Dr Bashiru Katibu Mkuu wa CCM; Prof. Mkumbo Katibu Mkuu Wizara ya maji-hali ya maji mwanza kama mlivyoiacha

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,222
5,946
Leonard Mapuli
2 hrs ·

SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA.
Nilijipa muda kuangalia endapo mamlaka ya maji Mwanza watabadilika na kuifanyia kazi ''issue'' ya maji ambayo Kwa sasa Mwanza ndio kero kubwa kuliko hata umeme.

Baada ya subra yangu ya takribani juma zima nimegundua mamlaka hii haina habari na wananchi,umevaa Miwani ya Mbao na imeamua jambo moja tu la ''Acha walie,watazoea''.

Gharama za maji zipo juu,sehemu kubwa ya watu huduma ya maji imekata kabisa,miundo mbinu ya maji mingi imekufa,mamlaka imebaki kutoa majibu mepesi katika jambo gumu linaoumiza wananchi moja Kwa moja,na wanahasira nalo.

Mwauwasa badala ya kuona namna ya kijitathmini na kuwa sehemu ya suluhu ya kadhia hii sasa wameanza kuumana wao kwa wao.Tunawaangalia tu.

Kama kuandika tumeandika sana,na tunaendelea kuandika kuwa Mwanza kuna shida ya Ankara za maji,na huduma za maji Kwa ujumla zimedorora sana,na ni maumivu makali Kwa wananchi wengi wa Mwanza.

Ukerewe ule mradi wa maji uko hoi,pampu zimekufa,naambiwa ni pampu moja tu inayofanya kazi.Pampu za hapa mjini ziko hoi hazisukumi maji na maeneo mengi hayana maji Kwa muda mrefu sasa.
Mwisho ni hivi,KILIO NI KIKUBWA,ila spika zimekatwa waya,Kanda inazunguka tu.

Mwambieni Dkt Bashiru kuwa wanamwanza walimwambia kero hii kubwa maana chama anachokatibu ndicho kilichopo madarakani na ndicho chenye kusimamia maendeleo na ustawi wa watu,mpaka sasa hakuna majibu licha ya kumtuma Katibu mkuu wa wizara ambae nae akaja kupiga siasa zilizopitwa na wakati kwa kumezeshwa mafanikio hewa na mamlaka husika akajikuta anacheza ngoma ya MWAUWASA badala ya ngoma ya serikali kuu.Dkt Bashiru ukisoma andiko hili popote fanyia kazi,usipofanyia kazi,basi anguko la chama chako Kwa Mwanza litaanzia uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa,maana kimeshindwa kutatua kero ya maji katikati ya maji.

Kero hii iliyojaa usumbufu Kwa walio wengi na wanyonge itatumiwa Kama TURUFU na vyama vya upinzani maana CCM imeshindwa tayari na inakumbatia watendaji corrupt wanaoiangusha serikali makusudi.
Mapuli
N:B

Picha (Facebook) picha ambatanishwa ni moja ya vibanda vya kutoa huduma ya maji Kwa umma ambacho Kwa sasa kinatoa huduma ya kuchaji simu.
Image may contain: tree and outdoor


19
 
Vipi ile sakata la waandishi na chama chao kupewa wali na posho ili kuibeba Mamlaka yenu ya maji MWAWASA limeisha?
Au kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake? Hayo mambo sio huko Mwanza tuu hata hapa Dar yapo?
 
Wizara ya maji inaongoza kwa kula rushwa. Miradi inamalizika kwa gharama kubwa kuliko wizara zote, ukabila umepamba moto, tenda zikitangazwa ni rushwa tupu. Maafisa maji na mabonde ni wale wala rushwa wakubwa.
 
Back
Top Bottom