DR Congo: Mgombea wa upinzani, Felix Tshisekedi ashinda Urais. Mgombea mwenza apinga matokeo hayo

Hili ni fundisho kubwa sana kwa Jiwe kwa kuwa yeye anaamini kupiga kura siyo "issue" kwa kuwa yeye ndiye mwenye uwezo kwa kutumia wasimamizi wa uchaguzi na Jeshi "lake" la Polisi kwa kupindua matokeo na kuweza kuwafanya wagombea wa CCM wawe wameshinda kwa asilimia 100!
 
Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tume ya uchaguzi imesema.

Matokeo ya awali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, alisema mapema Alhamisi kwamba Bw Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi wa urais kwa muda."

Source: BBC Swahili.

MY TAKE : Licha ya figisu za serikali ya Joseph Kabila lakini wingi wa kura za upinzani zimewapa wakati mgumu Tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi wa kulazimishwa kutoka chama tawala.

CCM, Taa nyekundu inawaka.! Stay tune.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguvu ya kanisa ka roman katoliki ndiyo hii

Walisema mshindi wanamjua na kweli katangazwa

Kwa Tanzania kanisa limebaki kuchukua sadaka tu ili migogoro iliyonayo na wananchi ya upokonyaji ardhi ilindwe
Acha upuuzi RC Tanzania imepora ardhi ya Nani? Wakati kuna wilaya fulani maafisa ardhi wamepima viwanja na kuviuza ilihali eneo ni la kanisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi hamjajua kuwa huyo Tshisekedi yawezekana ameshazungumza na Kabila, na akapewa ushindi wa Martin Fayulu.
 
Back
Top Bottom