Dr.Bilali atengewa bil 4 kwa matumizi ya kawaida, bil 32 kwa maendeleo ya Zanzibar!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.Bilali atengewa bil 4 kwa matumizi ya kawaida, bil 32 kwa maendeleo ya Zanzibar!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Jul 7, 2012.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..jamani tukisema Zanzibar wanatunyonya Tanganyika mnadai tunachonga sana.

  ..lakini kuna bil 4 zimetengwa kwa ajili ya Makamu wa Raisi, wanasema kwa matumizi "yake" ya kawaida.

  ..huyu ndiye makamu wa Raisi ambaye muda mfupi baada ya kula kiapo, aliamua kwenda likizo na familia yake kutembelea mbuga za wanyama, badala ya kuwatumikia wananchi.

  ..halafu kuna bilioni 32 kwa ajili ya maendeleo ya wa-Zanzibari. Je, fedha kiasi gani zimetengwa na ofisi ya makamu wa raisi kwa ajili ya maendeleo ya wa-Tanganyika??

  ..mwisho, hii ofisi ndiyo inayoshughulikia kero za muungano, lakini makamu wa raisi, na waziri mwenye dhamana ya muungano wote ni wa-Zanzibari. yaani ktk suala la kero za muungano wanakaa wa-Zanzibari wawili na kufanya maamuzi wenyewe.

   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Madaktari,walimu,wakulima,mama wa nyumbani woote gomeni
   
 3. w

  wikolo JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimesoma uzi wako na mawazo yangu yakaelekea kwenye hotuba ya Lissu aliyoitoa bungeni wiki hii. Kazi ipo.
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwani kero za Muungano ni kwa wazanzibari tu? Sisi waTanganyika hakuna kero za muungano zinazotusibu?
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,062
  Likes Received: 6,515
  Trophy Points: 280
  Huyu kaka ni mtu mzima sana kwani kupumzika anaona nini wakuu.
   
 6. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,803
  Likes Received: 2,576
  Trophy Points: 280
  Oh me what wretched errors has my heart commited when i thought myself so blessed never. So i return rebuked to my content and gain by ills three times what i have spent. End of storo.
   
 7. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45

  hakuna kunyonya hapa tunachukua kilicho chetu katika muungano tatizo lenu watanganyika hamjui lipi la muungano lipi si la muungano na kwa ujinga wenu kuingiza yenu yote katika muungano, madhali mmeingiza yote katika muungano yote yetu sote, hapa tunachukua chetu sawa? hamtaki rudisheni Tanganyika yenu? tuanze upya na madeni yote ya kwenu maana nyie ndio mlio kopo kwa wazungu sisi tulisimama kwa miguu yetu muda wote.

  tutabakiza muungano kwa kuwa tumezaa na dada zenu la sivyo mikufutuka kurudusha Tanganyika tungesema basi, nahata hivyo tuone hiyo MoU ya kurudishwa tanganyika maana tuna turufu siku hizi kama haina maslhi na sisi tanganyika hairudi, unabisha jaribuni kulianzisha mtaona nini tutawalipa, nyie hamna ujanja kwetu sisi ndio tuna mpini kwenye muungano maana hatukuingia kichwa kichwa na hatuwahitaji, nini nyinyi ndio mnatuhitaji sisi ndio mmekuwa ng'ang'anizi kama dada powa.
   
 8. d

  dguyana JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM=Chukua Chako Mapema
   
 9. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  mwenzako wanamwandaa kwa 2015
   
 10. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Una mawazo mfu sana,uwe unajaribu kushughulisha ubongo wako
   
 11. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dah!! nimepata kigugumizi ghafla!.
   
 12. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  Kama sikosei hesabu Bilion 1 ina milion 1000 hivyo bilioni 4 ni sawa na milioni 4000. Mwaka huwa na siku 365, ukuchukua milioni 4000 ukagawa kwa siku 365 unapata millioni 11 kwa siku. Je makamu wa rais anamatumizi gani haya yakawaida ya kughalimu nchi 11 kwa siku? Tafakari chukua hatua
   
 13. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hapa sioni cha kushangaza...ni kwamba,huu ndo utekelezaji wa ilani ya ccm! Hivyo ndo vipaumbele...!
   
 14. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kweli kama alivyoandoka mzenji hapo juu ninaungana nae kuwa wanaochangia hii mada hawajui wanachangia nini mradi tu anazungumza sias alafu kingine ni utoto mtupu. Pia mtoa mada namlaani kwa kupotosha umma. Bajeti ni ya ofisi ya makamu wa rais na siyo ya kwake ya mfukoni jamani. Ofisi ya rais ina ofisi yake kama makamu wa rais, waziri wa mazngira na waziri wa muungano. Fedha za matumizi ya kawaida hata kambi ya upinzani kupitia Mchungaji Mh. J. Msigwa ilieleza wazi inatumikaje. Fedha za maswala ya muungano ni fungu lao maana yapo mengi tunayoshirikiana na kwa maoni yangu hizo ni ndogo sana.

  Mwisho namsihi mtoa mada aache tabia mbaya ya uchochezi kwa kucheza na akili za watu. Sema fedha kiasi fulani kimetengwa kwaajili ya ofisi au wizara fulani na siyo kwaajili ya mtu fulani.

  Tuache kubwata kwwa kutumia hisia tutatue matatizo yetu kwa tafakuri na matengo yenye malengo na utaratibu sahihi.
   
 15. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  udhaifu bin udhaifu
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  Mabulangati,

  ..habari hii nimeitoa kwenye gazeti la mwananchi.

  ..wanaripoti kwamba bilioni 4 zimetengwa kwa matumizi "yake" ya kawaida.

  ..wananchi tunapenda kujua ni matumizi gani hayo? hata in the best case scenario ambapo matumizi hayo ni ya wizara, na si 'matumizi "yake" ya kawaida,' that is 11 million a day. yaani hata siku za mapumziko Ofisi ya VP, au huenda Bilali mwenyewe wanatugharimu wa-Tanganyika bilioni 11? Hivi Zanzibar wanachangia kiasi gani?

  ..Pia Ofisi ya makamu wa Raisi imeomba, au imetenga bilion 32 kwa maendeleo ya Zanzibar. je ni kiasi gani kimetengwa na ofisi hiyo kwa maendeleo ya Tanganyika?? au makamu wa raisi ameona sisi wa-Tanganyika hatuhitaji maendeleo??

  ..mwisho, kwanini portfolio ya muungano imepewa waziri mzanzibari, wakati tayari makamu wa raisi anatoka zanzibar? katika mazingira hayo ni nani atatutetea wa-Tanganyika?

  ..muungano huu unatunyonya wa-Tanganyika, imefika wakati tuachane nao.

  ..LET ZANZIBAR GO!!!
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Office ya Makamu wa rais ndiyo inahusika na mambo ya muungano, ningetaka kujua ni mambo gani hasa ya muungano? What exactly kinafanywa na hii office, na muhimu zaidi, Tanganyika inachangia kiasi gani na Zanzibar nayo inachangia kiasi gani kuendesha hii ofiice ya Muungano?

  LET ZANZIBAR GO!!!
   
 18. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hapa sioni cha kushangaza...ni kwamba,huu ndo utekelezaji wa ilani ya ccm! Hivyo ndo vipaumbele...!
   
 19. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,341
  Trophy Points: 280
  Mkuu Joka Kuu ukisoma watu kama hawa unaweza kujua tumeungana na watu wa aina gani.
  Mtumbatu kwa taarifa naona wewe ni mgeni hapa jamvini lakini tutakupa elimu ili ukirudi Mzalendo.net uwaeleze.

  Tumesahasema Tanganyika ikirudi pesa za bure kama hizo bilioni 32 hazitapatikana. Unaposema unachukua chako ni kipi hicho maana unachangia sifuri (zero) sasa unachukua kipi ? Lakini si hicho tu, mishahara ya Wabunge, Wawakilishi na Viongozi wote inatoka hazina Dar es Salaam, kwahiyo mnachukua cha kutosha na zaidi wala si chenu.

  Unajua Zanzibar ni nchi isiyo na jeshi wala polisi. Sasa unaposema Tanganyika inawahitaji, ni kwa lipi? Si unajaua Rais anachaguliwa Dodoma, na anapelelekwa na Polisi na kulindwa na jeshi lisilo za Znz, sasa mpini upi mumekamata.
  Salimin Amour alijaribu, baada ya hapo imebaki hadithi na tunasikia akienda India tu! Muulize Raza ilikuwaje!

  Anyway, Mkuu Joka kuu ukisoma Raia mwema utakutana na habari ya yule msemaji wa Wapemba na Sultani, Ahmed Rajabu. Anasema ZNZ sasa inajua haki na inadai haki. Haki ni hii ya kupewa mishahara watu wakicheza bao, haki ni hii ya kuwasha umeme wasiolipia, haki ni hii ya kupewa bilioni zisizojulikana ni za nini?

  Ukimsoma huyu bwana Mtumbatu, halafu uksaoma maoni ya Ahmed Rajabu utajua MZNZ ni mtu wa aina na kiwango gani.

  Haya yapo mwisho, Hotuba ya Tundu Lissu imeeleza vizuri tu, sisi tuna kazi moja tu, kuuleza umma kuwa hatuna sababu za kuwa na ZNZ, hatufaidi chochote wala lolote, sasa ni wakati wa kusema LET ZNZ GO!

  Akina Lisu wametusikia na wanatuelewa, najua Nape na akina Kigwangalla wote wataona udhalimu huu, nao uzalendo wa nchi yao utasimama. Bila kufanya jambo hawa WZNZ wataomba tuwapeleke makopo ya maji uani!

  Hakuna Mkataba
  Hakuna serikali 3

  Tukautane EAC, LET ZNZ GO!
   
 20. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mimi sielewi kinachowafanya hawa watawala waung'ang'anie huu muungano ambao unaligharimu taifa mambo mengi tu.
   
Loading...