Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,516
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dr. Bashiru Ally Kakurwa amesema kuwa kwasasa, kinyume na inavyosemwa na kudhaniwa, ndani ya CCM hakuna mpasuko wala mgogoro wowote ila kuna wapiga kelele wanaojaribu kupenyeza mambo yao binafsi kwenye chama hicho.
Dr. Bashiru alikuwa akihojiwa na Mtangazaji Deo Kaji Makomba wa Radio DW kwenye kipindi cha mchana huu cha Kinagaubaga jijini Dodoma. Kuhusu Waraka wa Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM, Dr. Bashiru amesema kuwa CCM hufanya kazi zake kwa mujibu wa vikao vya kichama vinavyoratibiwa na Katiba, Kanuni na Mazoea ndani ya CCM.
Dr. Bashiru amesema kuwa kwasasa CCM imeimarika, inaaminiwa na kuheshimiwa zaidi na wanachi kwakuwa inasimamia na kufanya mambo mazuri kwa Taifa hili na kwakuwa imeaminiwa na wananchi kupitia kura zao kuongoza Serikali mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dr. Bashiru alimaliza kwa kuwatoa hofu wanachama na wananchi wote kwa ujumla juu ya uwepo wa mgogoro au mpasuko ndani ya CCM. Amewaita wanaotajwa kuwa na mgogoro au mpasuko kuwa ni wapiga kelele na ambao wanataka kuufanya 'upuuzi' wao uaminike kama mgogoro ndani ya CCM.