DR Congo yatishia kuchukua hatua za Kimataifa dhidi ya Angola

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetishia kuchukua hatua za kimataifa dhidi ya Angola kufuatia kufurushwa kwa takriban Wacongo laki mbili kutoka taifa hilo jirani, huku ikiripotiwa waliondolewa nchini humo kwa nguvu na kwa kutumia ghasia.

Waziri wa mambo ya nje wa Congo Leonard She Okitundu amesema nchi yake inaitaka serikali ya Angola kufanya uchunguzi wa kina kujua ni kina nani walihusika na vitendo hivyo vya kikatili, la sivyo watalazimika kuliwasilisha suala hilo katika ngazi ya kimataifa.

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu, Angola imewafukuza Wacongo karibu laki mbili kutoka jimbo la kaskazini la Lunda Norte, linalopakana na Congo, wengi wao wakitajwa kuwa wahamiaji haramu wanaofanya kazi katika migodi ya Almasi.

Kulingana na ripoti iliyowasilishwa katika kikao cha baraza la mawaziri, kilichosimamiwa na Rais Joseph Kabila, Wacongo 30,000 walifukuzwa Angola katika mazingira ya ghasia na wengine waliuawa

IMG_20181019_083952_067.jpg
 
Back
Top Bottom