DR Congo: Mgombea wa upinzani, Felix Tshisekedi ashinda Urais. Mgombea mwenza apinga matokeo hayo

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,212
113,503
Opposition named winner in DR Congo poll

Mgombea urais wa upande wa upinzani huko Congo-Kinshasa, Bw. Felix Tshisekedi ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais na tume ya uchaguzi ya nchini humo, CENI.

Hii ni habari mpya kabisa kwa hiyo taarifa zaidi zitafuatia.

Ila nahisi kama chama tawala hakitokubali matokeo. Nahisi tu.

Tusubiri tuone........
=======

Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia wa Congo uliokuwa una ushindani mkubwa, tume ya uchaguzi imesema Alhamisi.

Matokeo ya awali yameonyesha kuwa yeye anaongoza katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya mgombea wa upinzani Martin Fayulu, na yule wa muungano wa chama tawala Emmanuel Shadary.

Atakapo thibitishwa, Tshisekedi atakuwa mshindani mpinzani wa kwanza kushinda tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupata uhuru.

Rais Joseph Kabila anaachia madaraka baada ya miaka 18 ya uongozi wake.

Alikuwa ameahidi kuwepo kubadilishana madaraka kwa njia ya utulivu DRC tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Ubelgiji 1960.

Chanzo: VOA Swahili

=============

Martin Fayulu, mgombea urais wa upinzani DRC aliyeibuka wa pili, ameyakataa matokeo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) yanaonesha Felix Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi mteule wa urais."

Bw Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye Bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni, huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akimaliza wa tatu akiwa na takriban kura 4.4 milioni.

Bw Fayulu ameambia Idhaa ya Kifaransa ya BBC kuwa: "Hii ni kashfa mbaya sana. Matokeo haya hayana uhusiano hata kidogo na ukweli halisi. Raia wa Congo hawataukubali utapeli kama huu daima. Felix Tshisekedi hakupata kura 7 milioni, haiwezekani. Alizitoa wapi?"

Awali, alikuwa ameambia kituo cha redio ya Radio France International (RFI) kwamba matokeo hayo ni "mapinduzi halisi kupitia uchaguzi" na akatoa wito kwa waangalizi wa uchaguzi kuchapisha matokeo waliyo nayo aliyosema ni ya kweli.

Nchini DRC hata hivyo, ni kinyume cha sheria kwa mtu mwingine kando na CENI kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mji mkuu Kinshasa, Tshisekedi amesema atakuwa "rais wa raia wote wa Congo.

Kumekuwa na tetesi kwamba kucheleweshwa kwa shughuli ya kutangaza matokeo, ambayo awali yalitarajiwa kutangazwa Jumapili, kulitoa muda kwa Rais Kabila na Bw Tshisekedi kuafikiana.

Kanisa Katoliki limesema matokeo rasmi yaliyotangazwa na tume hiyo yanakinzana na matokeo ambayo yameandaliwa na waangalizi wake.

Wamedokeza kwamba Bw Fayulu alipata kura nyingi, kwa mujibu wa takwimu walizo nazo. Baadhi ya kura za maoni zilikuwa zinamuonesha Bw Fayulu akiwa mbele ya wagombea wengine.

Msemaji wa Bw Tshisekedi Claude Lbalanky ambaye amesema siku ya leo ni "siku njema kwa taifa" ameambia BBC kwamba hakuna makubaliano yoyote kati ya Rais Kabila na Bw Tshisekedi.

Kwa taarifa zaidi, soma:
Uchaguzi DRC: Martin Fayulu apinga matokeo ya urais DRC, Felix Tshisekedi afurahia na kumtaja Kabila kuwa 'mshirika muhimu'
 
Opposition named winner in DR Congo poll

Mgombea urais wa upande wa upinzani huko Congo-Kinshasa, Bw. Felix Tshisekedi ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais na tume ya uchaguzi ya nchini humo, CENI.

Hii ni habari mpya kabisa kwa hiyo taarifa zaidi zitafuatia.

Ila nahisi kama chama tawala hakitokubali matokeo. Nahisi tu.

Tusubiri tuone....
Uthibitisho upi tena zaidi NN??
kama CENI ndio kama NEC ya TZ imeshatoa matokeo sidhani kama kuna haja ya kusubiri kwingine kuseme!

It's over
 
Opposition named winner in DR Congo poll

Mgombea urais wa upande wa upinzani huko Congo-Kinshasa, Bw. Felix Tshisekedi ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais na tume ya uchaguzi ya nchini humo, CENI.

Hii ni habari mpya kabisa kwa hiyo taarifa zaidi zitafuatia.

Ila nahisi kama chama tawala hakitokubali matokeo. Nahisi tu.

Tusubiri tuone....
Kabila keshafanya mpango na Felix Tshisekedi kumsukuma Fayulu pembeni (ambaye ndiye anaungwa mkono na kanisa katoliki). Fayulu kanyang'anywa mkate hapo.
 
Safi sana.
Kweli mabadiliko hayawezi kuzuilika, unaweza kuyachelewesha tu.

Baba yake alipambania Demokrasia nchini DRC toka enzi za Mobutu, Laurent Kabila na hadi kipindi cha hichi cha Joseph Kabila, akiteswa na kusumbuliwa mpaka alipofariki. Lakini hii kizazi chake ndio kimechukua madaraka.
Kweli kama ipo basi ipo tu.

Ipo siku Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi tutafikia hatua hii mpya na njema ya DRC. Tumewachoka hawa madikteta. Hawana jipya.
 
Opposition leader Felix Tshisekedi has won theDemocratic Republic of Congo's (DRC) long-delayed presidential election, according to provisional results announced by the country's electoral commission.
"Having gained ... 38.57 percent of the vote, Felix Tshisekedi is provisionally declared the elected president of the Democratic Republic of Congo," Corneille Nangaa, the head of the Independent National Election Commission (CENI), said late on Wednesday in the capital, Kinshasa.
Nangaa said Tshisekedi had received more than seven million votes, compared to about 6.4 million for opposition candidate Martin Fayulu, who led in polling and warned against manipulation.
Long-time President Joseph Kabila's hand-picked candidate, Emmanuel Ramazani Shadary, was third with about 4.4 million votes.

The announcement came hours after riot police deployed at the commission's headquarters in Kinshasa amid fears of violence due to a disputed result.
Election observers reported a number of irregularities during the December 30 vote and the opposition alleged it was marred by fraud.
The result could lead to the country's first democratic transfer of power since independence from Belgium in 1960, with Kabila due to leave office this month after 18 years in power - and two years after the official end of his mandate.
Some observers have suggested that Kabila's government sought to make a deal as hopes faded for a win for Shadary.
The result is certain to fuel further suspicion that Tshisekedi struck a power-sharing pact with Kabila. Tshisekedi's camp has acknowledged contacts since the vote with Kabila's representatives but denies there has been any kind of deal.
Losing candidates can contest the results before the country's constitutional court. It is not immediately clear whether Fayulu will do so.
Al Jazeera's Haru Mutasa, reporting from outside the commission's headquarters, said Tshisekedi's supporters were taking to the streets to celebrate the result.
"The news came as a surprise," she said. "A lot of people who didn't have much faith in the electoral commission really thought that Shadary, who is backed by Kabila, would win."
Tshisekedi, 55, is the son of the late Etienne Tshisekedi, the face of the DRC's opposition for decades.
Aljazeera.
 
87E39A31-2C74-47F8-81B9-2AA83E2CE60D_w408_r1_s.jpg

Rais mteule Felix Tshisekedi
Shirikisha

Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia wa Congo uliokuwa una ushindani mkubwa, tume ya uchaguzi imesema Alhamisi.

Matokeo ya awali yameonyesha kuwa yeye anaongoza katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya mgombea wa upinzani Martin Fayulu, na yule wa muungano wa chama tawala Emmanuel Shadary.

Atakapo thibitishwa, Tshisekedi atakuwa mshindani mpinzani wa kwanza kushinda tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupata uhuru.

Rais Joseph Kabila anaachia madaraka baada ya miaka 18 ya uongozi wake.

Alikuwa ameahidi kuwepo kubadilishana madaraka kwa njia ya utulivu DRC tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Ubelgiji 1960.

Tanzania inahitaji tume huru
 
Ucheleweshaji wa kutangzwa kwa mshindi ndio unaleta ukakasi. Pia ndogo idadi ya wapigakura inaondoa uhalali wa ushindi.
Mwisho, mkwara wa kanisa Katolik umesaidiia sana kuondoa figisu za Tume ya uchaguzi na serikali.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom