Dr Benson Banna: Kweli CHADEMA sasa inakubalika sana...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
Yule msomi na kiongozi wa REDET toka chuo kikuu cha DSM Dr Benson Banna hatimaye amekiri wazi kuwa CHADEMA sasa inakubalika.

Tofauti na kawaida ya Dr Banna kuonekana mara nyingi kulalia upande mmoja hasa wa CCM jana akiteta ofisini kwake, Dr Banna alisema wazi kwa mwenendo unavyoonekana na namna chama hiki kinavyoendelea kushika kasi kuna uwezekano mkubwa wa CHADEMA kushika dolla katika uchaguzi wa 2015.

Kama kitashikilia uzi na kuendelea kupambana kujenga mizizi hasa vijijini...
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
7,427
7,065
Aseme au asiseme hiki kitu ni hakika na kweli, na wala haihitaji msomi mwenye PhD kuweza kulitambua hili. Nadhani kwa sababu ya ushabiki wake kwa CCM alichelewa sana kuliona hili. Hakutakiwa kusubiri Igunga ndo apate uhakika sisi tusiokuwa na PhD tulishaliona hili siku nyingi kwa hiyo anachojaribu kukieleza leo kwenu ni kama marudio masikioni mwetu.

Labda asububiri kikao cha NEC ya CCM akawaeleze hayo.
 
Shalom

JF-Expert Member
Jun 17, 2007
1,315
111
Huyu coward wa CCM aseme nini sasa! anajua walichokifanya na anawasisi na what next kwa hiyo inamlazimu atafute neno la kupoza tu. Mwizi ndiyo huwa anakuwa wa kwanza kukuhurumia.
 
GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,319
305
Yule msomi na kiongozi wa REDET toka chuo kikuu cha DSM Dr Benson Banna hatimaye amekiri wazi kuwa CHADEMA sasa inakubalika,tofauti na kawaida ya Dr Banna kuonekana mara nyingi kulalia upande mmoja hasa wa CCM jana akiteta ofisini kwake,Dr Banna alisema wazi kwa mwenendo unavyoonekana na namna chama hiki kinavyoendelea kushika kasi kuna uwezekano mkubwa wa CHADEMA kushika dolla katika uchaguzi wa 2015,kama kitashikilia uzi na kuendelea kupambana kujenga mizizi hasa vijijini...

Mwanzo thread nyingi zilikuwa za tathmini ya Igunga kuwa chadema itashinda 74% , sijui 55% nk ila hivi sasa sizioni tena hizo takwimu , vp mkuu tathmini yenu imeishia wapi ?
 
GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,319
305
Aseme au asiseme hiki kitu ni hakika na kweli, na wala haihitaji msomi mwenye PhD kuweza kulitambua hili. Nadhani kwa sababu ya ushabiki wake kwa CCM alichelewa sana kuliona hili. Hakutakiwa kusubiri Igunga ndo apate uhakika sisi tusiokuwa na PhD tulishaliona hili siku nyingi kwa hiyo anachojaribu kukieleza leo kwenu ni kama marudio masikioni mwetu.

Labda asububiri kikao cha NEC ya CCM akawaeleze hayo.

Kushindwa nikushindwa tu hayo yote ni maneno yakujifariji , nia na madhumuni ilikuwa nikushinda uchaguzi, huu haukuwa uchaguzi wa kutafuta popularity ulikuwa ni uchaguzi wakutafute mwakilishi wa wananchi, sasa hayo maneno inakubalika sijui nn ni kama marehemu amekufa then unaanza kusema alikuwa mtu maarufu sana nk haimsaidii wakati huo
 
Parachichi

JF-Expert Member
Jul 22, 2008
511
98
Mwenyewe nimeisikia hiyo kwenye kipindi cha magazeti,nimeshangazwa nai Benson Bana yule yule au mwingine!ipo siku hata NAPE atakubaliana na ukweli!let us wait & see!
 
Godlisten Masawe

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
738
281
Yeye ndo anagundua leo hili, sisi tusiokuwa na PHD tumeligundua hili miaka mingi iliyopita. Kamanda Mbowe na Makamanda wote nchini hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,944
Mwanzo thread nyingi zilikuwa za tathmini ya Igunga kuwa chadema itashinda 74% , sijui 55% nk ila hivi sasa sizioni tena hizo takwimu , vp mkuu tathmini yenu imeishia wapi ?

Tumia akili kidogo, uchaguzi umekwisha hapa ni tathmini baada ya uchaguzi.
 
HAKI bin AMANI

Senior Member
Sep 5, 2011
156
34
Mwanzo thread nyingi zilikuwa za tathmini ya Igunga kuwa chadema itashinda 74% , sijui 55% nk ila hivi sasa sizioni tena hizo takwimu , vp mkuu tathmini yenu imeishia wapi ?

Unapoingia mashindanoni kusudi kubwa ni kushinda; kushindwa ni sehemu ya matokeo. Mbona CCM uchaguzi mkuu 2010 walidai watashinda kwa kishindo lakini wakapata matokeo ambayo hawakutegemea. Kumbe nyani haoni kundule. Thread iliyopo hapa ni kauli ya 'Bunsen Burner' ambaye tunamfahamu kuwa ni mnajimu wa CCM, leo hii utabiri wake upepo umegeuka. Thanks Banna ingawa kwa Dr. kama wewe is too late kwani vipofu walikwishaona, viziwi walikwishasikia, viwete walishatembea wakafika kabla yako.
 
Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,962
1,687
Mpaka naye Nape aje atoe majibu kama hayo na kuomba tiketi kuvaa magwanda.
Mkuu umesahau kuwa nnauye jr alishataka kuvaa magwanda pale ubungo akatoswa?Hizi kelele zote ni hasira tu za kukataliwa.Baada ya kuona ugumu yeye na wanafiki wenzeke wakataka kuasisi CCJ wakasalitiana dk za mwisho.
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,974
1,640
Huyu Dr Burner (Bana) huwa simuelewi kabisa, huenda amesomea mwezini huyu
 
Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
522
Mwanzo thread nyingi zilikuwa za tathmini ya Igunga kuwa chadema itashinda 74% , sijui 55% nk ila hivi sasa sizioni tena hizo takwimu , vp mkuu tathmini yenu imeishia wapi ?

Mkuu, Nape ameshatoa majibu kuwa wapiga kura wengi (kama 120,000) hawakujitokeza kupiga kura kwa kuwa waliogopa kumwagiwa tindikali.

Sasa hizo asilimia 74 sijui 55 zingefikiwaje?
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,893
7,196
Mwanzo thread nyingi zilikuwa za tathmini ya Igunga kuwa chadema itashinda 74% , sijui 55% nk ila hivi sasa sizioni tena hizo takwimu , vp mkuu tathmini yenu imeishia wapi ?
Sasa hivi tunatafuta takwimu za fedha za Serikali zinapokwenda mpaka inashindwa kununua madawati.
2wqy4jl.jpg
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom