DR Congo kuwa na Serikali ya pamoja, viongozi kutoka meengo wa Kabila na Tshisekedi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,289
2,000
Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila wamekubaliana kuunda serikali ya muungano.

Tangazo hilo lilifanywa na wapatanishi moja kwa moja katika runinga siku ya Jumatatu usiku na kuthibitisha ripoti kutoka siku ya Ijumaa kwamba pande hizo mbili ziliafikiana.

Serikali hiyo itakua na mawaziri 66. Hao ni pamoja na waziri mkuu Sylvestre Ilinkumba ambaye alichaguliwa na bwana Kabila.

Mawaziri 42 watatoka katika chama cha kabila huku 23 wakitoka katika muungano wa bwana Tshisekedi.

Majina ya watakaoshikilia nyadhfa hizo bado hayajatolewa.

Hatua hiyo inajiri miezi saba baada ya muungano wa bwana Tshisekedi kwa jina CACH kushinda uchaguzi huo.

Maswali yaliulizwa wakati huo kuhusu matokeo hayo huku kukiwa na madai kwamba bwana Tshisekedi alifanya makubaliano ya kugawana mamlaka na bwana Kabila kabla ya uchaguzi huo.

Duru zinaelezea kwamba huenda Rais Tshisekedi atamteua waziri wa mambo ya ndani, waziri wa mambo ya nje, yule wa bajeti na uchumi na gavana wa benki kuu, huku Joseph Kabila akiteua waziri mkuu, wizara ya ulinzi, sheria, fedha na akiba.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,198
2,000
Waziri Mkuu, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa fedha wote wa Kabila, jamaa sidhani kama anaheshimiwa kama Raisi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom