Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,584
Opposition named winner in DR Congo poll
Mgombea urais wa upande wa upinzani huko Congo-Kinshasa, Bw. Felix Tshisekedi ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais na tume ya uchaguzi ya nchini humo, CENI.
Hii ni habari mpya kabisa kwa hiyo taarifa zaidi zitafuatia.
Ila nahisi kama chama tawala hakitokubali matokeo. Nahisi tu.
Tusubiri tuone........
=======
Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia wa Congo uliokuwa una ushindani mkubwa, tume ya uchaguzi imesema Alhamisi.
Matokeo ya awali yameonyesha kuwa yeye anaongoza katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya mgombea wa upinzani Martin Fayulu, na yule wa muungano wa chama tawala Emmanuel Shadary.
Atakapo thibitishwa, Tshisekedi atakuwa mshindani mpinzani wa kwanza kushinda tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupata uhuru.
Rais Joseph Kabila anaachia madaraka baada ya miaka 18 ya uongozi wake.
Alikuwa ameahidi kuwepo kubadilishana madaraka kwa njia ya utulivu DRC tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Ubelgiji 1960.
Chanzo: VOA Swahili
=============
Martin Fayulu, mgombea urais wa upinzani DRC aliyeibuka wa pili, ameyakataa matokeo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) yanaonesha Felix Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi mteule wa urais."
Bw Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye Bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni, huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akimaliza wa tatu akiwa na takriban kura 4.4 milioni.
Bw Fayulu ameambia Idhaa ya Kifaransa ya BBC kuwa: "Hii ni kashfa mbaya sana. Matokeo haya hayana uhusiano hata kidogo na ukweli halisi. Raia wa Congo hawataukubali utapeli kama huu daima. Felix Tshisekedi hakupata kura 7 milioni, haiwezekani. Alizitoa wapi?"
Awali, alikuwa ameambia kituo cha redio ya Radio France International (RFI) kwamba matokeo hayo ni "mapinduzi halisi kupitia uchaguzi" na akatoa wito kwa waangalizi wa uchaguzi kuchapisha matokeo waliyo nayo aliyosema ni ya kweli.
Nchini DRC hata hivyo, ni kinyume cha sheria kwa mtu mwingine kando na CENI kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mji mkuu Kinshasa, Tshisekedi amesema atakuwa "rais wa raia wote wa Congo.
Kumekuwa na tetesi kwamba kucheleweshwa kwa shughuli ya kutangaza matokeo, ambayo awali yalitarajiwa kutangazwa Jumapili, kulitoa muda kwa Rais Kabila na Bw Tshisekedi kuafikiana.
Kanisa Katoliki limesema matokeo rasmi yaliyotangazwa na tume hiyo yanakinzana na matokeo ambayo yameandaliwa na waangalizi wake.
Wamedokeza kwamba Bw Fayulu alipata kura nyingi, kwa mujibu wa takwimu walizo nazo. Baadhi ya kura za maoni zilikuwa zinamuonesha Bw Fayulu akiwa mbele ya wagombea wengine.
Msemaji wa Bw Tshisekedi Claude Lbalanky ambaye amesema siku ya leo ni "siku njema kwa taifa" ameambia BBC kwamba hakuna makubaliano yoyote kati ya Rais Kabila na Bw Tshisekedi.
Kwa taarifa zaidi, soma:
Uchaguzi DRC: Martin Fayulu apinga matokeo ya urais DRC, Felix Tshisekedi afurahia na kumtaja Kabila kuwa 'mshirika muhimu'