Dr. Elly: Siyo kila mtu anatakiwa avae maski bali wanaohudumia wagonjwa na wanaohisi wameathirika

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
34,122
2,000
Kuna mjadala wa jinsi ya kujikinga na virusi vya Corona unaendelea muda katika luninga ya Channel Ten.

Mtaalamu Dr Elly Josephat kutoka MAT anasema kuvaa maski kwa mujibu wa maagizo ya WHO ni kwa wale wanaohudumia waathirika na wale wanajishuku au kuhisi kuwa wameathirika.

Na kuna jinsi ya kuvaa hizi maski, kama wewe unamhudumia muathirika ule upande wenye rangi ya blue ambao ndio una dawa unakuwa nje na kama wewe ni muathirika upande wenye rangi ya blue unakuwa ndani ili pumzi au sauti inapotoka tu inakutana na dawa kinga.

Source: Channel Ten
 

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
404
1,000
Kuna mazingira mawili makuu ya kuvaa mask

1. Unapohudumia mgonjwa ambaye unahisi au kathibitishwa ana Corona.

2. Unapokohoa ama kupiga chafya kama Mgonjwa au Mshukiwa wa Corona

Wenzetu China walikuwa wanahamasisha kuvaa mask Kwa watu wote, kitu ambacho WHO na nchi za Ulaya na Marekani hawaamini kama kinapunguza maambukizi.
 

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
22,918
2,000
Kwahiyo tajiri wa Simba kavua ile mask yake..

Mwana FA naye atakuwa kavua ile yake pia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom