Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Tahadhima kwenu wajumbe wa bodi huru!

Kwa muda sasa nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu Waziri huyu toka alipoteuliwa na Rais Magufuli kuwa Waziri wa Afya. Namzungumzia Dk. Dorothy Gwajima.

Kila ofisi zilizochini yake anapoingia huwadhalilisha sana madaktari wenzake. Dk. Gwajima anamtazama kila mtu kuwa ni mwizi na kujitapa kuwa hakuna anayejua kila kitu katika wizara hiyo kama yeye.

"Hivi mnajua mimi ni Field Marshal wa sekta ya afya?" anawafokea madaktari Bingwa zaidi yake na kuongeza, "kama ningekuwa Mwanasheria mngenidanganya sana" kuonesha kuwa mtangulizi wake Mwanasheria, Ummy Mwalimu alikuwa akidanganywa sana. Huku ni kumdharau Waziri mwenzie aliyeaminiwa na Rais Magufuli.

Lakini hata "body language" ya mama huyu inaonesha kuhemka mno kiasi Cha kufanana na kina mama "ndala ndefu" wa huko Tandale wanaochambana bombani huku ameshika kiuno.

Cha ajabu, kama alivyowahi kufanya Dk. Hamisi Kigwangala "mzee wa kukurupuka" naye kila anapotaka kuwadhalilisha wahudumu wa sekta hiyo ni lazima awe mbele ya kamera ili aonekane. Huyu mama ameenda mbali kiasi Cha kutorokwa hata na haiba na staha ya mwanamke wa Kitanzania mbele ya wanaume.

"Field Marshal" ni cheo Cha juu na Cha mwisho jeshini. Hivi, Dk. Gwajima anadhani ni Bingwa wa afya kuliko maprofesa wote wa tiba nchini? Kwani kuongoza ni lazima kudhalilisha wenzako hadharani?

Wakati yule "mkata viuno" aliyetembea na Ilani ya CCM akijiita "ninja" huyu kaja na skafu ya bendera akijiita "Field Marshal". Mwendo uleule wa kukurupuka na kujipendekeza.

My Take: Napendekeza madaktari wafuatilie faili lake la matibabu anakotibiwa kuona anasumbuliwa na ugonjwa gani? Yapo baadhi ya magonjwa ambayo humfanya mtu ku-react ukichaa kama mama huyu.

Lakini pia wadadisi wachunguze mahusiano yake ya ndoa. Je, ana familia au ni mtalikiwa? Maana mahusiano ya ndoa na familia yakiwa salama pia huleta utulivu katika uongozi wenye staha, hekima, busara na maarifa. Huwezi kukufanya kuwa wizara hiyo imeoza kiasi kwamba waliopita kabla yake hawakufanya chochote. By the way, si tunaambiwa utawala wa Magufuli umeondoa ufisadi na uzembe kazini?

Nawasilisha.
 
Kifupi serikali ya sasa ni mwendo wa vitisho tu siyo kutoa order!

"Wakurugenzi wote wasimamie hili, atakayeshindwa ahesabu hana kazi"

Kazi za umma zimekuwa za hovyo kuwahi kutokea katika vipindi vyote!! Maana nako tunapokea vijiti vya vitisho tu, kwa kila mtu kuogopa kuhesabu hana kazi!!
 
Hapana wewe ndiye una upungufu wa uelewa. Pamoja na mapungufu yaliyopo ya sekta ya afya, ila kulikuwa na wizi sana na mlizooea kuiba mno na kutoa huduma mbovu bila kujua wajibu wenu. Acha awanyooshe kabisa mlijijaza uzembe. Kikubwa mfano wa kuacha kutumia GOT HOMIS sekta ya afya inaibiwa mno. Pia waziri huyu anayo dhamira ya kazi toka moyoni mwake. Labda lile tukio la mkunga ndiyo linahitaji busara juu yake.
 
Back
Top Bottom