DR Congo: Polisi yamzuia Fayulu kuhutubia wafuasi wake

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
730
2,957
DRC: Polisi yamzuia Fayulu kuhutubia wafuasi wake

Polisi wamezuia wafuasi wa Martin Fayulu kukusanyika kwenye makao makuu ya chama chake alitakorajiwa kuwahutubia. Ingawa Korti ya Katiba imethibitisha ushindi wa Felix Tshisekedi, Fayulu anadai ameibiwa ushindi wake.

Msemaji wa Martin Fayulu Eve Bazaiba amesema polisi walivamia mahali ambako Fayulu alikusudia kuwahutubia wafuasi wake, na kulibeba jukwaa na vipazasauti vilivyokuwa vimeandaliwa.

''Wamevikamata vyombo vyote na kuwakamata pia watu, na sijui wamewapeleka wapi.'' amelalamika Bazaiba na kuongeza, ''nilipouliza kinachoendelea, nimeambiwa polisi wanacho kibali cha kuwazuia watu kuingia na kutoka.''

Licha ya kutawanywa na polisi baadhi ya wafuasi wa vuguvugu la upinzani la LAMUKA linalomuunga mkono Fayulu waliendelea kusubiri kuwasili kwa kiongozi wao kwenye makao makuu ya chama cha MLC.

Fayulu na wafuasi wake ambao wamepinga matokeo yaliotolewa na tume ya uchaguzi na kujitangaza kuwa mshindi wa uchaguzi huo amesema kwamba ni lazima raia wa kongo wapewe haki zao.

Chanzo: DW
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom