Dr. Edward Mwaikali avuliwa Uaskofu Dayosisi ya Konde KKKT

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,857
13,140
images.jpeg-14.jpg

Nimepata tetesi kuwa katika Mkutano Mkuu wa Dayosisi ya Konde KKKT, ulioitishwa na Mkuu wa Kanisa, leo 22/03/2022, aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Konde Dr. Edward Mwaikali , amevuliwa Uaskofu.

====

Mkutano mkuu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde umemuondoa madarakani aliyekuwa askofu wa Dayosisi hiyo Dr Edward Mwaikali pamoja na wakuu wa majimbo takribani watatu waliokuwa wakimuunga mkono na muda huu uchaguzi wa askofu mpya unafanyika .

Matokeo ya Awali;

Askofu mpya :Mwakihaba

Msaidizi Askofu: Mch Njinga

Dr Edward Mwaikali kavuliwa uaskofu

Mwambola kavuliwa uchungaji na ukuu wa Jimbo.

Kajela kavuliwa uchungaji

Mwakanyamale kavuliwa uchungaji

Clip ya mambo yalivyokiwa toka Busokelo Tv:
 
Sijawahi kuwaelewa KKKT wether ni dhehebu au chama cha siasa..kuazia pale mnachagua hao maasikofu yaan rushwa kama chaguzi za SSM
Wacha UMBEA, Hebu wataje hao waliotoa au kupokea rushwa.

Ukiona dhehebu au Kanisa lina uwezo na mamlaka juu ya Maaskofu ujue hilo kanisa ni zuri sana.

Tatizo lipo kwa yale makanisa ambayo Mtu anajiita Nabii, Mtume n.k halafu yeye ndio mwamuzi wa mwisho kwa kila kitu.

Hakuna mwenye mamlaka zaidi yake hata akifanya uovu hakuna wa kumwadhibu.
 
Makanisa yote kuanzia katoliki hadi kwa Gwajima wakati wa uchaguzi wa viongozi ni rushwa tupu.

Ndio maana tunasema makanisa ni taasisi za kitapeli. Mungu hayupo.
Kanisa Katiliki liondoe hapo, hakuna uchaguzi huwa unafanywa.

Wanamchagua nani? Kama ni Pope huwa wanaenda kumpigia kura mtu au Cardinal aliyependekezwa Vatican.

Wanaenda Cardinals. Huu uchaguzi wa kunyosha vidole juu unafanywa na madhehebu mengine!
 
KKKT hamna kanisa hapo, huu Ni ukweli mchungu Sana.
Kuchagua tu maaskofu Kuna Kuna na rushwa na vitimbi vya kila aina. Ukija kwenye mambo ya fedha ya Jimbo ndio hakufai kabisa
Acha chuki wewe,migogoro haipo Roma tu,ambako waumini ni kondoo ' kimfumo!

Lutheran kinachotokea ni aina ya Demokrasia iliyopo ndani...ndio maana ukizingua unazinguliwa!
 
Back
Top Bottom