DR Congo: Ebola yaibuka tena Mashariki mwa nchi hiyo katika maeneo ya Beni

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imetangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo mapya.

Hali ya wasiwasi imetanda katika maeneo mengi ya mashariki mwa Congo,baada y'a wizara ya afya kutangaza kugundulika kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo ya Beni mashariki mwa nchi hio. Serekali ya Kongo imetangaza hayo wiki moja tu baada ya shirika la afya duniani WHO na mamlaka za DRC kutangaza mafanikio na mwisho wa janga hilo la Ebola katika jimbo la Ecuador.

Wizara ya afya ya Nchini Kongo imetoa taarifa kwa shirika la afya duniani WHO kuwa, vipimo 4 kati ya 6, vimekutwa na virusi vya ugonjwa huko Kinshasa, bado vipimo vingine vinaendelea.

Mkurugenzi wa WHO Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa, ebola ni tishio kubwa nchini DRC, lakini uwazi na ukweli wa serikali ya Kongo katika kutoa taarifa za ugonjwa huo, ndio njia ya kwanza ya kuweza kufanikisha mapambano ya kumaliza Ebola DRC.

Mkurugenzi wa WHO kwa upande wa Afrika amesema ni rahisi kuanza mara moja jitihada za kuzuia Ebola kwasababu wametoka kupambana na tatizo hilo hilo, hivyo vifaa na wafanyakazi wako tayari.

Maambukizi makubwa yameonekana katika eneo la Mangina ambapo ni kilomita 30 tu kutoka mji wa Beni.
ebola_3359523b.jpg
 
Serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imetangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo mapya.

Hali ya wasiwasi imetanda katika maeneo mengi ya mashariki mwa Congo,baada y'a wizara ya afya kutangaza kugundulika kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo ya Beni mashariki mwa nchi hio. Serekali ya Kongo imetangaza hayo wiki moja tu baada ya shirika la afya duniani WHO na mamlaka za DRC kutangaza mafanikio na mwisho wa janga hilo la Ebola katika jimbo la Ecuador.

Wizara ya afya ya Nchini Kongo imetoa taarifa kwa shirika la afya duniani WHO kuwa, vipimo 4 kati ya 6, vimekutwa na virusi vya ugonjwa huko Kinshasa, bado vipimo vingine vinaendelea.

Mkurugenzi wa WHO Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa, ebola ni tishio kubwa nchini DRC, lakini uwazi na ukweli wa serikali ya Kongo katika kutoa taarifa za ugonjwa huo, ndio njia ya kwanza ya kuweza kufanikisha mapambano ya kumaliza Ebola DRC.

Mkurugenzi wa WHO kwa upande wa Afrika amesema ni rahisi kuanza mara moja jitihada za kuzuia Ebola kwasababu wametoka kupambana na tatizo hilo hilo, hivyo vifaa na wafanyakazi wako tayari.

Maambukizi makubwa yameonekana katika eneo la Mangina ambapo ni kilomita 30 tu kutoka mji wa Beni.View attachment 824776
Hao wananchi mbona wamesogea karibu sana na hao wahudumu wa afya? Hakuna athari yoyote kwao hapo?
 
Hakuna cha wazungu wala nini hapa dawa ni wakongo wakatazwe kula nyama ya nyani.
Huo mji wa Beni nimewahi fika ulikua maarufu sana kwa kilimo cha kahawa wakati huo na una misitu minene ingawa umasikini umetamalaki sana kwa watu wake. Ni sehemu ya DRC wanayoongea kiswahili kama lugha ya kwanza.

Watu wake ni wakarimu sana ingawa kwa asili Wakongomani ni wanafiki sana na sio watu wa kufanya nao biashara maana kukurusha na kisha kukuroga kwao ni kawaida
 
Back
Top Bottom