DR Congo: Rais Tshisekedi aamua kuvunja Serikali ya Muungano

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,663
2,000
Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi, aamua kuweka mpango wa kuvunja Serikali ya Muungano na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Katika hotuba yake kupitia matangazo ya televisheni Jumapili , bwana Tshisekedi alisema atachagua maofisa wapya kuunda Baraza jipya kwani Bunge la sasa lina wafuasi wengi wa Kabila ambao hawamsikilizi.

Alisema alikuwa amejiandaa kuvunja bunge lote kama kuna ulazima.

Takribani miaka miwili sasa, DRC iliunda serikali ya muungano, baina ya chama cha kabila na chama cha rais mpya Tshisekedi, vyama viwili ambavyo vilipingana kwa kipindi cha muda mrefu vilikubaliana kufanya kazi kwa pamoja, lakini baada ya siku chache tu mvutano ulianza kati ya vyama hivyo.

Baadhi ya wafuasi wa chama cha Tshisekedi walianza kususia ushirikiano huu, huku wakiwashutumu wafuasi wa chama cha kabila kumzuia rais mpya kutekeleza ahadi zake.

Hivi karibuni , katibu mkuu wa UN na kiongozi wa Umoja wa Afrika walieleza wasiwasi wao juu ya mvutano wa kisiasa wa pande zote mbili.
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,522
2,000
Waje Tanzania kukifunza Siasa za maridhiano

Bara Kamanda Halima Mdee na wenzie 18 kutoka Chadema wamekuwa Wabunge

Kule Znz Seif Sharif kala U makamu

Wazungu waliojipanga kuchochea kwa kujifanya kuja kusuluhisha wameumbuka
 
cmoney

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
3,267
2,000
Waafrika wamekuwa majogoo kugombanishwa na hao mabeberu kila Mara kwa maslahi yao? Vitu vingine Ni upumbavu
ungeweza kufikiri kwa kutumia akili badala ya kuwaza makoti ambayo hata hujawahi vaa usingepost hicho...fuatilia mgogoro wa congo vizuri kabla hujapost...Afrika for Afrikans....viongozi upande wa kabila walikua wananufaika kuuza rasilimali kwa mataifa ya ubelgiji na marekani....sasa wanamchallenge Tshisekedi akiingilia fursa zao
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,649
2,000
kabila bado anatawala

Unaweza kushangaa hata week hamalizi Wana mu-assasin . Anataka kuondoa maslahi ya waliomuweka

Tatizo Wacongomani starehe mno, wasipo kuwa serious na kuachana na mambo ya boringo boringo 24X7 wataendelea kutawaliwa na Watutsi miaka nenda rudi - Tsishekedi hasipokuwa makini yatampata yaliyo mtokea kwa Kabila Sr - hawa watu wako determined kuivuruga Congo DRC kwa plan zao ya muda mrefu za kutaka kupora jimbo lote la KIVU na kuliunga na Rwanda hapo wala mabeberu hawa husiki lolote - Nchi zote za Afrika zinapaswa kulishugulukia suala hili mapema kwa kuwapa onyo kali utawala wa Rwanda kwamba ujinga huu wa ku- incite vurugu kwa nchi jirani wether overtly au covertly hawezi kuvumilika hata kidogo, bila nchi za kiafrika kuwa na msimamo thabiti jamaa hawa wataivuruga sana Congo DRC - my opinion.
 
Emiir

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
23,946
2,000
Kabila anapenda sana madaraka na kwamba tangu aondoke madarakani bado anatamani madaraka, Na kinachonipa moyo kumhusu Tshisekedi ni kwamba anataka awapatie maendeleo Wakongomani. Tatizo ni je ataweza kufanya hivyo kwa maana mtangulizi wake bado anataka amtumie kama puppet wake, all in all namtakia kila la kheri Tshisekedi lakini lazima ajue hayuko salama.
 
hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
41,905
2,000
Tatizo Wacongomani starehe mno, wasipo kuwa serious na kuachana na mambo ya boringo boringo 24X7 wataendelea kutawaliwa na Watutsi miaka nenda rudi - Tsishekedi hasipokuwa makini yatampata yaliyo mtokea kwa Kabila Sr - hawa watu wako determined kuivuruga Congo DRC kwa plan zao ya muda mrefu za kutaka kupora jimbo lote la KIVU na kuliunga na Rwanda hapo wala mabeberu hawa husiki lolote - Nchi zote za Afrika zinapaswa kulishugulukia suala hili mapema kwa kuwapa onyo kali utawala wa Rwanda kwamba ujinga huu wa ku- incite vurugu kwa nchi jirani wether overtly au covertly hawezi kuvumilika hata kidogo, bila nchi za kiafrika kuwa na msimamo thabiti jamaa hawa wataivuruga sana Congo DRC - my opinion.
Kweli kabisa
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
6,714
2,000
Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi, aamua kuweka mpango wa kuvunja Serikali ya Muungano na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Katika hotuba yake kupitia matangazo ya televisheni Jumapili , bwana Tshisekedi alisema atachagua maofisa wapya kuunda Baraza jipya kwani Bunge la sasa lina wafuasi wengi wa Kabila ambao hawamsikilizi.

Alisema alikuwa amejiandaa kuvunja bunge lote kama kuna ulazima.

Takribani miaka miwili sasa, DRC iliunda serikali ya muungano, baina ya chama cha kabila na chama cha rais mpya Tshisekedi, vyama viwili ambavyo vilipingana kwa kipindi cha muda mrefu vilikubaliana kufanya kazi kwa pamoja, lakini baada ya siku chache tu mvutano ulianza kati ya vyama hivyo.

Baadhi ya wafuasi wa chama cha Tshisekedi walianza kususia ushirikiano huu, huku wakiwashutumu wafuasi wa chama cha kabila kumzuia rais mpya kutekeleza ahadi zake.

Hivi karibuni , katibu mkuu wa UN na kiongozi wa Umoja wa Afrika walieleza wasiwasi wao juu ya mvutano wa kisiasa wa pande zote mbili.
Siasa za Africa full comedy.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom