wa kutibiwa india,,,so they got nothing to do with that man(masao)
   
 3. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Vichwa vyetu bado vinawazia kwenda Indai..sasa ukijenga hapa trip za India zitaisha.
   
 4. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hii habari imenisikitisha sana, kweli tuna serikali ya ajabu &dhaifu
   
 5. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 849
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  lakini haya matibabu ikumbukwe hafanyi bure ni biashara na shirika la nyumba linafanya biashara pia, kwahiyo kulipa kodi ya pango ni sahihi kabisa. Tatizo la huyu daktari anataka atengeneze faida kubwa bila gharama. Kama kuna nyumba anayoweza kufanya shughuli zake bure popote pale duniani ruksa aende.
   
 6. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli THI inadaiwa na NSSF kodi ya pango na hakuwahi kupeleka michango ya wafanyakazi wake hukohuko NSSF?
  Naomba mnijuze Jamani
   
 7. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nasubiria siku nitakayoenda dai hela zangu nssf ntaua mtu
   
 8. K

  KINYEKINYE Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  serikali ina uwezo wa kuingilia kati suala hili dr masau akaendelea na kazi ya kuwatibu walalahoi kwa sababu nssf ni yake. kusema kwamba masau anafanya biashara na nssf inafanya biashara si kigezo cha kumfilisi kwani uamuzi wake wa kuwekeza bongo ilikuwa nafuu kwa hiyo hiyoo serikali. da! pole dr masau.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Daaah....takribani miaka minne iliyopita kuna moto uliwaka hapa, sitausahau!!
   
 10. H

  Haika JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mimi ilinisikitisha sana kipindi kile anafungiwa, alihangaika sana nadhani imepita miaka kadhaa, ndio sababu halipi pango. Hiyo ilikuwa hadithi ya zamani, nadhani imo humu JF.
  Ila serikali kwa sasa imefungua hosp/idara yake ya matibabu ya moyo.
   
 11. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,412
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya Dr. Masao hakusoma alama za nyakati! Kulikuwa na upinzani wa waziwazi toka kwenye high circles juu ya huduma hii, nafikiri ule ulikuwa wakati muhimu kwake kuwa na "plan B". Kiukweli huduma za moyo pale THI hazikupewa umuhimu wowote kwa sababu INDIA ipo. Hata wafadhili wa wagonjwa wa moyo, hasa watoto, wali-prefer kuwapeleka INDIA. Siku moja nilipokuwa na mgonjwa wangu pale THI, Nilishangaa kuwaona akina mama wajawazito wanaosubiri kujifungua. From magonjwa ya moyo, to Maternity home? Khaa sikuelewa!! Lakini kama mpangaji wako hakulipi kodi unatakiwa kufanyaje? Bunge lilikwisha rekebisha sheria ya upangishaji wa nyumba, NSSF wameitumia! Kwa Dr. Masao, wamekuchukulia kofia lakini akili yako unayo. JIPANGE UPYA!!
   
 12. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,757
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 280
  Dr.Amechelewa kujipanga,ni muda mrefu sana amepewa notisi na NSSF.
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Vyovyote iwavyo issue ya Dr Masao inasikitisha na kukatisha tamaa! Hii ilikuwa ni kwa faida yetu.Kuna vitu huwezi ku quantify thamani yake jamani! Tujiulize hapo TUMEOKOA nini? Tunataka nini Taifa hili?
   
 14. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni visasi tu! ndivyo tunavyotumia mamlaka tuliyopewa na umma! Upinzani ulianza kabla hata haijaanza kufanya kazi na wafadhili walisusa kupeleka pale wagonjwa (nadhani kwa maelekzo maalum). Okay tumemkomoa Dr Masao?
   
 15. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Oh kumbe ni huyu dr nilishapewa 411 zake! wow finally serikali imeweza kumfungia mmh!.....dayuuuuuuuuuuuum!....Inshallah one day Dr Masau....
   
 16. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nilisikia tangazo la mnada radio one leo asubuhi.i Nilishangaa sana.
   
 17. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mambo ya kuendekeza sera za nyerere hayo..uzalendo nirudi nyumbani nikajenge nchi,my foot!ndiyo malipo yake hayo sasa
   
 18. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Iko wapi ktk Tanzania hii?
  SUBIRI hadi mwakani uone kama itakuwa imeanza kufanyakazi.
   
 19. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sijui kwa kusema hivyo unamaanisha nini?

  Umewahi kufikiri gharama ya kumpoteza raia mmoja ikoje?
  Je! Umekwisha wahi kufikiri hasara ya kumpoteza raia mwenye ujuzi na weledi kwa Taifa hili ni kubwa kiasi gani?
  Umewahi kufikiri ni hasara kubwa kiasi gani Taifa linapata kwasababu watu hawaendi kuzalisha mali au kutoa huduma kwa kuwa ni wagonjwa?
  Pia ukifikiria gharama ya kuokoa maisha ya watu na kujadili kupata suruhu ya pango ni jambo la kupuuzwa kwa kiasi hicho?

  Hivi wakija wale wenye ngozi kama ya nguruwe huwa mnawapa msamaha wa kodi kiasi gani?

  Katika kujibu maswali hayo huenda ama uwezo wako wakufikiri au kuwaza ukabadilika na kuliƶna hili kwa mtazamo mpya.
   
 20. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  aombe kitambulisho cha Uzanzibari then ...
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...