Dr. Batilda Salha Buriani unayafanya haya kwanini?

Uislam unafundisha kuishi vema na watu...Mzee ES kachangia vyema asichkuliwe huyu kuwa KIOO...Waislam wana KIOO chao...ila kwa kuwa hizi ni TUHUMA lazima zithibitishwe...na kama kweli muanzishaji mada yupo serious basi airushe Mahakamani kama ilivyofanywa kwa MAHITA..naona week end imeingia na hakuna proved DATA...lkn pia ipo haja ya kujiuliza ni wangapi wanawanyanyasa wafanyakazi wao ndani?...
 
...watu wa anti human traffic wapo wapi......?? nasikiaga semina tu ..TAMWA???

HUYU binti kuna siku tumepanda naye ndege tukitoka mokoani ajiwa na kichanga chake...like 3 years baby girl..alikuwa peke yake nafikiri akitoka ziara light mkoani,i can relate it was somewhere august..sijui wakati huo akikuwa amekimbiwa na maids wake wote.....maana kwa mtoto wa umri huo ukiwa na maid mzuri unamwacha tu...tena afadhali watoto wa siku hizi enzi zetu ukiwa na mwaka mmoja na nusu ...unakuta tayari mama ana mdogo wako..na wala hana mpango na wewe ..unajikokota tu unajiokoteaga matunda .,wakati wa kula chakula kinawekwa mbele yako unajiliaga...ikifika miaka kumi unaenda kupimishwa mkono uingie la kwanza na bado unakataliwa ..kwani kaumbo kanaonesha bado hata miaka saba hujafika...lakini tumedunda tu..hayo ndio maisha ya watanzania tulio wengi...wakiwemo hawa mnaowaita mawaziri leo...sasa kweli kwa maisha hayo sijui utakuwa naroho gani kunyanyasa mtoto wa mkulima...aliyekuja kufanya kazi kwako kwa kuwa mazo yao yamekopwa na shule ameshindwa kwenda..au amekimbia kuolewa au kukeketwa...huruma hakuna???

Mkuu PM, heshima mbele kabisa, tatizo wamesahau. Ndio, wamesahau mkuu, kwamba na wenyewe wamepitia huko huko, lakini maadamu wapo kwenye ndege inayopaa sasa, hawawezi kukumbuka walikotoka!

Wamesahau mkuu ndio maan watu wanaokosoa mafanikio ya miaka 46 ya uhuru wanaitwa 'watu wabaya'....mwenye shibe hamju mwenye njaa!
Nadhani mheshimiw amesahau pia kuwa inapofikia mahali unajikuta unasafiri na mtoto wa miaka 3 kwenye safari ya kikazi, ujue tayari huiamini jamii inayokuzunguka...ni kwamba unaongoza watu usiowaamini na kwa hiyo 'umejifungia' ndani kwenye ulimwengu wako peke yako ambao 'umeutengeneza' kupitia hizi njia tunazopiga vita za ufisadi!
Mi nadhani uongozi/utawala ua raha kama umeupata kihalali, ukaongoza kihalali, ukaishi kulingana na maadili..hutahitaji kusafiri na mtoto..unaweza kumwachia raia mwema yeyote ukirudi unamkuta salama! ni mawazo yangu tu hayo........
 
Wamesahau shule zilizowaelemisha, wamesahau hospitali walikozaliwa, wamesahau miji walikokulia ndio ikawe mtoto wa mtu mwingine? Wamesahau wala hawataki hata kukumbushwa. Wanaona hao maids ni kama takataka tu na ndio maana hata hawataki kuwalipa inavyotakiwa.
 
Tunashukuru kwa kukua kwa technologia ya habari, mambo mengi siku hizi hadharani mara tu yanapotokea,,, yaani Tanzania itabadilika muda si muda... na wengine mlioko hapa mnaoota Kuwa Viongozi hakikisheni hamuachi alama za mabaya tutawapiga mabomu... ya aina ya BM52

Kilitime,
Yaani siku hizi naogopa sana- hata nikiona demu mzuri huwa macho mbele!
Du! Yaani kaazi sana!
 
Mzee ES kachangia vyema asichkuliwe huyu kuwa KIOO...Waislam wana KIOO chao...

Mkuu heshima mbele, unajua wananchi wanpaswa kuelewa maana ya dhamana ya uongozi kwa taifa, unapokuwa kiongozi unakuwa the role model kwa wananchi, sasa unapoamua kuwa mswalihina ili ujia-aline kisiasa na walioko kwenye power badala ya kujia-line na Mungu, unakosea kabisa, ni tabia ambayo sasa inaanza kuwa ni ya kawaida,

Ninawaona viongozi wetu wakienda kuhiji, wakienda Vatican kusafishwa na maji matakatifu, na kurudi bongo wakiendeleana maovu huku wakijiweka sawa kisiasa mbele ya waumini wa dini zao na viongozi flani ambao ni wanasiasa lakini waumini wa hizo dini zao, that is wrong kwa taifa maana kwa Mungu, watajijua wenyewe na Mungu wao, tatizo ni pale wanapojaribu kutudanganya wananchi, maana kama huyu mama ni mswahilina kiasi hataki wakristo wa-practice dini yao kwake, sasa inakuwaje anajirusha na mkristo?

That is all my concern, dini yake sijui na Mungu wake sijui lakini yaliyotokea kule kina mama kati yake na waziri ilikuwa aibu kubwa sana kwa waliojionea, maana haikuwa kwa ajili ya kazi ya taifa bali nani anatembea na nani lakini kwa the expense ya taifa letu, that I have a problem with and I don't care what, it is my dogon business!
 
Yaani tayari tushatoa hukumu kwa huyu mama based on one sided story..

Wako wapi watetezi wa mambo binafsi?
 
hapa ni chuki, majungu fitna na kwenda mbele.

data za kweli hamna

heeeeeeee heeeeeeeeeeee

hizi ndio fungia mwaka
 
data za nini yena wenye data si ndio hao wakipewa nafasi ya kufanya uchunguzi wanasema etii ohhh ripoti siri

hio haiondoi ukweli kuwa jamaa alibaka na yule binti alitumiliwa na mbaya zaidi jamaa sasa hivi ana skendo lingine lililo kavibaya ile kinoma

tazama hii picha...think you got a clue now

rkelly.jpg
 
Ingawa kila mtu anakuwa na imani yake. Tanzania bado ni nchi inayokubali na kuruhusu watu kufuata dini mbali mbali (ili mradi zinakubalika kisheria). Mheshimiwa kwa nini asitafute msaidizi wa ndani ambaye hawatapingani katika mambo ya imani? Lakini hili ni dogo. KUBWA NI WAZIRI KUWA NA MFANYAKAZI AMBAYE HANA MAKARATASI. NA KAMA ANAYO! JEE TUMEKOSA WA TANZANIA WA KUFANYA HIZO KAZI KWAKE? AU NDIO MA TX MPAKA MAJUMBANI? AU NDIO KULEWA MADARAKA?
 
Mengi yamesemwa haa lakini mimi mtoa hoja nasema huyu Mama ni Mbabe sana hata kwa Mama yake mzazi .Kuna siku Esther Mlokole mtumishi wake wa ndani alitoroka na kweknda kanisani na huyu mama aliamka saa 4 asubuhi na kukuta mlango uko wazi ndipo hapo alipotaka kumpelekea polisi kwa kudai kwamba ana njama ili aibiwe lakini akasahau kwamba Esther imani yake kwa Mungu wake ni zaidi ya kazi za ndani za Bi Salha. Bi Salha ameweza kumuungurumia Mama yake mzazi na kutishia kukata msaada hadi mama wa watu kaamua kuwa Muislam .kaacha ukatoliki.
Issue ya mgeni kuwa mtumishi wa ndani si siri nendeni kwake pale mtamuona na mtasema naye .Maana huyu dada amekula kiapo kwamba hataacha kwenda kanisani na Bi Salha ukitaja neno Yesu ndani ya compound yake anaweza kujinyonga kasahau kwamba kabadili dini kwa kuwa amempenda Mpemba wake huyu na kwamba ndugu zake kula daraja 2 hata wale Mama yake alio zaa na mzungu bado ni wakristo .Jambo la ubaguzi wa aina hii ikiwamo dini si jambo dogo hata mara moja . Lingalikuwa dogo kwa mtu ambaye hana madaraka na mamlaka lakini kwa hili nasema watetezi wake waje watueleze hapa .
 
Nakandamiza Kibara hio slogani yako ibadilishe Haina Ukweli..TFDA imewekwa kudhibiti nyie mnaoweka viduka vya dawa FEKI...please nikisoma posting zako..hicho kibwagizo chako naona kuna weakness KUBWA...Pia unapochangia TULIA.weka vituo na sentesi zenye kueleweka..una haraka ya nini?...
SI VEMA KUMTUHUMU MTU KWA JAMBO AMBALO HAKULIFANYA..kwa KANUNI za BINADAMU NA KIHISTORIA...UKIMSINGIZIA MTU JAMBO LOLOTE BAYA NA IKATHIBITI KUWA HANALO.BASI WEWE ULIETOA TUHUMA HUFI HADI NAWE LIKUKUTE...(Fanya utafiti)
Hizi Tuhuma za fulan kutembea na Fulan ni TATIZO JAMANI...HIVI kwanini hatuchukii ZINAA...UFISADI ktk NGONO na UFISADI ktk mali ya nchi hadi lini? Nakumbuka huko nyuma baadhi wa wachangiaji walisema FISADI wa NGONO hawezi kuipeleka nchi SALAMA..hata awe mtendaji kiasi gani lkn atavurunda...kwani ikiwa mtu ameshindwa kuwa muadilifu kwa mkewe au mumewe ktk MALI ya UMMA ataweza??????????
 
Hii mada nzito na pengine inaweza funga mwaka. Duh, huyu waziri kweli ama kuna mtu anayefanana naye maanake kilichonichosha zaidi ni pale alipozungumzia Ukristu hali ndio uliomkuza.
Nitamsamehe ktk ajira kwani wapo wengi wanaoyafanya haya. Maisha ya dada zetu hawa TX siku zote yamekuwa ktk utumwa, urithi mzuri tuloachiwa na mkoloni kwani sijawahi kumsikia kiongozi akizungumzia haki za hawa dada zetu - mama huyu hayupo pekee.
Swala la kusali nafikiri pia halina uzito mkubwa kwani sisi sote tumekuwa tukifanya kazi seriklini bila kupewa nafasi ya kwenda kusali ifikapo Ijumaa na huku majuu ndio kabisa hawaelewi. Ni maamuzi ya muumini kuacha kazi kwa sababu ya ibada ama kukubali kufuata matakwa ya mwajiri.
Lakini hili la kutukana imani ya mtu waziwazi hali ukijua kwamba ni makosa tena waziri mzimaa!.... duh, nadhani hao waajiriwa wote kwa pamoja inabidi waunde timu kufungua mashtaka mahakamani na swala hili lipatiwe ufumbuzi kisheria, hata kama atashinda lakini jina lake litakuwa limeingia tope na sidhani kama atarudia tena.
 
Chuma kibwagizo kitabaki na najua nisemelo maana nimesha deal nao hao kwa njia za uwazi na nikaishia mahapa ambapo nitasema when is right time . TFDA hawadhibiti kwa kiasi hicho usemacho na kama wanafanya basi ni kiasi kidogo na zaidi wanachukua Mulungula nina ushahidi wa kibwagizo hiki .Wacha kuharibu mada tafadhali na kama unataka kuwatetea fine anza mada nije huko nikumalize maana nina ushahidi mwingi sana .

Juu ya habari ya Bi Salha ni kitu ambacho kinakufanya useme ni tuhuma ?Kama ni tuhuma si ujibu basi badala ya kuboyongoka mkuu ?Tuhuma huwa zina ukweli wake na mimi nasema ukweli ni huu sasa wa yeye kuwa na Mmalawi ndani bila ya vibali na kuwadhulumu wasichana wa kazi na kuwazuia hata kumwabudu Mungu wao . Unataka nani aje aseme ndipo ujue ni kweli ? Lini CCM walisema hizi tuhuma ni za kweli ?Au unataka sasa kuomba pesa upite mikoani kusema madai ya uongo ama JF tuna beef naye ?Mbona imekuwa ni kawaida ya wakubwa kuanzia UK hadi US na TZ kuwatumikisha watu wao na wanakuwa wa kwanza kusimama na kusema haki sawa kwa wote na hata kuvaa t-shirt na kofia ili waonekana kama kuhamasisha Ukimwi na wakitoka hapo wanafanya kinyume ?We Chuma weeee au umetumwa kuja kumtetea ?
 
Mengi yamesemwa haa lakini mimi mtoa hoja nasema huyu Mama ni Mbabe sana hata kwa Mama yake mzazi .Kuna siku Esther Mlokole mtumishi wake wa ndani alitoroka na kweknda kanisani na huyu mama aliamka saa 4 asubuhi na kukuta mlango uko wazi ndipo hapo alipotaka kumpelekea polisi kwa kudai kwamba ana njama ili aibiwe lakini akasahau kwamba Esther imani yake kwa Mungu wake ni zaidi ya kazi za ndani za Bi Salha. Bi Salha ameweza kumuungurumia Mama yake mzazi na kutishia kukata msaada hadi mama wa watu kaamua kuwa Muislam .kaacha ukatoliki.
Issue ya mgeni kuwa mtumishi wa ndani si siri nendeni kwake pale mtamuona na mtasema naye .Maana huyu dada amekula kiapo kwamba hataacha kwenda kanisani na Bi Salha ukitaja neno Yesu ndani ya compound yake anaweza kujinyonga kasahau kwamba kabadili dini kwa kuwa amempenda Mpemba wake huyu na kwamba ndugu zake kula daraja 2 hata wale Mama yake alio zaa na mzungu bado ni wakristo .Jambo la ubaguzi wa aina hii ikiwamo dini si jambo dogo hata mara moja . Lingalikuwa dogo kwa mtu ambaye hana madaraka na mamlaka lakini kwa hili nasema watetezi wake waje watueleze hapa .

Hapa ndugu yangu nadhani umetuongezea chumvi kiasi kama si sana. Sidhani kama suala la mama yake kubadili dini linatokana na kukosa misaada, hiyo naona ni msimamo binafsi wa huyo mama. Unataka kuniambia miaka yote aliyoishi hadi kuzaa mtoto ambaye sasa ni waziri (na unadai kuna wengine aliozaa na mzungu), hakupata kuona vishawishi vingine vya kubadili dini, hadi aje "kungurumiwa" kwa tishio la kukosa misaada uzeeni? Huyo ndio mtoto pekee anayeweza kumsaidia huyo mama yake? Sidhani kama hili ni kweli. Shutuma za kunyanyasa mtumishi wa ndani, kuajiri mtu asiye na vibali na nyingine kama hizo, nadhani hayo kweli ni makosa kama kweli huyo mheshimiwa kayatenda, lakini hili la mama yake kubadili dini naona unapoteza mwelekeo wa mada. Huyo ni mama mtu mzima mwenye utashi wa kufuata msimamo wake wa kiimani anaoona unamfaa, sidhani kama anahusika kwenye hizi tuhuma zilioibuliwa dhidi ya mwanae.
 
Mengi yamesemwa haa lakini mimi mtoa hoja nasema huyu Mama ni Mbabe sana hata kwa Mama yake mzazi .Kuna siku Esther Mlokole mtumishi wake wa ndani alitoroka na kweknda kanisani na huyu mama aliamka saa 4 asubuhi na kukuta mlango uko wazi ndipo hapo alipotaka kumpelekea polisi kwa kudai kwamba ana njama ili aibiwe lakini akasahau kwamba Esther imani yake kwa Mungu wake ni zaidi ya kazi za ndani za Bi Salha. Bi Salha ameweza kumuungurumia Mama yake mzazi na kutishia kukata msaada hadi mama wa watu kaamua kuwa Muislam .kaacha ukatoliki.
Issue ya mgeni kuwa mtumishi wa ndani si siri nendeni kwake pale mtamuona na mtasema naye .Maana huyu dada amekula kiapo kwamba hataacha kwenda kanisani na Bi Salha ukitaja neno Yesu ndani ya compound yake anaweza kujinyonga kasahau kwamba kabadili dini kwa kuwa amempenda Mpemba wake huyu na kwamba ndugu zake kula daraja 2 hata wale Mama yake alio zaa na mzungu bado ni wakristo .Jambo la ubaguzi wa aina hii ikiwamo dini si jambo dogo hata mara moja . Lingalikuwa dogo kwa mtu ambaye hana madaraka na mamlaka lakini kwa hili nasema watetezi wake waje watueleze hapa .

sasa kama anachukia wakristo hivi amekubali vipi kuwa nyumba ndogo ya UCHUMI UNAPAA..na kama tunavyojua uchumi ni mkristo...au yupo mbioni kusilimisha na huyu???
 
Huyu Bi Salha Ni Mtu Wa Kiburi Sana Jaribu Hat Kukumbuka Siku Anatoa Hukumu Kwa Mh Zitto Alilkuwa Anatoa Kwa Madharau Sana Yote Hayo Yanaonyesha Kwa Kiasi Tu Jinsi Anavyoonekana Ktk Jamii. Sijui Watu Kama Hawa Wametokea Wapi Hadi Kuupata Na Huo Uwaziri. Hafai Kabisa Kama Ni Mtumishi Wa Serikali Anayejua Sheria Za Nchi Yatakiwa Amwombee Kibari Cha Kazi Huyo Mfanya Kazi Wa Ndani Ppia Amlipe Kulingana Na Viwango Vya Serikali Vilivyotangazwa Hivi Karibuni.
 
sasa kama anachukia wakristo hivi amekubali vipi kuwa nyumba ndogo ya UCHUMI UNAPAA..na kama tunavyojua uchumi ni mkristo...au yupo mbioni kusilimisha na huyu???

Habar hii bado haijakaa sawa hapa. Imekuwa ya kimajungu zaidi, kuliko kuwa ya kusadikika.
Kama huyu waziri ni 'MDINI' kiasi hicho kinachosemwa na mleta mada ni vipi aendelee kuwatafuta hao wakristo, tena na walokole wamlelee mwanae?

Nijuavyo mimi, Dar yetu hii, pwani, morogoro nenda hata kigoma, lindi, mtwara na kwingineko Tanzania nzima - asingeweza kumkosa mwislamu mwenzake, tena pengine mwenye msimamo imara (mkali) zaidi kumshinda yeye ili amlele mwanae katika maadili ya uislamu anaouona unafaa zaidi. Kote huko atakuwa hata amekosa mpagani mwenzangu, ambaye pengine angeweza kumfunulia wokovu, ili na yeye neema zimmwagikie zaidi?

Na ukiongeza hilo la mama yake kubadirishwa dini bila ya yeye kutakaa, kwa kuogopa kukosa ulaji, habari inazidi kuwa ya mvuruganyo tu. Nakandamiza Kibara, sio vizuri kuwazulia watu jambo; na hasa haya ya udini hayatusaidii kamwe.

Kama una-concrete information, licha ya hizi rasha rasha, iweke yote hapa watu wahukumu. Vinginevyo, achana nayo haya.
 
Back
Top Bottom