Dr. Emmanauel Nchimbi secondary school

kanda2

JF-Expert Member
Apr 22, 2007
1,318
72
Emmanuel Nchimbi alipokuwa mkuu wa wilaya ya Bunda-Mara alijipa ujiko na kuipa shule ya sekondari jina lake akiongeza na Title ya Udaktari feki wake.

Jina shule bado linaitwa Dr.Nchimbi sasa hatuwezi kufanya mpango wa kubadili jina la shule ile? Vijana wanaosoma shule hiyo wakisoma kitabu hiki cha Msemakweli wanaweza kuathirika kisaikolojia.

Vyeti vyao vitakuwa na jina ambalo limejipachika hadhi isiyo yake tena ya kitaaluma. matokeo ya kidato cha nne mwaka huu ya shule hiyo ni mabaya sana. na kusikika kwa habari hizo ndio kutazidisha kufanya matokeo yawe mabaya zaidi.

Tufanyanye nini huko Bunda?
 
Navyofahamu mie jina la shule, mtaa, zahanati nk huwa hayapendekezwi au kutolewa na mkuu wa wilaya!! Na kwa majina ya shule wahusika ni kamati ya shule& afisa elimu wa wilaya au mkoa...na ni wao km kuna lawama ndo wastahili kupewa kwa kujipendekeza kwao na kutowa majina ya watu wasiostahili! Kwa hapa tumwache Dr (?) Nchimbi wa watu jamani
 
Wewe mzazi jaribu kumpa mwanao Jina kama Hasara, Matatizo, Mjinga, Mwizi, Jambazi, Uchuro, Kisasi, etc uone kazi. Huyo mtoto ataathirika kisaikolojia na kuanza kuwa na tabia inayofanana na hiyo laana uliyombatiza. Please, tuinapochagua majina ya watoto, mtaa, shule, kijiji, kata, wilaya, mkoa etc lazima tuwe waangalifu. Imagine wewe umeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa au we unatoka kwenye mkoa unaitwa MALAYA, FISADI, MWIZI, je utajisikiaje? Please, kuna haja ya kuaangalia upya jina la shule hii kama kuna ushahidi wa kutosha kuwa Dr. Nchimbi kweli PhD yake haina hadhi hiyo!!!
 
Mwenzenu ngoja nibadili wilaya ya Sikonge na kuifanya wilaya ya EPA na kijiji chetu ntakiita RICHMOND. Jina la kata liwe Lowassa na Mtaa uwe Kingmaker.
 
Mwenzenu ngoja nibadili wilaya ya Sikonge na kuifanya wilaya ya EPA na kijiji chetu ntakiita RICHMOND. Jina la kata liwe Lowassa na Mtaa uwe Kingmaker.

Sikonge, yatakushinda!! Huko hakuna Mtemi wa Sungusungu tumuombe akukamate mara moja. Nikipata muda nitakuasa kwa lugha ya Kinyamwezi au Kisukuma ili uelewe vizuri athari ya majina ambayo kwenu munayaita ya NGELO. Sikonge, lekaga amamihayo ago gati na ntwe na magulu!!!
 
'Chuki' dhidi ya Nchimbi inahamishiwa mpaka kwa shule..

Objectivity sufuri.
Nunda mmoja anpochomoza kwa ujanja ujanja akipata madaraka anawezakutengeneza manunda wengi zaidi wa aina yake.
Si ajabu watakaofaulu toka shule hii watakuwa moja kwa moja ma-"DR"
 
Naona objectivity bado sana.

Shule itabaki kuwa shule tu, japo itaitwa Nchimbi et etc. Jina halina correlation na kilichomo. Kuwa na jina 'zuri' hakusaidii lolote kama hakuna vitu vya kuwezesha kuwa shule nzuri, and the converse is a tautology.

Sasa nyie endeleeni kupiga domo.
 
Wewe mzazi jaribu kumpa mwanao Jina kama Hasara, Matatizo, Mjinga, Mwizi, Jambazi, Uchuro, Kisasi, etc uone kazi. Huyo mtoto ataathirika kisaikolojia na kuanza kuwa na tabia inayofanana na hiyo laana uliyombatiza. Please, tuinapochagua majina ya watoto, mtaa, shule, kijiji, kata, wilaya, mkoa etc lazima tuwe waangalifu. Imagine wewe umeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa au we unatoka kwenye mkoa unaitwa MALAYA, FISADI, MWIZI, je utajisikiaje? Please, kuna haja ya kuaangalia upya jina la shule hii kama kuna ushahidi wa kutosha kuwa Dr. Nchimbi kweli PhD yake haina hadhi hiyo!!!

Huyu Nchimbi amekili mwenyewe pengine bila kujua kuwa muda wote huu akijiita "DR" alikuwa hastahili kuitwa hivyo; yeye amejiandikisha upya Chuo Kikuu cha Mzumbe akisomea huo UDAKTARI!!!. Ndio maana hata vile vitisho vyake vya kwenda mahakamani hakuvitekeleza kwani angeumbuka big time!! Kuwaepusha wanafunzi wasiathirike kisaikolojia ingefaa jina la shule hii libadilishwe na hapo baadae kama ikibidi waiite jina hilo wakipenda mara atakapofanikiwa kuhitimu huo udaktari anaousaka sasa!!
 
Naona objectivity bado sana.

Shule itabaki kuwa shule tu, japo itaitwa Nchimbi et etc. Jina halina correlation na kilichomo. Kuwa na jina 'zuri' hakusaidii lolote kama hakuna vitu vya kuwezesha kuwa shule nzuri, and the converse is a tautology.

Sasa nyie endeleeni kupiga domo.
Tunapolaani matendo ya mtu fulani kutokana na ubadhilifu au kudanganya ni kumpa fursa huyo mtu abadilike. Mfungwa hufungwa kwa makosa aliyoyafanya, na akitoka kwenye uraia huanza maisha upya. Nchimbi pamoja na kuwa na hiyo PhD (msemao ya uongo), lakini vilevile ana basic education. In case he can plead and change, I don't see a problem. He is a human being who has committed a mistake, tumpe time; tusiwe na hizi condemnation za "kijihadist". He got a message.
 
Hivi kuna grounds gani zinazotumika kuipa shulw jina la mtu binafsi? Hilo mi ndo najiuliza zaidi kuliko kuwa hao madogo watafaulu au la
 
Huyu Nchimbi amekili mwenyewe pengine bila kujua kuwa muda wote huu akijiita "DR" alikuwa hastahili kuitwa hivyo; yeye amejiandikisha upya Chuo Kikuu cha Mzumbe akisomea huo UDAKTARI!!!. Ndio maana hata vile vitisho vyake vya kwenda mahakamani hakuvitekeleza kwani angeumbuka big time!! Kuwaepusha wanafunzi wasiathirike kisaikolojia ingefaa jina la shule hii libadilishwe na hapo baadae kama ikibidi waiite jina hilo wakipenda mara atakapofanikiwa kuhitimu huo udaktari anaousaka sasa!!

Kwenye bold hapo.
Yaani baada ya kupata kashfa ya kupata PhD ndio anaenda kuitafuta PhD yake Mzumbe?? Mbona hapo hata walimu wenyewe tunasikia wana PhD kama yake? Kwanini asisome hapo SUA au UDSM tu kama alivyofanya Dr.Mag.? Aache kwenda sehem za mashaka unless kama ana mashaka na uwezo wa kupiga kitabu.
 
Nchi yetu watu kwa kupenda ujiko. Sasa kuweka title katika jina la institution ndio nini? Dr ya nini katika jina la shule? Itabidi basi hata shule nyingine zitangulizwe na titles, mf: Mr. Shaaban Robert Sec School, Mrs. Barbro Joha Sec School etc.

Tanzania ukimu'address Profesa bila kutanguliza Prof. inakuwa kashfa.
 
Katoma you right ,Watz tunajisikia sana hasa ukiwa na elimu feki au wadhifa fulani.
kuna shule inaitwa Dr John Magufuli vilevile.For God sake !
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom