DR Congo: Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu athari za kuvunja muungano wa kisiasa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,776
2,000
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umetahadharisha hapo jana kwamba mzozo wa kisiasa nchini humo uliochochewa na hatua ya rais Felix Tshisekedi kuuvunja muungano kati ya vyama tiifu kwake na rais wa zamani Joseph Kabila huenda ikaathiri uchumi wa taifa hilo na hali ya kiusalama iwapo hautasuluhishwa.

Kiongozi wa ujumbe huo nchini Congo, Leila Zerrougui ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba hatua hiyo inaweza kuwa na athari kubwa na kuchochea kufikiwa kwa makubaliano yatakayotanguliza maslahi ya watu wa Congo, kabla ya malengo ya muda mfupi ya kisiasa ambayo yanaweza kuongeza wasiwasi.

Wanachama 15 wa baraza hilo walifanya kikao cha ndani baada ya taarifa hiyo, lakini halikuchukua hatua zozote za haraka na wala halikutoa taarifa yoyote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom