Dr. Benson Bana: Rais alishauriwa vibaya kuhusu waliogushi vyeti

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,859
19,726
Mhadhiri huyo maarufu na mkereketwa wa chama cha kijani ameyazungumza haya maneno akiwa anahojiwa na kipindi cha mizani ya week Azam two television .Aliongeza na kwenda mbali zaidi kwa kushauri kungekua na utaratibu mwingine wa kulishugulikia suala la kughushi vyeti aidha kwa kupewa muda wakutimiza sifa zinazohijika au vinginevyo na sio adhabu kali waliyopewa
Akiwa anazungumza kwa mifano na masikitiko alinukuliwa kuwa kuna daktari mmoja anayemfahamu alisoma clinical officer kwa kughushi cheti cha form four lakini ni daktari mbobezi tu ameokoa na anatibu watu wengi tu ila yumo kwenye list ,tutafute njia au namna nyingine ya kuwapima watu ,mtu kama dereva unahitajia nini elimu ya form four?ikiwa kusoma na kuandika na kuzielewa alama za barabani anaweza"?alihoji

"Alienda mbali zaidi na kusema unaweza ukakuta hawa baadhi ya watumishi walioghushi kwenye appraisal za kila mwaka kwa mujibu wa taratibu za serikali walikua wanapata daraja la kwanza"
Hakusita kutoa la moyoni kuwa hakubaliani kuwa suala walilolifanya ni jinai ,pia alilaumu kwanini uhakiki uishie kwa watumishi wa kawaida tu bila wakuu wa wilaya ,mikoa,wabunge na madiwani

Hakusita pia kui kosoa report ya ukaguzi wa vyeti kwa kuuliza idadi ya watu 1500 ambao vyeti vyao vinafanana ,ufanano wake upo kwenye credits,majina au shule na vyuo?hii report haijakaa sawa alikazia"

Mwisho kabisa aliishauri serikali ifanyie reform utumishi wa umma

My take:Mkuu mfikirie Bana sijatarajia alivyoonyesha criticism za wazi wazi amekitetea sana chama tena kwa ukihiyo wa kiwango cha lami na kuisahau PHD yake ,matumaini ya cheo yameanza kupotea na watetezi wako wanapungua kwa kasi ya ajabu huku nyikani
 
Mhadhiri huyo maarufu na mkereketwa wa chama cha kijani ameyazungumza haya maneno akiwa anahojiwa na kipindi cha mizani ya week Azam two television .Aliongeza na kwenda mbali zaidi kwa kushauri kungekua na utaratibu mwingine wa kulishugulikia suala la kughushi vyeti aidha kwa kupewa muda au vinginevyo na sio adhabu kali waliyopewa
Akiwa anazungumza kwa mifano na masikitiko alinukuliwa kuwa kuna daktari mmoja anayemfahamu alisoma clinical officer kwa kughushi cheti cha form four lakini ni daktari nzuri tu ila yumo kwenye list
"Alienda mbali zaidi na kusema unaweza ukakuta hawa baadhi ya watumishi walioghushi kwenye appraisal za kila mwaka kwa mujibu wa serikali walipata daraja la kwanza"
Hakusita kutoa la moyoni kuwa hakubaliani kuwa suala walilolifanya ni jinai ,pia alilaumu kwanini uhakiki uishie kwa watumishi wa kawaida tu bila wakuu wa wilaya ,mikoa,wabunge na madiwani
Mwisho kabisa aliishauri serikali ifanyie reform utumishi wa umma

My take:Mkuu mfikirie Bana sijatarajia alivyoonyesha criticism za wazi wazi amekitetea sana chama tena kwa ukihiyo wa kiwango cha lami na kuisahau PHD yake ,matumaini ya cheo yameanza kupotea
juzi wakati anafundisha yombo2 ndo nilichoka kabisa alivyokuwa anamtetea bashite
na kauli yake kubwa "you cant question the power of president"
[HASHTAG]#anaijua[/HASHTAG] public administration vilivyo bt ukada unamfanya afundishe kukitetea chama!
 
Juzi tarehe 27 Aprili 2017, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) . Angela Kairuki alikabidhi rasmi Ripoti ya Uhakiki wa Vyeti ambapo iliripotiwa kuwa jumla ya watumishi 9932 wanatumia vyeti feki.
Chama cha ACT Wazalendo kinaunga mkono uamuzi wa serikali kuwachukulia hatua watumishi wote wa umma waliobainika kutumia vyeti feki ikiwemo kuwafukuza kazi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Bila shaka hatua hii itapanda mbegu ya uwajibikaji, kuchochea uadilifu na kuhakikisha uweledi kwenye utumishi wa umma.
Mbali na kupongeza, yapo masuala kadhaa yaliyoibuka kwenye zoezi hilo ambayo tunaamini hayakwenda sawasawa na hivyo basi sisi kwa nafasi yetu tunao wajibu wa kuyakemea ili kuufanya mchakato huu uende kwa haki:
Mosi, kauli ya Mh. Rais kuwasamehe wale watakaojiondosha kazini wenyewe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na wale watakaoendelea kubaki kwenye nafasi zao ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi.
Kisheria Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu anayetuhumiwa kufanya kosa la jinai iwapo mtu huyo hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuhukumiwa.
Madaraka pekee aliyonayo Mh. Rais ni kutoa Msamaha kwa wafungwa wanaotumikia kifungo (President's Prerogative of Mercy) kama alivyofanya hivi karibuni kwenye Sherehe za Muungano.
Iwapo tutaacha hulka ya viongozi kuchukua hatua wapendavyo hata kama kwa kusigina sheria za nchi basi tujue wazi tulipeleka taifa kwenye "Utawala wa Mtu Binafsi" badala ya "Utawala wa Sheria".
 
Lumumba hawatakosa la kuzungumza, ooh huyu kawa mpinzani, huyu anataka cheo, huyu ndumilakuwili nk.
 
Dr kulalamika ni aibu
Atoe mapendekezo ya mtumishi akifoji vyeti afanyweje kwa uchambuzi wake
Sasa utafanyaje reform utumishi wa umma kwa kukwepa ukweli kuwa wapo na waliofoji ambao hawakustahili kuwepo walipo
Naungana mkono nae kwenye suala la wanufaika wa kodi zetu kama mshahara wao lkn wametengwa kwenye zoezi wakiwemo wakuu wa mikoa, wilaya na Wabunge na mawaziri...
 
Au na yeye aligushi cheti cha form 4!!!sijamwelew hapa!!!wamegushi wamegushi basi!!huyo clinical officer akamtibu yeye!!!jamani reform yoyote ile lazima watu waumie!!!Hata Yesu alikubari kufa ili ulimwengu uokolewe!!!
Anasahau kuna wakati wa kichwa alioperetiwa goti na wa goti kichwa? Ni kutokana na huu ujinga wa kusema maadam anaweza kazi basi tusifuatilie kughushi kwake.

Yaani ni kama kusema maadam kafikikishwa kileleni basi ye atasahau kuwa alibakwa nae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom