DR Congo: Makaburi 10 ya halaiki yagunduliwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasema kwamba imepata zaidi ya makaburi kumi ya pamoja katika mkoa wa Kasai, mahali ambapo vikosi vya serikali na makundi ya waasi yametuhumiwa kwa mauaji ya raia.

Mwendesha mastaka wa kijeshi Generali Joseph Ponde amesema anaamini mauaji hayo yamefanywa na sehemu waasi wa Kamuina Nsapu ambao wamekuwa wakipiga vita majeshi ya serikali.

Mnamo wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulielezea hofu yake juu ya mauaji yanayoendelea kila uchao katika mkoa huo, ambapo takriban watu elfu mbili waliangamizwa katika kipindi cha miezi mitatu.

_96693206_c6f03126-a8d8-4045-87c6-0b70c89bfadc.jpg

Umoja huo aidha ulinyooshea kidole jeshi la taifa la Kongo kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.

Hata hivyo jopo maalum la uchunguzi wa mauaji hayo iliamua kwamba hakuna uhalifu wowote wa kivitu uliyotekelezwa na kwamba hakuna mapigano yaliyotangazwa rasmi mkoani Kasai.

Inadaiwa baadhi ya wanajeshi hao walinaswa katika kanda ya video wakiwapiga risasi raia ambao hawakuwa na silaha.

Chanzo: BBC
 
Enough is Enough, Wakongo wanatakiwa wasimame pamoja, wameshachezewa vya kutosha.
Anahitajika kiongozi mwenye Hekima na unyenyekevu wa Hali ya Juu kuwaunganisha hawa watu,

Ni mataifa makubwa Duniani yakishirikiana na majirani wa Congo ambao ni Waafrica wameichezea Congo kwa Lengo la kuiba rasilimali zao.
 
Ushauri wako ungemfikia Kabila ingekua safi sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom