Dr Bashiru: Suala la Umoja ndani ya CCM ni la lazima siyo hiyari, asiyetaka Umoja tutamfukuza mara moja

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema swala la umoja ndani ya chama ni la lazima na mwanachama yoyote atakayekuwa na viashiria vya kutotaka umoja atafukuzwa chamani mara moja.

Ili kuwagundua wabinafsi Dr Bashiru amesema chama kitafuatilia mienendo ya wanachama wake na ikibainika unataka kutugawa Tutakutimua mara moja.

Dr Bashiru ameyasema hayo mjini Bukoba akiwa kwenye ziara ya kuimarisha chama.

Source Star tv habari!
 
Ukimsoma vizuri Dr. Bashiru haongelei umoja, bali analazimisha ukondoo kwenye chama chao. Umoja anaomaanisha yeye ni kutii chochote kinachooamuliwa na mwenyekiti na genge lake. Na kwa mtazamo wake na waliomtuma, yeyote mwenye mtazamo tofauti na genge la mwenyekiti huyo sio mmoja wao.
 
Bila CCM imara na yenye umoja nchi itayumba hivyo CCM kuwa moja maana yake ni nchi kuwa imara. Maneno ya Dkt. Bashiru yàmejaa hekima na iliyobeba matarajio makubwa kwa Tanzania
 
Mnapoambiwa kuhusu chama chenu mnalialia kama kasuku, kumbe huwa mnafuatilia ya CCM? Sasa ya ngoswe yanawahusu nini nyinyi mliojipambanua kwamba mnapinga kila kitu anachofanya JPM? Poleni kwa maumivu ya Mbowe hadi ang'oke wakati mtakapokuwa vikongwe.
 
Tofautisha umoja na ukondoo, hivyo ni vitu viwili tofauti. Ccm haihitaji umoja maana nguvu halisi ya ccm sio umoja, bali ni madaraka ya mwenyekiti wake kupitia kofia ya urais. Unahitaji vipi umoja ambapo mwenyekiti wa ccm anaweza kuagiza mamlaka zote zimtangaze mgombea wa ccm kushinda, au chaguzi kunajisiwa na kusiwepo na hatua yoyote? Kinachohitajiwa ndani ya ccm ni ukondoo tu wa kutii matakwa ya mwenyekiti na genge lake.
 
Mnapoambiwa kuhusu chama chenu mnalialia kama kasuku, kumbe huwa mnafuatilia ya CCM? Sasa ya ngoswe yanawahusu nini nyinyi mliojipambanua kwamba mnapinga kila kitu anachofanya JPM? Poleni kwa maumivu ya Mbowe hadi ang'oke wakati mtakapokuwa vikongwe.

Hujui hata unaongea nini, jambo lolote likiletwa huku jukwaani kila mtu anaweza kulijadili apendavyo. Kuna mtu umemuona kaenda kusimama nje ya mlango wa ofisi za ccm anafuatilia kinachoendelea humo? Mzuie aliyeleta mada ya ccm humu ndani, uone kama kuna mtu atakwenda kwenye ofisi za ccm kuulizia chochote.
 
Hujui hata unaongea nini, jambo lolote likiletwa huku jukwaani kila mtu anaweza kulijadili apendavyo. Kuna mtu umemuona kaenda kusimama nje ya mlango wa ofisi za ccm anafuatilia kinachoendelea humo? Mzue aliyeleta mada ya ccm humu ndani, uone kama kuna mtu atakwenda kwenye ofisi za ccm kuulizia chochote.

Hiyo sio issue mkuu naongelea comments ambazo mara kwa mara umekuwa unakejeli kwa nini nina-comment wakati mimi nilisema sio Mwanachama wa Chadema na nikakupa mfano kwamba wakati wa kupiga kura na wakati vyama vinajinadi huomba kura kwa kila Mtanzania.

BTW vipi umekula sikukuu vyema? Mwaka ndio unakwisha hivyo!
 
Sina popote ninapomzuia yoyote kujadili chama chochote, kiwe cdm au hata chama cha walemavu. Hili ni jukwaa huru, yoyote anaweza kujadili chochote, na ukipotosha tutakuambia acha kupotosha na utapata dozi stahiki.

Kwakweli sikukuu imeenda vizuri japo ukata uko palepale. Mwaka tunaungoja huenda hali ikawa afadhali kuliko mwaka huu. Nashukuru kwa salamu ya sikukuu!
 
V
Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema swala la umoja ndani ya chama ni la lazima na mwanachama yoyote atakayekuwa na viashiria vya kutotaka umoja atafukuzwa chamani mara moja.

Ili kuwagundua wabinafsi Dr Bashiru amesema chama kitafuatilia mienendo ya wanachama wake na ikibainika unataka kutugawa Tutakutimua mara moja.

Dr Bashiru ameyasema hayo mjini Bukoba akiwa kwenye ziara ya kuimarisha chama.

Source Star tv habari!
Mwulize barua za wale jamaa lini?
 
Bashiru ajifunze Siasa toka kwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete

Heka heka zote za Lowassa aliweza kwenda nazo mwanzo mwisho bila ya kufukuza wala kusimamisha Uanachama hata mmoja

Siasa za Darasani na za Field ni kama mbingu na Ardhi
 
Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema swala la umoja ndani ya chama ni la lazima na mwanachama yoyote atakayekuwa na viashiria vya kutotaka umoja atafukuzwa chamani mara moja.

Ili kuwagundua wabinafsi Dr Bashiru amesema chama kitafuatilia mienendo ya wanachama wake na ikibainika unataka kutugawa Tutakutimua mara moja.

Dr Bashiru ameyasema hayo mjini Bukoba akiwa kwenye ziara ya kuimarisha chama.

Source Star tv habari!
Inaonekana kuna fukuto huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom