Dr. Bilal kasahau yeye ni Makamu wa Rais wa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Bilal kasahau yeye ni Makamu wa Rais wa Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mozze, Feb 17, 2011.

 1. m

  mozze Senior Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa najiuliza huyu jamaa anapoalikwa kuwakilisha serekali kwenye sherehe za Kiislam anasahau kuwa yeye ni kiongozi wa watu wote? Huwa anatoa hotuba zake utafikiri yuko Zanzibar au anaongoza nchi ya Kiislam.

  Nimesoma kwenye The Citizen nikaona ni vyama niweke hapa ili atakayeweza amfikishie ujumbe kuwa yeye anawakilisha watu wote, na sio kuongea kama yeye ndie shehe mkuu.

  Quote from the newspaper:
  Meanwhile, presiding on Maulid celebrations on Tuesday night, the Vice President, Dr Mohammed Gharib Bilal, called for unity among Muslims in the country.He urged them to emulate the life of Prophet Mohammed SAW whose teachings direct them to be loyal and love one another
  .............

  He reminded them that the solution to such problems lies with cooperation among them, cherishing peace, harmony and unity. He warned that there was no peace in an area where people do not respect each other.

  “In such a big gathering I see it fit for me to insist on the need to embrace unity and love among ourselves. God will not bless us if we live in enmity,” he stressed.........#. .... Je hapa ana maana Waislamu wasiungane na dini nyingine? Hii inadhihirisha kuwa wale mashehe wanaotetea maovu ya serekali wanafuata wito huu.

  He urged them to improve their relationship with people of other religious beliefs.“When you debate with them, please do so amicably as we have been directed by the Almighty,” he said....... so haongelei waislamukushirikiana na dini nyingine bali anawaasa wawe na mawasiliano mzuri tu ........

  Huu ni mtazamo wangu tu.... ni vizuri kuwakumbusha hawa viongozi wetu
   
 2. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45

  Hapa Bilal Mkuu yuko sahihi,sherehe hiyo haikuwa ya chama ni ya dini na tena kiislam.Yeye kaalikwa kidini na wala si kisiasa na si kosa ku -quote maandiko.Alikuwa anawasilisha hotuba yake kwa hadhira iliyokuwepo na hapa "fanani" ni waislaam ambao ndio walengwa.Haya mbona yanaeleweka na ndio maana kuna madhehebu.Dhana ya kupendana ni ya kiimani zaidi na hapa imani iliyopo ni ya kiislam na ndio maana kaanza na Waislam na baadae kuwaunganisha na watu wa madhehebu Mengine.Hivyo hakuna kosa Mkuu.
   
 3. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sijaona tatizo kwenye hotuba yake! kumbuka alikuwa kwenye sherehe y waislam si sherehe ya kitaifa lazima atoe nasaha sinazofanana na waliopo pale! kumbuka katika maelezo aliyotoa [kama nlivyoyasoma kwenye thread yako] hakuna sehemu anaposema Serikali yaani hatambulishi kuwa huo ujumbe anaotoa ni ujumbe wa Serikali ya Jamhuri! UNLESS IF I MISUNDERSTOOD SOMETHING THERE!
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,172
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Nadhani lugha ya kwa Malkia imeleta shida tu, Dr wa watu yuko sahihi.
   
 5. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWACHENI BILAL AMWAGE SUMU JAMANI SISI YETU MACHO.....TUMJUE :sad:
   
 6. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 80
  Im feel sorry for you mozze. you distort and fabricate everything inoder to give way your corrupted illusion.....move on
   
 7. v

  vickitah Senior Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwenye hili nakubaliana na wewe mi pia sijaona tatizo kwenye hiyo hotuba especially pale aliposisitiza relationship with people of other religious beliefs!!
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Itafute ya mwinyi pale chuo cha Agha Khan walipohitimu ndo utashangaa misimo ya watawala wetu!
   
 9. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  OFCOURSE KAULI KAMA HIZO HAZIFAI KUTAMKWA NA KIONGOZI MZALENDO. and viseversa
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,946
  Trophy Points: 280
  elizabetian english
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jamani tusijichanganye, Hapa Prof anahimiza upendo, ushirikiano NK, lazima tujue kwamba hata katika uislamu kuna madhehebu, kuna tofauti za misimamo, sasa tulitegemea aseme nini. Nadhani tusipende kutafsiri mambo vibaya kuchochea udini.
  Hapa mimi naona alikuwa sawa tu. Na alizungumza kama Makamu wa Raisi, aliyeandaa hotuba yake vizuri.:bump:
   
 12. D

  Dar Es Salaam. Member

  #12
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Naomba tumsamehe tu Mheshimiwa Balal, kwani kilichotokea hapo kinatupa mwanya wa kuona mengi.

  Hata kama alialikwa pale kama muumini wa kawaida, bado yeye anamwakilisha Rais wa jamhuri ya muungano wa watanzania na watanzania woote kwa ujumla. Hayo majukumu hawezi kuyavua eti kwa kuwa hiyo haikuwa shughuli ya kiserikali. Mara nyingi kwenye shughuli za kidini anapoalikwa mtu toka serikalini, si kwa ajili ya udini wake, ila ni kwa ajili ya kuonyesha mshikamano na umoja kwa watanzania woote bila kujali dini zao. Ndo maana Rais wa jamhuri huwa anaalikwa katika shughuli za kikristu, ingawa yeye ni kidini siyo mkristu. Na katika mialiko hiyo, yeye kama kiongozi wa kiserikali, hana haja kuzungumzia mambo ya dini yake, bali mambo yenye manufaa kwa serikali na watanzania wote kiujumla.

  Ingawa sijaona ubaya wa kauli aliyotoa mheshimiwa Makamu wa Rais, ila ninakubaliana na mtoa hoja kwamba ameshindwa kusimama kama Kiongozi wa serikali katika shughuli hiyo ya kidini. Asisahau kwamba yeye ni mwakilishi wa watanzania woote, hadi siku atakayoamua kutupa ushindi wetu walioupata kutokana na matunda ya uchakachuaji.

  Inawezekana kabisa kwamba tunachokiona hapa ni ukweli kwamba hawa viongozi wanasutwa na nafsi zao. Kwamba ingawa wamejivisha kofia za uongozi, lakini kwenye nafsi zao wanajua kabisa ni nani anayestahili kuwa kiongozi. Ndiyo maana wanajisahau katika shughuli kama hizi kuwakilisha wananchi woote; Mfano mwingine wa hali kama hii ni ukimwa wa Rais kwenye mauaji ya Arusha na suala la Dowans.
  Ukiangalia kwa makini unaona kwamba hii nchi inaongozwa na vyama vya upinzani na bunge ndo maana hata maswala ya ufuatiliaji wa sheria, mikataba tata, utatuaji wa tatizo la umeme n.k yanarudishwa bungeni baada ya serikali kuleta utata au kushindwa kuyatatua. Kwa maana nyingine, serikali tunayoifahamu ni "kivuli" na serikali kamili iko bungeni. It is sad, but true.

  Ukiangalia yoote hayo, hautakuwa na ugumu kumsamehe Mheshimiwa makamu wa Rais. Tuombe Mungu serikalini wazidi kulala, ili upinzani uongoze nchi kwa kupitia Bunge, kwani tukitegemea hekima ya "Chama Cha Majambazi" kutuwakilisha tutazidi kudidimia.
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hivi Dar Es salam aka zomba si amepigwa ban ... huyu ni DSM gani..? harooo ..jitambulishe hapo ulipo
   
 14. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  <br />
  <br />
  Siasa za majitaka zimekula kichwa chako,yaani hata kwenye hoja tofauti unapachika upuuzi.Acha ujinga wewe,jadili kilichopo na usichanganye mambo huko unapopataka patafika tu na ole wako usipige kura.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Quote from the newspaper:
  Meanwhile, presiding on Maulid celebrations on Tuesday night, the Vice President, Dr Mohammed Gharib Bilal, called for unity among Muslims in the country.He urged them to emulate the life of Prophet Mohammed SAW whose teachings direct them to be loyal and love one another
  .............

  He reminded them that the solution to such problems lies with cooperation among them, cherishing peace, harmony and unity. [/QUOTE]

  Kwa mtazamo wangu hapa Makamu Wa Rais Bilari hajaongea kama kiongozi mwenye mtazamo wa umoja wa kitaifa ila kama kiongozi mtetezi wa maslahi ya dini yake na waumini wake.
  Kiongozi wa kisiasa mwenye mtazamo mapana angeongea kwa mtazamo mpana zaidi kisiasa, lakini hapa nasita kusema amesema kuhusu umoja wa kitaifa bali umoja wa kiislamu.
  Tujue huyu ni mara ya kwanza kuja kushika wadhifa katika Jamhuri ya Muungano, anafikiria bado yuko Zanzibar.
  Wanasiasa wenzake wampe msasa kidogo vinginevyo ataendelea kuharibu.
   
 16. D

  Dar Es Salaam. Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5

  Hapana ndugu yangu, mimi siyo "Zombe" wala simfahamu huyu mtu. Labda ungenisaidia kufahamu ni utambulisho gani unaouhitaji, ningeweza kukusaidia. Ila kwa mtazamo wangu, naona cha umuhimu hapa ni hoja zetu, bila ya kujali ni nani aliyetoa hoja hizo.
   
 17. D

  Dar Es Salaam. Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Samahani ndugu yangu kama nimekukwanza na hoja yangu. Naomba ufahamu kuwa hiyo haikuwa ni nia yangu. Pamoja na hayo sidhani kama nilichoandika ni "upuuzi" au matokeo ya siasa taka kama ulivyoainisha. Hata kama hilo ni kweli, basi nielimishe kwani hizi lugha za maneno makali kama haya hazitatupeleka popote zaidi ya kujenga tu chuki kati yetu.

  Nilichoandika ni mtazamo wangu, na nimejaribu kuoanisha hali ilivyo sasa, tabia za viongozi na chimbuko lao. Sasa kama kufanya hivyo ni "upuuzi" labda nisaidie nifanyeje kuepuka kuleta huo "upuuzi" hapa jamvini.
   
 18. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wakiristo bwana inawachoma, sasa ulitaka aongee nini ? yule alikuwa kwenye shughuli ya kiisilamu na sio ya kitanzania, maana ukiwa na waisilamu ongea kuhusu uisilamu. sasa vipi munataka aongelee masuala ya ushirikiano na wakiristo wakati wakiristo hawana ushirikiano na waisilamu kila siku wanawapinga waisilamu wanapohitaji mambo yao kama mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC halafu eti munataka aongelee ushirikiano ushirikaiano gani huo big up Dr Bilal
   
 19. m

  mozze Senior Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio kuhudhuria au kuwa muislamu, tatizo ni uwakilishi wake. Yeye ameenda kwenye ile sherehe, japo ni muislamu, lakini kuwakilisha serekali. Hivyo hotuba yake haitakiwi kuwa hotuba ya kuleta ubaguzi..... He reminded them that the solution to such problems lies with cooperation among them, badala ya kuonyesha umuhimu wa waislamu kushirikiana na kusaidiana na jamii nzima nadhani sio sahihi...... yeye angekuwa amehudhuria ile sherehe kama Sheikh nadhani isingekuwa na shida...lakini kiongozi wa nchi anapossema kama yeye ni mmoja wa hilo kundi, anatumia "tushirikiane kama waislamu" hapo anaonyesha kabisa mtazamo wake kwa dini na makundi mengine ya jamii...na mimi naona hizi ni chembe za ubaguzi.
   
 20. m

  mozze Senior Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "In such a big gathering I see it fit for me to insist on the need to embrace unity and love among ourselves. God will not bless us if we live in enmity," he stressed.........
  je hapa anaongelea ushirikiano na makundi mengine ya jamii au ushikiriano kati ya waislamu.....

  wewe kama kiongozi wa nchi ukisema kundi fulani liongeze umoja, una maana lijitenge na kundi lingine....angesema waislamu wahakikishe umoja na upenda na watu wa dini nyingine angeweza kueleweka......lakini lugha aliyotumia inaweka sumu kwenye jamii.....huu ni mtazamo wangu....... mana kesho na kiongozi wa kikristo akiwaambia wakristu wahakikishe ushirikiano baina yao then hapo tutakuwa na makundi mawili yasioyoshirikiana.....na tuomeona hili wakati wa issue ya Arusha.... Baadhi ya maaskofu walitoka na kukaripia, wale wa upande wa pili (waislamu) wakatoka na kuwakaripia Maaskofu na walisema clear kuwa maaskofu wanapinga serikali kwa sababu Rais ni Muislam...... Ndio mana mimi nimeona Dr. Bilal amekosea kuwakilisha serekali kama vile Sheikh!
   
Loading...