DR Congo: Mgombea wa upinzani, Felix Tshisekedi ashinda Urais. Mgombea mwenza apinga matokeo hayo

Asante sana papa Joseph Kabila kwa kuruhusu mkono wa democrasia, itapunguza Uhasama na makundi.Bale balitaka kuona machafuko zaidi bapate dorari zaidi na masoko mahindi na wana jeshi bao,bajirudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambacho sijaelewa imekuwaje namba 2 sijui 3 kawa wa kwanza. Na je France na Kanisa katoliki zinauwezo wa kubadilisha matokeo? Je bwana Felix ameingia makubaliano na kina Kabila? Je wakiamua kurudia kupiga kura na kuiweka ile mikoa ambayo haikupiga kura kwasababu ya Ebola, je matokeo yatampendelea Bwana Felix? Ningependa kujua SADC wamesemaje kuhusu haya matokeo kwasababu wale ndiyo wananguvu Congo kuliko France na Kanisa katoliki kama sijakosea!DRC kuna maswali mengi kuliko majibu!
Hahaa watu na mipango yao " kabila hataki ujinga aise

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahali ambapo kuna demokrasia ya kweli na ambapo wananchi wanapewa uhuru wa kuchagua wamtakaye , Maamuzi ya nani awe kiongozi huamuliwa na wananchi wenyewe.

Joseph Kabila mamluki aliyepewa uongozi wa DRC kwa njia za panya hatimaye ameanguka rasmi , Mgombea wa chama chake ameanguka vibaya sana , hata mamluki aliyemweka aitwaye Shishekedi naye ameanguka ! Martin Fayulu Mgombea wa wananchi ameshinda kwa kishindo , Tayari Serikali ya Ufaransa imepinga Mamluki Shishekedi kutangazwa mshindi , bado tunasubiri tamko la kanisa Katoliki ambalo linao ushawishi mkubwa sana kwenye siasa za Congo , bali kinachojulikana ni kwamba Kabila ameanguka mithili ya gunia lililojaa uchafu linavyotupwa dampo.

Shukrani kuu iende kwa taasisi za Kimataifa zilizohakikisha Mamluki Kabila anashindwa.

Mungu ibariki DRC[/QUakubari
OTE]
Belgium na France naona bado wanaweweseka mtu wao Martin hajapita na kabila aliona bora ampe Felix cos yupo naye karibu kuliko Martin,generally kabila amekufa kiume na bora amempa mpinzani maana angejifanya kumpa nchi Rama Congo isingetawalika tena
 
Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC

_105127738_gettyimages-1079948250.jpg
Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tume ya uchaguzi imesema.
Matokeo ya awali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary.
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, alisema mapema Alhamisi kwamba Bw Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi wa urais mteule."

Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye Bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni, huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura 4.4 milioni.
Matokeo yaliyotangazwa na CENI:
  • Felix Tshisekedi 7,051,013 (38.57%)
  • Martin Fayulu Madidi 6,366,732 (34.83%)
  • Emmanuel Shadary 4,357,359 (23.84%)
*Waliojitokeza kupiga kura kwa mujibu wa CENI ni 47.56%.
Bw Fayulu ameyapinga matokeo hayo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
Ameambia Idhaa ya Kifaransa ya BBC kuwa: "Hii ni kashfa mbaya sana. Matokeo haya hayana uhusiano hata kidogo na ukweli halisi. Raia wa Congo hawataukubali utapeli kama huu daima. Felix Tshisekedi hakupata kura 7 milioni, haiwezekani. Alizitoa wapi?"
_105127740_goma.jpg
Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionWafuasi wa Bw Tshisekedi wakisherehekea mapema asubuhi mjini Goma, mashariki mwa DRC
Bw Tshisekedi, kwa upande wake ameyafurahia matokeo hayo na kumsifu pia rais anayeondoka Joseph Kabila.
Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mji mkuu Kinshasa, Tshisekedi amesema atakuwa "rais wa raia wote wa Congo".
"Namshukuru Rais Joseph Kabila ambaye leo hatufai tena kumchukulia kama adui, lakini kama mshirika katika mabadiliko ya kidemokrasia nchini mwetu," amesema.
Idhaa ya kifaransa ya BBC?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona inaonesha matokeo ya awali? Nadhani mshindi hajatangazwa rasmi. Nasema hivi kwa kuwa Congo nayo ni nchi ya Afrika na Waafrika tunajuana. usishangae ukasikia mengine!
 
Back
Top Bottom