Dr. Bashiru. Viwanja vyote vya CCM vilivyopo katika maeneo yenu hakikisha vinapata hati halali ya umiliki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
DKT. BASHIRU ATOA MAAGIZO KWA MAKATIBU WA CCM WA MIKOA NA WILAYA

Leo tarehe 23 Novemba, 2019 Katibu Mkuu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally akiwa njiani akitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar Es Salaam amepita na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa CCM Kibaha Mkoani Pwani.

Akikagua ukumbi huo, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Makatibu wa CCM wa Mikoa Wilaya nchini kuhakikisha viwanja vyote vya CCM vilivyopo katika maeneo yao kuhakikisha vinapata hati halali ya umiliki. "Napenda kutumia wanachama na viongozi mliopo hapa kutoa maelekezo, viwanja vyetu vyoote nchi nzima ambavyo tumevitambua na tutakavyovinunua lazima vipate hati, na ninawaagiza Makatibu wa mikoa na wilaya nchi nzima wawasiliane na ofisi yangu, tumeshaweka utaratibu mzuri wa namna ya kumudu gharama kila kiwanja kiwe cha Chama au Jumuiya zake kipimwe na kipate hati kutegemea na maeneo kilipo, ardhi zote yawe mashamba, viwanja ni lazima tupate hati za kudumu za mila na za makazi" Dkt. Bashiru ameeleza

Aidha, Katibu Mkuu akizungumza na baadhi wanachama hao na viongozi waliojitikeza kumpokea, ameeleza kuwa, "Haya mafanikio makubwa yanayopatikana hata kabla ya kufika mwisho wa utekelezaji wa Ilani yetu ni kutokana na matokeo ya Serikali za CCM kutimiza ahadi zake na pia kuwa na viongozi shupavu na jasiri wanaofanya maamuzi sio maneno matupu". Hivyo kuwataka wananchi wote kuendelea kuwa na umoja na mshikamano katika kipindi hiki ambapo nchi inaendelea kujengwa kwa kasi kubwa kama ambavyo wanashuhudia ukamilishaji wa miradi mbalimbali yenye tija na manufaa makubwa.

Mapokezi hayo yamehudhuriwa na Wanachama na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Ndg. Ally Makao na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mama Assumpter Mshana.

Imetolewa na;
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI ( CCM)
jamhuridigital_20191123_10.jpeg
 
View attachment 1270455
Ninachompendea Dr Bashiru hafagilii kuvaa misare ya CCM....... kama makamanda wa Chadema misare hadi mahakamani!!!
 
Kuna siku yaja Watanzania watavirejesha kwa wananchi, vimilikiwe na halmashauri husika. Mali zote ardhi umiliki kabla ya mfumo vyama vingi.
 
Vina hati hivi, hivi hata sheria ya kumiliki ardhi unaijua huko chademani

State agent
Kuna siku yaja Watanzania watavirejesha kwa wananchi, vimilikiwe na halmashauri husika. Mali zote ardhi umiliki kabla ya mfumo vyama vingi.
 
ccm ni genge hatari sana nchini.. yaani viwanja walivyopora kutoka kwa wananchi hii leo wanaagiza vitafutiwe umiliki halali!!
 
DKT. BASHIRU ATOA MAAGIZO KWA MAKATIBU WA CCM WA MIKOA NA WILAYA

Leo tarehe 23 Novemba, 2019 Katibu Mkuu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally akiwa njiani akitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar Es Salaam amepita na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa CCM Kibaha Mkoani Pwani.

Akikagua ukumbi huo, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Makatibu wa CCM wa Mikoa Wilaya nchini kuhakikisha viwanja vyote vya CCM vilivyopo katika maeneo yao kuhakikisha vinapata hati halali ya umiliki. "Napenda kutumia wanachama na viongozi mliopo hapa kutoa maelekezo, viwanja vyetu vyoote nchi nzima ambavyo tumevitambua na tutakavyovinunua lazima vipate hati, na ninawaagiza Makatibu wa mikoa na wilaya nchi nzima wawasiliane na ofisi yangu, tumeshaweka utaratibu mzuri wa namna ya kumudu gharama kila kiwanja kiwe cha Chama au Jumuiya zake kipimwe na kipate hati kutegemea na maeneo kilipo, ardhi zote yawe mashamba, viwanja ni lazima tupate hati za kudumu za mila na za makazi" Dkt. Bashiru ameeleza

Aidha, Katibu Mkuu akizungumza na baadhi wanachama hao na viongozi waliojitikeza kumpokea, ameeleza kuwa, "Haya mafanikio makubwa yanayopatikana hata kabla ya kufika mwisho wa utekelezaji wa Ilani yetu ni kutokana na matokeo ya Serikali za CCM kutimiza ahadi zake na pia kuwa na viongozi shupavu na jasiri wanaofanya maamuzi sio maneno matupu". Hivyo kuwataka wananchi wote kuendelea kuwa na umoja na mshikamano katika kipindi hiki ambapo nchi inaendelea kujengwa kwa kasi kubwa kama ambavyo wanashuhudia ukamilishaji wa miradi mbalimbali yenye tija na manufaa makubwa.

Mapokezi hayo yamehudhuriwa na Wanachama na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Ndg. Ally Makao na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mama Assumpter Mshana.

Imetolewa na;
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI ( CCM)
View attachment 1270455
KANU walipokuwa madarakani walijimilikisha kiwanja na jengo la KICC lakini walipokonywa walipotolewa madarakani ni suala la muda tu CCM oyeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... mbona hili ni suala la dakika tu chama kingine kikikamata nchi! Watu walivyo na hasira, jambo la kwanza ni CCM kufutwa usiku huo huo wa kuapishwa rais mpya; nakuhakikishieni jambo la kwanza atakalofanya ni kukifuta hicho chama. La pili, ni kutupa mahabusu viongozi wote waliotokana na hichi chama hususan waliowatenda wengine ndivyo sivyo au kujilimbikizia keki ya taifa wao na maswahiba zao. Halafu jambo la tatu ni kurejesha serikalini mali zote zinazodaiwa kuwa za CCM.
 
Kuna siku hivi viwanja walivyopokonywa wananchi na CCM kuamua kujimilikisha, vitarudi kwa wamiliki halali bila ya kujali vina hata au havina hati.
 
... mbona hili ni suala la dakika tu chama kingine kikikamata nchi! Watu walivyo na hasira, jambo la kwanza ni CCM kufutwa usiku huo huo wa kuapishwa rais mpya; nakuhakikishieni jambo la kwanza atakalofanya ni kukifuta hicho chama. La pili, ni kutupa mahabusu viongozi wote waliotokana na hichi chama hususan waliowatenda wengine ndivyo sivyo au kujilimbikizia keki ya taifa wao na maswahiba zao. Halafu jambo la tatu ni kurejesha serikalini mali zote zinazodaiwa kuwa za CCM.
Kama walivyofanya Sudan kuvunja kabisa kile chama cha Bashiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo naona kuna watu wataandikisha majina yao kama mali zao believe me this is Africa

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom