DR Congo: Takriban watoto 5,000 wafariki kutokana na mlipuko mbaya zaidi wa surua dunianigaza janga la surua

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,103
Ugonjwa wa ukambi ama Surua umewaua takriban watoto 5000 katika taifa la Jamhuri ya KidemokrasIa ya Congo mwaka 2019, kulingana na mamlaka baada ya ugonjwa huo kusambaa hadi mikoa yote.

Takriban watoto 250,000 wameambukizwa mwaka huu pekee.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa ugonjwa huo ndio janga linalosambaa kwa kasi mno.

Ugonjwa huo wa surua nchini DR Congo umeua idadi ilio mara mbili ya wagonjwa waliofariki kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola katika kipindi cha miezi 15 iliopita.

Serikali ya DRC kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO imezindua chanjo ya dharura mwezi Septemba inayowalenga watoto 800,000.

Lakini miundo msingi mibaya, mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, mbali na ukosefu wa tiba za mara kwa mara zimekwamisha juhudi za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Watoto milioni 4 tayari wamepewa chanjo, lakini wataalam wameonya kwamba idadi hiyo ni chini ya nusu ya jumla ya watoto nchini humo na kwamba chanjo zilizopo hazitoshi.

Wengi ya wale walioathirika na ugonjwa huo ni watoto wachanga.

Je surua ni nini?

Surua ni virusi vinavyosababisha mtoto kuwa na mafua , kuchimua mara kwa mara na kuwa joto mwilini.

Siku chache baadaye mgonjwa anapata vipele mwili mzima ambavyo vinaanza usoni na kusambaa mwilini.

Wengi hupona , lakini surua inaweza kusababisha ulemavu wa muda mrefu. Inaweza kusababisha kifo hususan iwapo utasababisha homa ya mapafu ama uvimbe katika ubongo.

Inakadiriwa kwamba jumla ya watu 110,000 duniani hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.

1574420247359.png
 
Back
Top Bottom