Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Katibu mkuu wa CCM, Dr Bashiru Ally amesema wale wote waliomtukana Mwenyekiti wa CCM, Dr. Magufuli bado wana kesi ya kujibu mbele ya kamati ya nidhamu ya chama.

Dr. Bashiru amesema wale walioomba msamaha na kusamehewa walifanya hivyo kama watu binafsi na Dr. Magufuli aliwasamehe kama mzazi lakini kwenye chama mashtaka yao yapo palepale na muda ukifika wataitwa kujieleza na kuchukuliwa hatua " rasmi" kwa namna itakavyoonekana inafaa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Chanzo: ITV habari!
 
Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza kutukanwa sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka.

Yani, katika watu ambao mtu anaweza kuwatukana vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais.

Wananchi wengine wote wanatakiwa kuwa na kinga ya kisheria dhidi ya kutukanwa kumpita rais.

Kwa nini?

Kuna msemo mmoja wa Kifaransa, wanasema "Noblesse Oblige". Maana yake ni kwamba, wanaopewa nafasi kubwa za kuongoza jamii, wanawajibika kubeba mzigo mkubwa zaidi".

Msemo huu unatoka katika Biblia. Bwana Yesu (namuongelea kama mwanafalsafa, si Mungu wala Mtume, kwa wale ambao watataka kurukia hili kuonesha namuamini kidini) alitoa mfano wa talanta katika kitabu cha Mathayo 25: 14 - 30.

Kwa kifupi, alisema kwamba, kama kuna watu vijakazi kadhaa, wamepewa mtaji na bwana wao wakafanyie kazi, wengine wamepewa mtaji mkubwa, wengine wamepewa mtaji mdogo, wakimaliza kufanya kazi zao, nani atadaiwa marejesho zaidi?

Aliyepewa mtaji mdogo atadaiwa arejeshe mapato zaidi ya aliyepewa mtaji mkubwa?

La hasha.

Aliyepewa mtaji mkubwa atadaiwa kurejesha mapato makubwa zaidi.

Kupewa uongozi wa nchi ni kupewa mtaji, mtaji mkubwa. Ukipewa mtaji mkubwa, utadaiwa kuleta mapato makubwa zaidi.

Unapogombea uongozi, inabidi ujitafakari. Ujiulize, mimi naweza mikiki ya public life? Nawez akuwa na ngozi ya mamba ya kutotetereka nikitupiwa mawe? Nina kifua cha kukaa na maneno? Kutojibu matusi kwa matusi?

Kama huwezi, usigombee uongozi.

Waswahili wanasema "ukubwa gunia la chawa". Walielewa kwamba ukubwa unamletea mtu matusi na kejeli, kufanya kazi bila kushukuriwa, lawama n.k.

Noblesse Oblige.

Hizi sheria za kukingia viongozi matusi (Lese Majeste), ni sheria za zama za kisultani an kifalme. Enzi za demokrasia, sheria hizi zimepitwa na wakati.

Hizi ni zama za uhuru wa kujieleza, si zama za censorship.

Rais anatakiwa kuwa mtu w amwisho kabisa kulindwa na sheria dhidi ya matusi.

Lese Majeste is not protection of leaders against insults.

No.

Lese Majeste is an insult to freedom of speech.
 
Safi kabisa,muda ukifika Hawa kina January na nape tutawapa udiwani ili liwe funzo kwa wengine.
Harafu na wale wahujumu walioomba msamaha nao tutadeal nao ndani ya chama wasidhani ndo yameisha hivyo,mpaka wanyooke Kama ubao wa mninga
 
Kiranga,
Uhuru wa kujieleza tusiujenge kwenye dhana hiyo. Utakuwa ni ujinga!

Matusi hayaleti masikilizano bali mifarakano tu. Mtu akikutukana maana yake hakuheshimu na hakuthamini, sasa nani anakusikiliza ukimtukana?

Hata humu JF tunajadiliana na kukosoana kwa hoja, siyo matusi. Sheria za hapa zenyewe haziruhusu lugha za hivyo kwa sababu hazina muafaka.

Matusi sio hoja wala shauri. Ni matusi. HAYAFAI.
 
Uhuru wa kujieleza tusiujenge kwenye dhana hiyo. Utakuwa ni ujinga!

Matusi hayaleti masikilizano bali mifarakano tu. Mtu akikutukana maana yake hakuheshimu na hakuthamini, sasa nani anakusikiliza ukimtukana?

Hata humu JF tunajadiliana na kukosoana kwa hoja, siyo matusi. Sheria za hapa zenyewe haziruhusu lugha za hivyo kwa sababu hazina muafaka.

Matusi sio hoja wala shauri. Ni matusi. HAYAFAI.
Matusi ni nini? Kipi ni tusi na kipi ni ukweli tu ambao rais hataupenda?

Unajuaje nikisema "John Magufuli ni mshamba wa kutupwa" hilo ni tusi la kumvunjia heshima mkuu wa nchi na ni haki nifungwe jela au ni ukweli ambao ni haki yangu ya kikatiba kuueleza?

Kati ya serikali na mwananchi, nani ana mzigo wa kuonesha hili ni tusi na hii ni haki ya kikatiba ya kujieleza tu?
 
Naunga mkono hoja, ila kanuni ya kutukana kwanza ni mtu yoyote anayemtukana mwingine, lazima huyu aliyetukanwa alalamike

Pili hilo linaloitwa ni tukano lazima liwe tukano kweli, mimi nimezisikiliza zile voice notes, kuna wengine wameomba tuu msamaha kwa vile wamemzungumzia rais na voice notes zao zika leak lakini hazina matukano yoyote.

Kwa vile aliyedai kutukanwa kesha samehe, who is he kuendelea kuwahoji?. Na kamati ya maadili inaweza kwanza ku establish matukano kwanza ndipo iwaite?.

P
 
Huyu nae hajielewi, sijui alisomea ujinga.
Akili zimekombwa
tapatalk_1558852188968.jpeg
 
Kwa comment hii , hawa ndio wanataka uhuru wa kujieleza
Hawa nani? Umetaja uhuru wa kujieleza, wewe unajua kujieleza?

Uhuru wa kujieleza ni nini?

Kwa mpango gani?

Tanzania hatuna hata sheria za kuongoza uhuru wa kujieleza.

Na tuna vinara waliopoka mchakato wa kutunga sheria.

Sasa utaniambia nini kuhusu uhuru wa kujiekeza kama hata definition ya uhuru wa kujueleza inabidi niipigie magoti kwa rais?

Na kama rais ndiye ana define uhuru wa kujieleza ni nini, akitaka kusema neno lolote la kumkosa haliwezi kuwa kwenye uhuru wa kujieleza, utapigaje hilo?

Do not pigeonhole me into your narrow fake morality universe.

I am bigger than that.
 
Back
Top Bottom