Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,606
- 696,708
Intelijensia ya Mugabe kali lakini pia tunaweza kusema ni ya aina yake na ya kushangaza pia kama si kuchekesha... Ana mapandikizi informers mpaka kwa matabibu wa nguvu za giza...!!!
Makamu wa rais baada ya kusubiri sana babu afe ama walau ang'atuke na kumwachia madaraka makubwa kama alivyofanya Mwl. J. K. Nyerere mwaka 1984 na kumwachia Mzee Mwinyi....! Akaona hakuna hata dalili za kufa ama kuachia madaraka... Waswahili wana msemo wao.... Ngoja ngoja yaumiza tumbo!
Dr Mnangagwa akachoka kusubiri, akashindwa kabisa kungoja, akajiuliza hiki kikongwe. Kimekula nini mpaka katika umri huu wa miaka 93 hakifi tuu!? ... Akaamua apate jibu lake kupitia nguvu za giza, wataalam wa kupuliza walau wamsaidie kumwambia ni lini babu anaweza ku rest in piece ⚰... Ni katika kuhangaika huko kumbe kati yao kuna mapandikizi ama Mzee babu ni mteja wao.... Wakaenda kumsemea kwa siri, wakamwambia mzee kama hujui jua sasa...! msaidizi wako mkuu kazini anatuuliza tumwambie UTAKUFA LINI!??? Yani hawakutaka kuzunguka walienda direct moja kwa moja....
Khaa mzee babu akaona hii ni treason kabisa! Neno la kiingereza hili ile lugha ya malkia Queen Elizabeth wa ngapi sijui pale Birmingham Uscotsh.. Tamka uskotishi... Yaani msaidizi wangu ninayemuamini ananichulia kifo!? Akaiona hatari kubwa iliyo mbele yake...
Haikuchukua masaa 24, akamfuta kazi mazima.... Sasa hivi Makamu wa rais wa Zimbabwe bwana Emarsson Mnangagwa yuko South Africa kwa wazulu, kakimbilia huko... MUGABE HATAKAGI UPUUZI KABISA