Dr. Bashiru: Tanzania siyo ya waislamu au wakristo bali ni ya watu wa dini zote, wanasiasa acheni udini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,737
141,603
Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema Tanzania haina dini bali watu wake ndio wenye dini hivyo amewaasa wanasiasa kuacha udini.

Dr Bashiru amesema Tanzania siyo ya waislamu au wakristo ila ni e watu wa dini zote.

Dr Bashiru ameyasema hayo katika mashindano ya kuhifadhi kuruani yaliyofanyika wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Source channel ten tv!
 
Naona wateule kwenye nafasi nyeti wengi zaidi ni kutoka dini moja, dini nyingine tunaahidiwa kujengewa nyumba za ibada tu.

Kweli hapo tumebalansisha dini zetu!
 
Naunga mkono hoja, CCM imepata kiongozi mzuri anayekemea udini.

P
 
..anze na PROF.KABUDI anayehubiri ZABURI ktk shughuli za KISEREKALI.
Na awaambie wale wanaosalimia ''asalam aleko, bwana Yesu asifiwe'' waache
Huu ni udini wa hali ya juu sana, kwamba, Tanzania ni asalam aleko na akina Bw. Yesu asifiwe kwamba ndio wenye nchi. Ukiwa nje ya makundi hayo wewe si Mtanzania halisi

Hatukuwahi kusikia salam za aina hii huko nyuma. Hakuna hata siku moja kiongozi kama Nyerere au '' wanafunzi wake akina Salim, Msuya, Warioba, Malecela, Kingunge(RIP) n.k tuliwahi kuwasikia wakisalimia kidini

Huu udini umepamba moto nyakati hizi na Katibu mkuu alione hilo na alizungumzie mijini si Kondoa. Haya yanafanywa siku hizi bila aibu wala haya na yanaonekana ya kawaida tu

Tatizo, udini unaelezwa na wenye mapembe ndiyo maana anazungumzia vichochoroni Kondoa. Hii awamu imepalilia sana tatizo la udini .

Afadhali hata Bashiru amejitahidi kunyanyua ulimi na kusema lipo tatizo, afadhali

Wakikaa katika vikao awaambie matatizo ya kupanua udini na hizi salamu za kidini, bad

Pascal Mayalla
 
..anze na PROF.KABUDI anayehubiri ZABURI ktk shughuli za KISEREKALI.

Pascal Mayalla
No kutumia Qotes za Bible or Quraan au dini yoyote sio udini bali ni kuonyeshea what you believe in, kuonyeshea imani yako, hata Bungeni, Wabunge wengi huwa wana quote maandiko ya dini.

Udini unaozungumziwa ni preferential treatment ya dini fulani, mfano kwenye urais wa Tanzania, rais akiwa Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki.

P.
 
Unazungumziaje swala la wanasiasa kufuturisha.......huo siyo udini!
 
Mkuu ile dua inayosomwa bungeni ni sala au ni nini.. Maana Tanzania haiamini katika dini ila kuna maneno yanayodhihirisha wazi kwa kificho tumebase wapi.
 
Naunga mkono hoja, CCM imepata kiongozi mzuri anayekemea udini.

P
Mbona Hayati Baba wa Taifa alishakemea kwa hiyo wasiotekeleza ni Upinzani au Nani?
 
Na awaambie wale wanaosalimia ''asalam aleko, bwana Yesu asifiwe'' waache
Huu ni udini wa hali ya juu sana, kwamba, Tanzania ni asalam aleko na akina Bw. Yesu asifiwe kwamba ndio wenye nchi. Ukiwa nje ya makundi hayo wewe si Mtanzania halisi

Wakikaa katika vikao awaambie matatizo ya kupanua udini na hizi salamu za kidini, bad

Pascal Mayalla
Mkuu Nguruvi3, Salaam Aleykum na Bwana Asifiwe ni salaam zenye maana moja, amani na iwe kwenu, hivyo sio udini.

Hata neno Shikamoo ni salaam ya kitumwa kwa lugha ya Kiarabu kumaanisha niko chini ya miguu yako.

Udini mbaya ni ule udini wenye kuhatarisha amani na umoja wetu na sio hizi salaam za maamkizi.

P
 
Unazungumziaje swala la wanasiasa kufuturisha.......huo siyo udini!
Tatizo la watu wengi kama wewe unaangalia udini kwa jicho la Uislam na Ukristo
Tunapokemea udini tuna maana moja, kwamba, hata wasio na dini, mabudha, Hindu n.k. ni raia wa nchi hii na hawapaswi kutengwa kwa kauli za ''asarama aleko na Bwana Yesu''
Huo ndio udini

Kufuturisha si suala la udini likifanywa kwa nia njema. Ni utamaduni uliopo miongoni mwa Watanzania kwa miaka mingi. Na wala siyo huo tu hata kutoa zawadi za Krisma n.k. ni vitu vinavyoleta umoja wa kitaifa katika tofauti za dini.
Maeneo yanapotengwa kwa kuchoma miili kwa wahindi na mtu akaaliwa si udini

Sir Chande alipofariki, watu walialikwa kwenye mazishi yake yalihusisha ''cremation''
Hakuna udini kwasababu ni Mwaliko

Hili la wanasiasa kufuturisha ni udini kwasasa. Hapa utaona nina ji contradict kama nilivyoeleza awali. Tayari kumekuwa na nyufa za udini zinazojengwa na kupaliliwa na hizi salama za asalam aleko na Bw Yesu afisiwe. Siamini kabisa kuwa kufuturisha kwasasa ni kule kwa utamaduni wetu

Tayari kuna element za udini ambazo zinapaliliwa sana na wale wanaopaswa kuzikemea

Hivyo, kufuturisha kwa wanasiasa wa leo ni udini kwasababu tumepoteza thamani ya umoja wetu uliotufanya tusiangaliane kwa jicho la udini.

Ni kwasababu hiyo, at least Bashiru amesema! Jambo jema kwamba kuna mmoja miongoni mwao ameona tatizo

Na hili la asalam aleko na bw Yesu si la CCM tu, hata wapinzani wamenasa katika mtego huo

Tukemee hizi salam, je, nchi hii ni ya wote, dini ni suala la mtu na si agenda ya Taifa
 
Mkuu Nguruvi3, Salaam Aleykum na Bwana Asifiwe ni salaam zenye maana moja, amani na iwe kwenu, hivyo sio udini.

Hata neno Shikamoo ni salaam ya kitumwa kwa lugha ya Kiarabu kumaanisha niko chini ya miguu yako.

Udini mbaya ni ule udini wenye kuhatarisha amani na umoja wetu na sio hizi salaam za maamkizi.

P
Nakubaliana nawe kabisa. Hayo ni maneno yenye maana moja kabisa

Tanzania ya leo hayatumiwi hivyo. Ningeleewa kama mtu angesema amani iwe nayi

Tofauti kabisa utasikia ''kwa waislam asalama areko, kwa Wakristo bw Yesu asifiwe''

Hapa maana yake maneno ya amani iwe nanyi hayatumiwi kama yanavyojieleza
Kutaja waislam na Wakristo tayari kunachagua makundi. Kwa maana nyingine, vipi wasio na dini, wasio amini, mabudha , Hindu n.k. wanaangukia katika eneo gani?

Hivyo wakati nakubaliana nawe kuhusu maneno hayo na maana yake, napenda nikutaarifu kuwa Tanzania ya sasa imegubikwa na udini na salama areko na bw Yesu asifiwe hazitolewi vinywani kwa ni njema, ni kwa nia ya ''kisiasa'' inayolenga kugawa Taifa

Miaka 23 ya Mwalimu na mingine 15 ya wanafunzi wake hatukuwahi kusikia haya hata siku moja
leo imekuwa kama formula '' wasilam asaram aleko, wakristo bw yesu asifiwe''

Nilitegemea kama wanatakiwa watu amani, basi waseme '' Amani iwe nanyi sote''
Siyo ku dissect taifa kwa makundi ya waislam na Wakristo

Katibu mku Bashiru ameliona hilo na ndiyo maana tunasema, afadhali amenyanyua kinywa
 
No kutumia Qotes za Bible or Quraan au dini yoyote sio udini bali ni kuonyeshea what you believe in, kuonyeshea imani yako, hata Bungeni, Wabunge wengi huwa wana quote maandiko ya dini.

Udini unaozungumziwa ni preferential treatment ya dini fulani, mfano kwenye urais wa Tanzania, rais akiwa Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki.

P.
Mkuu P, katika mawasiliano kuna vitu kadhaa, nitaongelea viwili
Kuna message na Messenger
Message inaweza kuwa mbaya sana ikatolewa na messenger mzuri na kusiwe na tatizo
Message inaweza kuwa nzuri sana ikatolewa na messenger mbaya ikawa ni tatizo

Nyerere aliyekuwa na kipaji cha message na kama messenger alitumia vitabu vya dini kwa njia nzuri sana. Always alikuwa anasema ''kuna kisa kimoja ...halafu anakielezea''

Kutumia maneno ya dini katika kusisitiza au kufafanua jambo si jambo baya
Imekuwa inatumiwa katika kuhuisha ujumbe

Tatizo linalojitokeza siku hizi si ''message kutoka katika bible au Quran''
Tatizo ni Messenger wanaopeleka message kwa receivers

Kiongozi anasema hivi ''Kwasisi tunaoamini biblia....'' hapa tayari keshatengeneza kundi kwa wao. Au utasikia '' Sisi Waislam....'' hapa tayari keshatengeneza kundi sisi
Hivyo maneno sisi au kwasisi tayari yanatenga jamii bila kujali message

Hoja yangu hapa ni kuwa message si tatizo, messengers ni matatizo makubwa

Hawa wanasiasa ndiyo messenger kwa bahati mbaya hawa si akina Sitta, Warioba, Amir Jamal, Al nur Kassam, Warioba, Msuya, Malecela, Sokoine n.k.

Hawa wa siku hizi ni wale aliosema Bashiru, Taifa limeshindwa kuwaaanda

Kwahiyo hoja nzima ina resonate katika maeneo mawili, message ambayo haina tatizo lakini messenger wetu ni matatizo kweli kweli. Hawa ndio wanaotumbukiza message kwa udini na kulifanya suala zima lichukue sura ya udini.
 
Back
Top Bottom